Envaya

                                  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 

 

 

 

MWONGOZO NA MAJUKUMU YA MABARAZA YA WAZEE

NGAZI YA VIJIJI/MTAA, KATA, WILAYA, MKOA NA TAIFA

 

        Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003.

(Uk. 16 Sura ya 3, Ibara ya 3.14-.3.15 na Uk.17, Sura ya 4, Ibara ya

4.1 – 4.4)

 

Maamuzi kuhusu mipango shirikishi ya maendeleo ya maisha ya watu yanafanywa katika ngazi za Vijiji/Mitaa, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa. Wazee ni miongoni mwa wananchi ambao mchango wao ni muhimu sana katika maendeleo ya Taifa letu. upo umuhimu wa kuweka utaratibu utakao hakikisha upatikanaji wa mchango wa wazee kuhusu maisha yao na ya jamii kwa ujumla. Ili kufanikisha azma hii, Sera ya Taifa ya Wazee (National Aging Policy–NAP 2003) inasisitiza kwamba

       “YATAUNDWA MABARAZA YA USHAURI WA WAZEE KATIKA

        NGAZI ZA VIJIJI/MITAA, KATA, WILAYA, MKOA NA TAIFA”

 

Hivyo, itambulike kuwa mabaraza ya wazee ni huru, si ya kiitikadi, kidini au ukabila na kila mtu mwenye umri wa miaka 60 na kuendelea ana haki ya kuwa mjumbe wa Baraza la Wazee.

 

        Namna – Mabaraza yanavyoundwa.

Ngazi ya vijiji/Mtaa

  • Halmashauri ya Wilaya kupitia Watendaji na Wenyeviti wa Vijiji/Mtaa itaitisha mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwabaini wazee wote.
  • Kwa kushirikiana na serikali ya kijiji/Mtaa, Halmshauri itasimamia uundaji wa Baraza la Kijiji/Mtaa kwa kusimamia uchaguzi wa viongozi wa Baraza (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Katibu Msaidizi, Mtunza Hazina, Wawakilishi 2 (Me na Ke) katika Baraza la Maendeleo la Kijiji/Mtaa na Wafuatiliaji 2 (me na ke) wa masuala ya wazee (OPMGs-Older People’s Monitoring Group).

 

  • Katika zoezi hili Mtendaji wa Kijiji/Mtaa atakuwa Mwenyekiti au Msimamizi wa uundaji wa Baraza la Wazee. Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji atakuwa Katibu na atawajibika kuandika muhtasari wa uundaji wa Baraza la Kijiji/Mtaa.

 

  • Nakala ya Mhutasari wa uundaji wa Baraza la Kijiji/Mtaa itakabidhiwa kwa Mtendaji wa Kijiji, Mtendaji wa Kata.

 

Ngazi ya Kata

  • Halmashauri ya Wilaya kupitia Watendaji wa Kata itaitisha mkutano wa viongozi wa Mabaraza ya Vijiji/Mtaa yana katika Kata ambayo imeunda Mabaraza ya Wazee ya Vijiji/Mtaa (viongozi 9 kutoka kila Kijiji/Mtaa.

 

  • Kwa kushirikiana na Serikali ya Kata, Halmashauri itasimamia uundaji wa Baraza la Kata na kusimamia uchaguzi wa viogozi wa Baraza ngazi ya Kata (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mtunza Hazina, Wawakilishi 2 (me na ke) katika Baraza la Maendeleo la Kijiji/Mtaa na Wafuatiliaji 2 (me na ke) wa masuala ya wazee (OPMGs –People’s Monitoring Group).

 

  • Katika zoezi hili Mtendaji wa Kata atakuwa Mwenyekiti au Msimamizi wa uundaji wa Baraza la Wazee. Afisa Maendeleo au Afisa Ustawi wa Jamii atakuwa Katibu na atawajibika kuandika mhutasari wa uundaji wa Baraza la Kata.

 

  • Nakala ya Mhutasari wa uundaji wa Baraza la Kata itakabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya na Mratibu wa Wazee Wilaya (Order People’s Focal Person).

 

Ngazi ya Halmashauri

  • Halmshauri ya Wilaya kupitia Afisa Ustawi wa Wilaya kitengo cha Wzee Focal Person itaitisha mkutano wa viongozi wa Mabaraza ya Kata zote katika Wilaya ambazo zimeunda Mabaraza ya wazee ya Kata (viongozi 9 kutoka kila Kata)

 

  • Kwa kushirikiana na Afisa Ustawi wa Jamii Kitengo cha Wazee (Focal Person), Halmashauri itasimamia uundaji wa Baraza la Wilaya na kusimamia uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Wilaya (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti Katibu, Makamu Katibu, Mtunza Haziina, Wawailishi 2 (me na ke) katika Baraza la Madiwani la Halmashauri.
  • Katika zoezi hili Mkurugenzi wa Halmashauri atakuwa Mwenyekiti au Msimamizi wa uundaji wa Baraza la wazee la Wilaya. Afisa ustawi wa Jamii –Focal person atakuwa Katibu na atawajibika kuandika mhutasari wa uundaji wa Baraza la Wilaya.
  • Nakala ya Mhutasari wa uundaji wa Baraza la Wilaya itakabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mratibu wa Wazee (Older People’s Focal ) na Mkuu wa Wilaya.
  • Baada ya uchaguzi wa uongozi wa Baraza la Wilaya Halmashauri itapanga siku maalum ya uzinduzi rasmi wa Baraza hilo ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya.

 

Ngazi ya Mkoa

  • Mkoa kupitia Afisa Ustawi wa Mkoa kitengo cha Wazee Focal Person itaitisha mkutano wa viongozi wa Mabaraza ya Wilaya zote katika Wilaya ambazo zimeunda Mabaraza ya Wazee ya Kata (Viongozi 9 kutoka kila Halmashauri Mkoani)
  • Kwa kushirikiana na Afisa Ustawi wa Jamii Kitengo cha Wazee (Focal Person), Mkoa utasimamia uundaji wa Baraza la Mkoa na kusimamia uchaguzi wa viongozi wa Baraza Mkoa (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Makamu Katibu, Mtunza Hazina, Wawakilishi 2 (me na ke) katika baraza la Madiwani la Wilaya.
  • Katika zoezi hili Afisa Tawala atakuwa Mwenyekiti au Msimamizi wa uundaji wa Baraza la Wazee la Mkoa. Afisa Ustawi wa Jamii (Focal Person) atakuwa Katibu na atawajibika kuandika mhutasari wa uundaji wa baraza la Mkoa.
  • Nakala ya Mhutasari wa uundaji wa Baraza la Wilaya itakabidhiwa kwa Katibu Tawala Mkoa, Mratibu wa Wazee Mkoa (Older Person’s Focal Person) na kuu wa Mkoa.
  • Baada ya uchaguzi wa uongozi wa Baraza la Mkoa, Mkoa utapanga siku maalumu ya uzinduzi rasmi wa Baraza hilo ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa.

 

Umuhimu wa Mabaraza ya Wazee Kijiji/Kata/Wilaya na Mkoa

  • Kushauri na kuishawishi Serikali na wanasiasa kuboresha huduma kwa Wazee na wategemezi wao.
  • Kuimarisha utambuzi wa pamoja wa Wazee na kuwapa Wazee hali ya kujiona nao ni sehemu muhimu ya jamii.
  • Kuajadiliana na wawakilishi wa Kikatiba na kujitolea kama wawakilishi wa mambo yanayohusu Wazee.
  • Kuboresha mawasiliano kati ya Wazee na Serikali katika hali inayokubalika Kikatiba, Halmashauri/Manispaa, Mkoa, Idara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Jamii, Afya, Polisi n.k.
  • Kutetea masuala ya Wazee kwa Mashirika, Serikali, Taasisi za Kidini na watoa huduma wengine wowote.

 

Wajumbe

  • Wazee wote wenye lengo la kutafuta kuboresha hali ya maisha ya Wazee wote katika Jamii.
  • Kuwa wajumbe wa Uzee kulingana na umri. Kigezo cha kuwa Mzee ni kuanzia miaka 60. Japokuwa hii inaweza kubadilika kulingana na mazingira au mahitaji Fulani.
  • Watendaji wa Serikali ambayo ni Wazee wanaoishi katika maeneo hayo wanaweza kuwa wajumbe kwa kigezo cha umri na si nafasi za Serikalini.
  • Watendaji wa Serikali watakao alikwa wanaweza kuwa na sauti kama wajumbe wengine.

 

Uongozi

  • Kila Baraza litakuwa na Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti, Katibu, Makamu Katibu na Mtunza Hazina. Nafasi hizi kupendekezwa na kupigiwa kura na wajumbe.
  • Wajumbe wawili (me na ke). Hawa ni wakusanyaji takwimu (Older People’ Monitoring Group), Kero za huduma za Afya Kipato, haki mbalimbali za Wazee.
  • Uchaguzi hufanywa siku ya mkutano wa uchaguzi kwa tarehe iliyokubalika.
  • Ili Mzee aweze kuchaguliwa ni lazima apendekezwe na wajumbe na si kujipendekeza mwenyekiti.
  • Viongozi ni lazima wawe Wazee wenyewe na ambao wanakubalika katika Kijiji na wenyenia hasa ya kujitolea kuwakilisha Wazee wenzao.
  • Baraza litapendekeza kikundi cha watu wachache wmbao watawasilisha mapendekezo yao na mipango kwa wahusika.
  • Kundi hili litakapopendekezwa linaweza kua la wanaotunza wagonjwa majumbani (HBCs), wafuatiliaji wa mambo ya sheria (Paralegals), wafuatiliaji wa masuala ya Wazee waelimishaji rika n.k.

 

Utendaji:

  • Baraza linaweza kutumika na Serikali, Wabunge, Wanasiasa Watendaji na Taasisi mbalimbali kama chanzo cha habari za Wazee takwimu, na mambo kadhaa ya Wazee kabla ya mipango, uboreshaji hudua na utekelezaji wa mambo yanayohusu maisha ya Wazee kuanzia Kijiji hadi Taifa.
  • Baraza linaweza pia kuwa kama sehemu ya kiutendaji wa Shirika au Mashirika ya Wazee yanayofanya kazi kusaidia Wazee Kijiji au Wilaya.
  • Wajumbe kukutana kubadilishana mawazo na kupeana tarifa muhimu za maisha yao ili kuleta mabadiliko.
  • Baraza litakutana na kuzungumzia mambo/kero zinazogusa maisha ya Wazee katika eneo lao kama vile Afya, huduma za matibabu, pensheni kwa wazee wote na namna nyingine za kipato kwa wazee n.k.

 

  • Baraza katika kila Wilaya litafanya kazi kusaidia au kutaarifu Serikali, Mashirika ya kuhudumia Wazee, jamii na Wazee kuhusu mambo yanayohusu maisha ya Wazee.

 

Mikutano.

  • Inaweza kuamliwa na wajumbe lakini mara nyingi huwa mara moja kwa mwezi.
  • Inaweza kuwa ya dharura linapotokea jambo kama msiba/mauaji uchaguzi wa dharura n.k.
  • Utaitishwa na Katibu kwa kushirikiana na Mwenyekiti
  • Serikali ya Kijiji au Kata au Wilaya au Mkoa inaweza kuhudhuria ili kuweza kujua na kutoa majibu juu ya matatizo yanayokabili Wazee wa Kijiji/Kata/Wilaya husika.

 

 

Majukumu ya Mabaraza ya Wazee kuanzia ngazi ya Vijiji/Mta hadi Taifa

 

  1. BARAZA LA WAZEE LA KIJIJI/MTAA
  2. Kubadilishana mawazo na kupeana taarifa za maisha yao ili kuleta mabadiliko.
  3. Kuzungumzia Kero/Changamoto mbalimbali zinazowakabili Wazee katika maeneo yao (mf. Afya, huduma za matibabu, pensheni kwa wazee wote na namna nyingine za kipato.)
  4. Kutoa takwimu, taarifa mbalimbali za Wazee kabla ya mipango na bajeti za Serikali, Taasisi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na wanaharakati wa masuala ya Wazee.
  5. Ni sehemu ya kiutendaji ya Mashirika ya Wazee yanayofanya kazi kusaidia Wazee Kijiji/Mtaa, kwenye Kata au Mkoa.
  6. Kutoa changamoto, kushauri na kupendekeza masuala ya kimaendeleo, haki na stahili za Wazee kwa watunga Sera na watoa maamuzi.
  7. Kuchagua viongozi na wafuatiliaji wa masuala ya Wazee (OPMG OLDER PEOPLE MONITORING GROUPS).
  8. Kuboresha na kupeana maarifa, uzoefu, na uwezo baina yao na kutatua masuala mbalimbali ya msingi mfano uboreshaji huduma rafiki za afya kwa Wazee, Usafiri, miundombinu bora kwa Wazee, kushughulikia kesi mbalimbali. N.k.

 

  1. MAJUKUMU YA BARAZA LA WAZEE LA KATA
  2. Kufanya utambuzi wa mahitaji ya Wazee ili yaingizwe kwenye mipango na bajeti za Kata husika.
  3. Kufanya Mkutano wa Baraza la Wazee la Kata Mara 1 kwa mwezi kwa maana hiyo Baraza la Kata litakutana Mara 12 kwa mwaka.
  4. Kufanya uchaguzi wa viongozi wanne (4) kutoka Baraza la kila Kijiji kwenye Kata husika (yaani, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Katibu Msaidizi) kukutana katika ngazi ya Kata na kuunda Baraza la Kata. Kufanya uchaguzi wa uongozi wa Baraza la Kata (Mwenyekiti, Mwenyekiti Msaidizi, Katibu na Katibu Msaidizi) utafanya chini ya usimamizi wa Mtendaji wa Kata, Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri/Kata na Wenyeviti wa Vijiji ndani ya Kata husika.
  5. Kuchagua Wazee wawili (Me na Ke) ili kuwawakilisha kwenye Baraza la Maendeleo ya Kata (WDC).
  6. Kusimamia haki na stahili za Wazee katika Kata.
  7. Kushauri Baraza la Maendeleo la Kata (WDC) kufanya utambuzi na mahitaji ya Wazee katika Kata.
  8. Kuwajumuisha Wazee katika mipango ya uzalishaji mali kwenye Kata.
  9. Mabaraza ya Wazee kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ulinzi kwa wazee.
  10. Kuelimisha Wazee na jamii kuhusu masuala ya Uzee na Kuzeeka na ushiriki wa Wazee katika maendeleo ya Taifa.

 

 

  1. MAJUKUMU   YA   BARAZA   LA WAZEE WILAYA.
  2. Kupitia majumuisho ya kero mbalimbali   za   wazee   zilizoletwa   na   wawakilishi/wajumbe wa Baraza   la wilaya kutoka   kwenye   Kata mbalimbali wilayani ,kwa kuzijadili na kuzitafutia ufumbuzi.
  3. Kufanya   Mkutano wa baraza la   wazee   la   wilaya   kila   baada   ya miezi mitatu. Kwa maana hiyo Baraza la Wilaya   litakutana   Mara   4   kwa Mwaka
  4. Viongozi   (4) wanne kutoka mabaraza   ya Kata kwenye Wilaya husika ( yaani : Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti,Katibu na Kaimu Katibu) kukutana katika ngazi   ya Wilaya   na kuuunda BARAZA LA WILAYA. Uchaguzi uongozi   wa BARAZA LA WILAYA (Mwenyekiti,Mwenyekiti Msaidizi, Katibu na Katibu Msaidizi) utafanyika chini   ya usimamizi wa Afisa Ustawi   wa Jamii Wilaya, Mwenyekiti wa Huduma za Kijamii   wa Wilaya, Watendaji wa Kata zote ndani   ya Wilaya   husika na litazinduliwa   Rasmi na Mkuu wa Wilaya/Katibu Tawala wa Wilaya.
  5. Kupeleka kero ambazo zimewashinda kuzitatua kwenye   Baraza la Madiwani la wilaya.
  6. Kuchagua wawakilishi 2 (me   na   ke) kuwawakilisha   wazee   wote   wilayani kwenye Baraza la Madiwani (Full Council).
  7. Kushawishi   Halmashauri kutenga bajeti maalumu   za Miradi ya uzalishaji   mali kwa makundi   ya wazee   wasiojiweza.
  8. Kushawishi   serikali   kutoa vitambulisho kwa wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea kwa ajili   ya kupatia huduma mbalimbali mf. Huduma   za afya, maji, kupata msamaha wa kodi   ya   majengo.
  9. Kuratibu mabaraza ya   kata

 

 

 

 

D. MAJUKUMU YA BARAZA LA MKOA.

  1. Kufanya Mkutano wa Baraza la Wazee la Mkoa kila baada ya miezi 6. Kwa maana hiyo Baraza la Mkoa litakutana Mara mbili (2) kwa Mwaka.
  2. Kusimamia utoaji wa huduma kwa Wazee Wilaya zote Mkoani.
  3. Viongozi (4) wanne kutoka Mabaraza ya Wilaya kwenye Mkoa husika yaani: Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Katibu Msaidizi, Kukutana katika ngazi ya Mkoa na kuunda Baraza la Wazee la Mkoa. Uchaguzi wa uongozi wa Baraza la Mkoa (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Katibu Msaidizi) utafanyika chini ya usimamizi wa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Afisa Ustawi wa Jamii wa Sekretarieti ya Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya kwenye Mkoa husika, Wenyeviti wa Huduma za Kijamii wa Halmashauri katika Mkoa husika, na litazinduliwa Rasmi na Mkuu wa Mkoa au Katibu Tawala wa Mkoa (RAS).
  4. Kuhimiza Halmashauri za Wilaya Manispaa, Majiji, Asasi na Wakala za Hiari ili kutoa huduma mbalimbali za msingi kwa Wazee wote wa miaka 60 na kuendelea.
  5. Kushauri Serikali kuwa na mwakilishi wa Wazee kwenye Bunge kama ilivyo kwa makundi ya wanawake, Walemavu na vijana.
  6. Kupokea kero mbalimbali za Wazee kutoka Wilaya na kuzitafutia ufumbuzi.
  7. Kuchagua wawakilishi wawili watakaoshiriki katika kuunda Baraza Huru la Wazee la Taifa.
  8. Kuratibu shughuli za Mabaraza ya Wazee ya kila Wilaya na Mkoa

               

March 11, 2018
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.