Envaya

VIFUNGASHIO LEBO NA ELIMU YA MASOKO NI VIKWAZO KWA WAJASIRIAMALI TANZANIA

TUMPALE MWAKASANGULA (DODOMA)
April 6, 2017 at 1:39 PM EAT

Ni ukweli ulio wazi kuwa kila mteja atapenda kununua bidhaa iliyofungashwa vizuri na yenye lebo ya kuvutia, Ni kweli pia kuwa bidhaa hata iwe nzuri vipi kama imefungashwa vibaya haiwezi mvutia mteja yeyote yule.

Nayaandika haya ndugu zangu kwakuwa nchini mwetu hatuna bidhaa hiyo na mara nyingi hata ukitaka kuagiza nchi za nje unatakiwa uwe na mtaji mkubwa pengine wa kontena zima. Vilevile wajasiriamali wengi wadogo wa Tanzania hawana uelewa mpana wa namna ya kutumia mitandao kama vile intaneti kupata wauzaji wa vifaa hivi.

Elimu ya namna ya kuteka masoko mbalimbali ya ndani na nje imekuwa haitolewi sana hasa kwa wafanyabishara wa vijijini amako ndiko organization hii ya PRETTY inatulenga.

Ombi langu kwa Pretty ni moja tu kwamba kama mmeweza kutuletea huduma hizi tunaomba sana pia tupate vifungashio mbalimbali kwa kadri ya mshine mnazozitengeneza.

Ombi langu kwa wajasiriamali wenzangu ..! tuungane tuinuke tutafute elimu ya jinsi ya kutumia TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) tushiriki kwenye warsha na makongamano mbalimabli huko tutatengeneza (network) na tutaonana na watu waliotutangulia kiuchumi nao watatusaidia kutupatia taarifa mbalimbali ambazo kwetu zitatusaidia.

 

Ahsante sana

 


Add New Message

Invite people to participate