Envaya

NAFASI ZA KAZI KWA MAAFISA MASOKO

MAAFISA MASOKO WAANDAMIZI 70 NA MAAFISA MASOKO 200 WANAHITAJIKA Asasi ya Pretty Development for Poverty Reduction (PDPR) inayojihusisha na kutoa huduma za jamii, mafunzo, ushauri, ufugaji wa kuku, samaki na nyuki inazo nafasi za kazi kama ifuatavyo;
Maafisa masoko waandamizi 70.
Asasi ya Pretty Development for Poverty Reduction inataka kuajiri Maafisa masoko waandamizi wenye ujuzi na wachapakazi. Bidhaa zinazouzwa na huduma zinazotolewa na kampuni ni pamoja na mashine za kutotolea vifaranga vya kuku, mizinga ya nyuki, vifaranga, miche ya matunda na mbao, Ushauri wa biashara, semina za ujasiriamali, kuandaa michanganuo,fursa za kilimo biashara na ufugaji wa kuku, samaki, nyuki, sungura, na mikopo ya mashine na vifaa vingine.

Kazi zake;
1.Kuandaa mikakati ya mauzo na malengo ya mauzo kwa kampuni
2. Kutafuta masoko na kuuza bidhaa za kampuni
3. Kutangaza bidhaa za kampuni na kutafuta wateja.
3. Kusimamia na kuongoza maafisa masoko walio chini yake.
4. Kuandaa semina.
Sifa za muombaji;
Awe na shahada ya Biashara mchepuo wowote.
Siyo lazima kuwa na uzoefu kazini lakini akiwa na uzoefu wa kufanya kazi hizi kwa muda wa kuanzia mwaka mmoja na zaidi atafaa zaidi.
Mshahara;
Mwombaji atakayepata ajira atalipwa asilimia 20% ya mauzo atakayofanya kwa mwezi.

Maafisa masoko 200.
Asasi ya Pretty Development for Poverty Reduction inataka kuajiri Maafisa masoko wenye ujuzi na wachapakazi. Bidhaa zinazouzwa na huduma zinazotolewa na kampuni ni pamoja na mashine za kutotolea vifaranga vya kuku, mizinga ya nyuki, vifaranga, miche ya matunda na mbao, Ushauri wa biashara, semina za ujasiriamali, kuandaa michanganuo,fursa za kilimo biashara na ufugaji wa kuku, samaki, nyuki, sungura, na mikopo ya mashine na vifaa vingine.


Kazi zake;
1. Kutafuta masoko na kuuza bidhaa za kampuni
2. Kutangaza bidhaa za kampuni na kutafuta wateja.
3. Kuandaa semina

Sifa za muombaji;
Awe na elimu ya Kidato cha nne na kuendelea, mwenye kujituma ambaye anaweza kuuza .
Akiwa na cheti au shahada ya Biashara mchepuo wa masoko atatufaa zaidi.
Siyo lazima awe na uzoefu katika kazi lakini kama ana uzoefu wa kufanya kazi katika makampuni ya usambazaji wa bidhaa atatufaa zaidi.

Mshahara;
Mwombaji atakayepata ajira atalipwa asilimia 15% ya mauzo atakayofanya kwa mwezi.

Kwa maelezo zaidi piga simu 0754397178 au tuma maombi kwa email; pdprngo@gmail.com
IMMA SALINGWA
MKURUGENZI MTENDAJI PDPR Njombe. www.envaya.org/pdpr

July 5, 2015
« Previous Next »

Comments (18)

Issabelah Samwel mlay (Dar es Salaam) said:
hello, I read your activities and inspire me a lot. I want to know one thing from you. are you operating in Njombe only or you can implement your project in other areas? I want to deal with fishing activities but I stay at Dar es Salaam. check if we can do the business together.
Regards

Issabelah S. Mlay
July 13, 2015
PRETTY DEVELOPMENT FOR POVERTY REDUCTION (via email) said:
we operate whole national, for more information call 0754397178, 0652556833
July 13, 2015
gustavo thomas (shinyanga) said:
naitwa gustavo nipo shinyanga naulizia kuhusu hizo kazi nipataje na mimi nipo shinyanga hahitaji kuwa mtu wa masoko,elimu yangu ni astashahada ya uongozi na uhasiau
July 15, 2015
PRETTY DEVELOPMENT FOR POVERTY REDUCTION (via email) said:
Piga simu 0754397178, 0754397178 Tuma maombi yako kwenye pdprngo@gmail.com
July 15, 2015
JOHN PROSPER (Dar es salaam) said:
Nimevutiwa sana na swala la ufugaji wa kuku na utotoleshaji wa vifaranga hasa kwa mashine za mafuta ya taa.
ila mm ni civil engineering technician.naweza na mm kuaply?
August 4, 2015
PRETTY DEVELOPMENT FOR POVERTY REDUCTION (via email) said:
ndiyo unaweza kununua au kuomba mkopo kwa maelezo zaidi piga simu
0754397178, 0652556833 utahudumiwa.
August 4, 2015
JOHN PROSPER (Dar es salaam) said:
Nashukuru kesho tutawasiliana kwa ajili ya clarification zaidi.
August 4, 2015
gustavo mnemele (via email) said:
mnaweza kunifunza jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala?
August 6, 2015
PRETTY DEVELOPMENT FOR POVERTY REDUCTION (via email) said:
Ndiyo kitabu kinauzwa elfu 3000 pamoja na DVD ila ukinunua mashine
vyote bure mashine inauzwa TSH: 160,000
August 6, 2015
gustavo mnemele (via email) said:
kwahyo kitabu na dvd jumla elfu tatu.
August 7, 2015
PRETTY DEVELOPMENT FOR POVERTY REDUCTION (via email) said:
Kila kitu ni 3000/=
August 7, 2015
gustavo mnemele (via email) said:
so dvd 3000 na kitabu 3000,kama ni hvyo naomba unisaidie unitumie
vyote kitabu na dvd cna mtaji kbsa naomba unisaidie ndugu yangu
August 7, 2015
ABDUL CHOROBI (DAR ES SALAM) said:
Naitwa abdul chorobi naiishi dar na nasomea shahada ya ukadiliaji wa gharama za ujenzi(QS) naulizia mashine ya kufyetulia tofari shiling ngapi na nahitaji kuwa wakala
August 22, 2015
PRETTY DEVELOPMENT FOR POVERTY REDUCTION (via email) said:
laki 4
August 22, 2015
MARIA DITRICK (LUPONDE NJOMBE) said:
Naitwa Maria Ditrick ,toka Luponde Njombe.Naomba kazi ya Afisa Masoko. Asante.
August 30, 2015
PRETTY DEVELOPMENT FOR POVERTY REDUCTION (via email) said:
Naomba unitumie annuani ya barua pepe yako, pia unaweza nipigia simu
0754397178, 0652556833 Nikutumie fomu ya maombi.
August 30, 2015
Isabelah Samwel (via email) said:
Barua pepe yangu ni isabefit@gmail.com. Asante
August 30, 2015
abdul chorobi (dar es salam) said:
P.box 455 dar es salam
August 31, 2015

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.