2 Kanama, 2012 at 18:21 EAT (edited 2 Kanama, 2012 at 18:26 EAT)
sheria zetu napata shida kuzizungumzia, wakati katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inamtambua mtoto kuwa ni yule aliye chini ya miaka 18. serikali inaendelea kuhimiza uundwaji wa sera na sheria zinazomlinda mtoto kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa. chakushangaza sheria hii ya ndoa inatoa ruhusa kwa mtoto kuolewa chini ya umri wa miaka 18 kwa idhini ya wazazi wake. Je huku ni kumtendea haki kijana??