Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

mwanzoni mwa mwaka 2009 tulianza kutengeneza filamu mbalimbali kama sehemu ya kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana lakini pia kuwapa nafasi vijana kukutana na kupashana habari juu ya mahusiano na matumizi ya dawa za kulevya.

kufungua kituo cha habari na sanaa,kwa vijana katika kata ya mwangata kama sehemu ya vijana kukutana na kupata habari mbalimbali za afya ya uzazi na ujinsia.

kushirikiana na NYP+ (Mtandao wa vijana wanaoishi na VVU) Kuendesha mradi wa Afya ya uzazi na Stadi za maisha kwa vijana wa kyela katika kata za Ngonga, Kyela na Kujunjumele.

kuendesha mradi wa AFYA YA UZAZI NI HAKI YA KIJANA "TUITETEE" kwa usimamizi wa AMREF katika manispaa ya Iringa hususa kata za Mwangata na Ruaha.