Envaya
SI KILA UVIMBE NI SARATANI

Uvimbe ni nini?
Uvimbe ni ukuaji wa chembe hai za mwili(seli) usio wa kawaida na ambao hauwez kudhibitiwa na mwili.
  Ukuaji huu huusisha kuaribika wingi(namba) pamoja na umbo la chembe hai za mwili.
    
  KUNA AINA NGAPI ZA UVIMBE?
       Zipo aina mbili za  uvimbe nazo ni 
            (a) Uvimbe  usio na madhara(Benign)
             (b) Uvimbe wenye madhara. (Malignant).

(a) UVIMBE USIO NA MADHARA.
          .Aina hii ya uvimbe ukuaji wake ni wa taratibu ukilinganisha na ule wenye madhara.
           .Pia uvimbe wa aina hii hausambai kutoka eneo moja la mwili na kwenda eneo lingine la mwili.
        NB. Uvimbe usio na madhara huwe za kubadilika na kuwa wenye madhara .

(b) UVIMBE WENYE MADHARA.
       . Uvimbe wa aina hii pia huitwa Saratana au Kansa.
        .Pia aina hii ya uvimbe hukua kwa haraka zaidi ukilinganisha ukuaji wa chembe hai (seli) za kawaida za mwili.
        .Pia uvimbe huu  huweza kusambaa kutoka eneo moja la mwili mpaka lingini.

NB. Sio kila kansa lazima iwe imevimba. 
Kansa nyingine zaweza kuwa na mabadiliko tu ya umbo na namba ya chembe hai (seli) mfano kansa ya damu hauvimbi popote.
       
      JE, NITAJUAJE IKIWA UVIMBE WANGU NI WENYE MADHARA(Saratani) AU HAUNA MADHARA?
       Haiwekani kuutambua uvimbe kama ni saratani au si saratani kwa kuutazama kwa macho peke yake .Ili kuuthibitisha huitaji vipimo maalumu ambavyo hupatikana katika maabara za afya hivyo nenda hospitali ya jiran ili kuthibitisha.
  
   JE NI MAMBO AU VITU GANI HUWEZA KUNIWEKA KATIKA HATARI YA KUPATA SARATANI(Kansa)?
      .Uvutaji wa sigara, huweza kusababisha kansa za mapafu,mdomo na koo.
      .Utumiaji wa vyakula vya mafuta kwa wingi, huweza kusababisha kansa  ya utumbo. 
       .Kuanza mapenzi katika umri mdogo pamoja na kuwa na wanaume wengi huongeza hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.
       .Unywaji wa pombe uliopindukia huweza kusababisha magonjwa ya ini na baadaye kansa ya ini.
       .Historia ya saratani katika familia au ukoo,watu walio katika familia zenye historia ya kuwa na mgonjwa wa kansa wana hatari pia ya wao kupata kansa.
        .Mionzi mfano ya jua huweza kusababisha saratani ya ngozi hususani kwa Albino.
      Zipo nyingi sana nitazidi kuwafahamisha kupitia facebook page ya Tacaso.
      
JE  NIFANYE NI  ILI NIPUNGUZE HATARI YA KUPATA KANSA?
   . Ukitazama vizuri  mambo yanayoweza kuongeza hatari ya kupata kansa utaona yanahusiana na aina ya mfumo wa maisha , vinywaji na vyakula ambavyo wengi tunavipenda ili kuepuka hatari hii ni vema tukapunguza au kuacha matumiz ya vitu hivyo mfano sigara,  pombe ,kushea mapenz nk.
     .Pia inashauriwa kutumia vyakula vya mboga na matunda kwan tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwa aina hii ya chakula inauwezo mkubwa wa kupunguza hatari ya saratani ya utumbo.
      .Ikiwa ni Albino basi ajikinge na mionzi ya jua mfano kwa kuepuka kutembea au kufanya kaz juani kwa muda mrefu pia kuvaa mavaz ambayo yatamkinga kama kofia nk.
       Pia tunashauriwa kufanya mazoezi ya mwili angalau dakika30 kunasaidia kupunguza hatari ya kupata saratani.

SASA UMEJUA KUA SIO KILA UVIMBE NI SARATANI MWAMBIE NA MWENZIO. 
  References
    .Pathologic Basic of diseases.by Michael Kumar,Abbas Fausto.
     .Principle and practise of Radiotherapy.
       .Internet sources. 

November 28, 2014
Next »

Comments (1)

DANIEL MGEYEKWA (Tabata) said:
Je ninaweza kutibiwa kansa ya tumbo ya stage 1 bila upasuaji.
May 15, 2017

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.