KIKAO cha Kikundi cha Waishio na Vrusi vya UKIMWI na Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na UKIMWI Kitangari chaleta changamoto.
Kikao hicho kilichofanyika tarehe 20 Agosti,2010 katika ukumbi wa kituo cha Afya Kitangari chini ya mlezi wake Ndg.Florence Mnipa, kimeeleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wana mtandao hao.
Kubwa kabisa ni pale walipomwelekeza Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na Ukimwi Kitangari kwamba jamii inayowazunguka inawanyanyapaa.
Mkurugenzi alihitaji kujua ni kwa kiasi gani unyanyapaa upo kwenye makazi yao.
Maelezo waliyoyatoa walisema,kwa wale wanaotoka Kata ya Malatu idadi yao wapo wengi lakini wanaojitokeza ni 11 tu wengine hawajitokezi kuchukua dawa za ARV sababu kila wanaporudi Hospitalini mitaa wanayopita huwapachika majina ya dhihaka kama; wasanii,wafiwa watarajiwa.
Pia kwa wale wanaotoka Kata ya Maputi unyanyapaa upo kwa kiasi kikubwa,jambo ambalo linafanya hata wataalamu wa afya wanapohitaji kufanya uhamasishaji wa kupima Damu inakuwa ngumu kwa jamii.
Ombi lililotolewa na Mtunza hazina wa mtandao wa waishio na VVU Ndg.Saidi Shamba mwenye picha hiyo hapo kulia,alisema itolewe elimu kwa jamii ili waelewe na kuelimika kuhusu umuhimu wa kuwajali waishio na VVU kusudi walioanza Dozi wasikatishwe tamaa ili kuokoa vifo vinavyotokea kabla ya wakati wake kutimia.
Ombi la kutolewa Elimu kwa Jamii liliungwa mkono naMw/Kiti wa Kikundi hicho cha waishio na VVU Ndugu Fakihi Mwarabu mwenye picha hiyo hapo kulia.
Pia wajumbe, picha hapa chini walionesha kukerwa na tabia wanayowafanyia wenzao kwenye makazi wanakoishi ya kuwanyanyapaa.
Wajumbe hao kwa pamoja wamesisitiza sana kuomba wafadhili ili wasaidie kutolewa kwa Elimu kwa jamii ili kutokomeza tabia ya kuwanyanyapaa.
Katibu wa kikundi hicho Ndg.Asia Mtavala anayeonekana kwenye picha kulia naye aliwakumbusha wenzake wawe na utaratibu mzuri wa kufuata masharti wanapoendelea na Dozi katika kipindi hiki,tabia ya kukatisha Dozi wanapojisikia nafuu si mzuri sababu dawa inajenga usugu kwa Virusi pia wanaovuta sigara na kunywa pombe waache alisisitiza katibu.
Mwisho alimalizia kwa kusema kijiji anachotoka yeye anaitwa ukubwa wa mbuyu unyanyapaa upo kiasi kikubwa tena kinaudhi sana.
Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na UKIMWI Kitangari amewaambia wana mtandao waishio na VVU kwamba atashirikiana nao ili kwa kuanzia kupunguza kasi ya unyanyapaa hata kama si kuziba maneno machafu hayo, lakini yapungue.
Mkurugenzi alisikitishwa na tabia ya unyanyapaa kuendelea kubaki katika Tarafa ya Kitangari.
Comments (1)
Jambo waliloomba waviu ni kwamba jamii iache kuwanyanyapaa ili kuwawezesha kujisikia vizuri na huru.