KATIBA YA MFAWICA.
UTANGULIZI
TAFSIRI / TAMKO RASMI KWA NGO YA MFWICA.
TAFSIRI YA ASASI YA MFAWICA NI KWAMBA:-
- NI SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI
- NI SHIRIKA LISILOFANYA KAZI YA FAIDA BINAFSI
- NI SHIRIKA HURU KATIKA SHUGHULI ZAKE
- NI SHIRIKA LISILO LA KISIASA
- NI SHIRIKA LISILO LA KIDINI
- NI SHIRIKA LISILO LA UKOO, UKABILA, JINSIA MOJA, WAJANE, YATIMA N.K.
- NI SHIRIKA LINALOFANYA SHUGULI ZAKE KWA KUJITOLEA
- NI SHIRIKA LINALOFANYAKAZI KWA UWAZI, UKWELI, KISHERIA, TARATIBU NA KATIBA YA ASASI.
- NI SHIRIKA LINALOFANYA SHUGHULI ZA KIJAMII KWA MAENDELEO YA TAIFA NA DUNIA NZIMA.
HISTORIA
Shirika la MFAWICA lilianzishwa mwaka 2005 katika Kijiji cha Lubalisi – Kata ya Igalula, Tarafa ya Buhingu, wilaya ya Kigoma, Vijijini – Mkoa wa Kigoma ambao unapakana na :-
- Nchi ya Burundi – upande wa Magharibi
- Nchi ya Congo (DRC) – upande wa Kusini Magharibi
- Mkoa wa Rukwa – upande wa Kusini
- Mkoa wa Tabora – upande wa Mashariki
- Mkoa wa Shinyanga – upande wa Kaskazini Mashariki
- Mkoa wa Kagera – upande wa Kaskazini
Shirika lilianzishwa na wanachama kumi na moja (11) kwa lengo la kutunza mazingira, misitu na wanyama pori tokana na uzoefu wa kazi hiyo.
Uzoefu wa kazi hiyo ni kutokana na kufanya kazi ndani ya Hifadhi ya Mahale National Park, Kigoma.
Wanachama waanzilishi mwaka 2005 ni:-
- RAMADHANI NYUNDO SIKA
- BARAKA PETER NZOVU
- SILINDILA ATHUMAN KALIMBA
- SALUMU SHABANI KITOPENI
- MAKELELE MASANYUKE KAKOMO
- AKSA ANDREW CHAGAMBA
- MOHAMED HAMIS KALIMALINZA
- MOSHI HARUNA MADIGIDI
- BUHURU HAMISI BUTATI
- RAULENTI RICHARD GABRIEL
Wanachama wapya wa kujiunga mwaka 2009/12ni:-
- HAMISI ALMASI
- MWAMBA KIEMENA.
- ALEX EKAMA MNENE
- Simoni Patilo Bwilo
- Imani Richard Gabriel
- Issa Lufwifwi
- Simon Petro
- Laimond Simon
- Rajabu Juma Madolla
- Rajabu Kakumo
- Shabani Mussa Kibanga
- Mashaka Almas
- Shabani Kijungi
- Goodnes Issak Baziyaka
Shirika lilisajiriwa tarehe 10 Machi, 2008 na kupata Usajiri Namba OONGO/0436 inayotoa kibali kwa Asasi kufanyakazi katika eneo lote la Tanzania. Pia shirika linamiliki eneo la ekari 2000 zinazohifadhiwa kwa kutunza Maliasili zote zilizopo eneo hilo la hifadhi ya Milele Forest Kalobwa kijiji cha Lubalisi kata ya Igalula Kigoma Vijijini.
Lengo kuu la asasi ni kuona uharibifu wa mazingira, misitu, vyanzo vya maji, viumbe hai n.k. umepungua na kukoma kabisa. Na kuona hali ya umaskini na magonjwa yamepungua ndani ya jamii ya Watanzania mahali lilipo shirika na duniani kote. Na kuzingatia utaratibu mzima kama ilivyo tafsiriwa au tamko rasmi hapo juu.
BAADHI YA RASLIMALI ZILIZOPO ENEO LINALOHIFADHIWA NA MFAWICA:
WANYAMAPORI
Tembo, nyati, pongo, chui, sokwe mtu, nguruwe pori, nyani, kima, tumbili mwekundu (tusolima), ndugulungu (jamii ya kima), digidigi, mbuzi mawe, seuzi, mbubhu, swala, ngiri, panya n.k.
WADUDU
Vipepeo, panzi, nyuki, sisimizi, minyoo n.k.
NYOKA
Mamba pori, chatu, nyoka kamba, n.k.
NDEGE
Kwale, kanga, kiluwiri, kukutanda mdogo n.k.
MAHALI OFISI KUU YA ASASI ILIPO.
Ofisi ilipo ya Asasi ya MFAWICA ni Kijiji cha Rukoma kata ya Igalula, tarafa ya Buhingu, wilaya ya Kigoma vijijini mkoa wa Kigoma.
Ukiwa Kigoma Bandarini hadi Kituo cha Meli cha Rukoma penye ofisi kuu ya MFAWICA ni km.121 kwa kipomo cha GPS muda wa safari ya Meli ni wastani wa masaa 10. Kwa kutumia Boti za abiria kutoka Forodhani Ujiji ni wastani wa masaa 14 kufika Rukoma. Kwa usafiri wa ndege ni wastani wa dakika 30. Usafiri kutoka ofisi kuu ya Asasi ya MFAWICA Rukoma hadi kwenye Hifadhi ya
MILELE FOREST KALOBWA Kijiji cha Lubalisi –. Ni safari ya km zipatazo 30. Zaidi ya hapo Asasi bado inahitaji ujuzi, na vifaa kwa kupata taarifa sahihi zaidi.hifadhi hiyo yenye kufahamika kwa jina la milele forest KALOBWA ni moja ya juhudi zinazofanywa na Asasi ya MFAWICA kwa maendeleo ya Taifa na kimataifa katika kupambana na umaskini, magonjwa na usimamizi wa maliasili.
KATIBA
SEHEMU YA KWANZA
1.0 KATIBA
1.0 JINA LA ASASI : MILELE FOREST AND WILDLIFE CONSERVATION
ASSOCIATION (MFAWICA)
1.1 MAKAO MAKUU YA ASASI
KIJIJI CHA RUKOMA
KATA YA IGALULA
TARAFA YA BUHINGU
WILAYA YA KIGOMA (V)
KIGOMA, TANZANIA – AFRIKA MASHARIKI
1.2 OFISI NDOGO
IPO KATIKA ENEO LA UWANJA WA MPIRA LAKE TANGANYIKA
KATA YA RUSIMBI
TARAFA YA KIGOMA KUSINI (LAKE TANGANYIKA STADIUM)
KATIKA MANISPAA YA KIGOMA/UJIJI
1.3 MAWASILIANO
S.L.B. 35, KIGOMA
SIMU: +255 762 219605; +255 714 465053
Simu/nukushi; +255 28 2803976
EMAIL: mileleforest2007@yahoo.com/info@mfawica.org
TOVUTI: www.mfawica.org
1.4 ENEO LA UTENDAJI WA ASASI TANZANIA BARA
1.5 NEMBO YA ASASI
PICHA YA MNYAMA SOKWE JUU YA MTI
1.6 KUTAKUWA NA MATAWI NDANI YA TANZANIA BARA AMBAYO YATAKUWA NA MAMLAKA YA KUJIENDESHA YENYEWE KWA KUFUATA KATIBA HII.
SEHEMU YA PILI
2.0 LENGO KUU LA ASASI (DIRA)
2.1 KUONA HALI YA UMASKINI NA MAGONJWA NDANI YA JAMII YA WATANZANIA NA
DUNIANI KOTE INAPUNGUA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA, UCHOMAJI MISITU
VIUMBE HAI NA VYANZO VYA MAJI UNAKOMA KABISA
SEHEMU YA TATU
3.0 LENGO MAHUSUSI (DHAMIRA)
3.1 KUTOA ELIMU YA KUPAMBANA NA UMASKINI, MAGONJWA, UHARIBIFU WA
MAZINGIRA, UCHOMAJI MISITU, VIUMBE HAI NA VYANZO VYA MAJI KATIKA JAMII YA WATANZANIA NA DUNIANI KOTE.
SEHEMU YA NNE
4.0 SHUGHULI
4.1 UTOA ELIMU YA KUTUNZA MAZINGIRA YAWE BORA NA ENDELEVU KWA
MANUFAA YA KIZAZI CHA SASA NA BAADAYE
4.2 KUTOA MAFUNZO YA KUTUNZA NA KULINDA VYANZO VYA MAJI KATIKA MAENEO
YA JAMII WALIPO WATANZANIA KWA KUBORESHA MITO, MABWAWA, MAZIWA, VISIMA NA BAHARI KWA FAIDA YA WATANZANIA NA DUNIA NZIMA.
4.3 KUTOA ELIMU YA KUTUNZA NA KULINDA MISITU KATIKA MAENEO YA MISITU YA
ASILI NA YA KUPANDIKIZWA KATIKA TANZANIA KWA KUELEZA SERA YA TAIFA YA
MISITU.
4.4 KUANZISHA HIFADHI YA MAZINGIRA,MISITU, VYANZO VYA MAJI NA VIUMBE HAI
KATIKA MAENEO YA JAMIIKWA MALENGO YA KUTUNZA KI-UJUMLA KAMA MFANO
KWA JAMII YA KITANZANIA NA DUNIA.
4.5 KUTOA ELIMU YA UJASILIA MALI KWA JAMII ILI KUJIONGEZEA KIPATO
KISICHOWEZA KUATHIRI MAZINGIRA, VYANZO VYA MAJI, MISITU NA VIUMBE HAI ILI KUONDOKANANA UMASKINI KAMA NJIA MBADALA YA KULINDA MALI ASILI
4.6 KUANZISHA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI KWA KUTOA ELIMU NA MAFUNZO JUU
YA:- KILIMO, UFUGAJI KUKU, NYUKI, MABWAWA YA UFUGAJI SAMAKI, MIFUGO
NA VIKUNDI VYA KUWEKA NA KUKOPA NA KUTUMIA FURSA ZINAZOPATIKANA ILI
KUONGEZA KIPATO NA KUONDOKANA NA UMASKINI, BILA KUATHILI MALI ASILI.
4.7 KUWEKA SHERIA NDOGO NDOGO KWA AJILI YA USALAMA WA MALI ASILI, MISITU,
VYANZO VYA MAJI, MITO, MAZIWA, VIUMBE HAI WAISHIO KATIKA MAZINGIRA
HAYO KWA JAMII KOROFI, SAWA SAWA NA MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI.
4.8 KUSHAWISHI JAMII KATIKA MAENEO YANAYOFIKIWA NA UTENDAJI WA MFAWICA
KUANZISHA MICHEZO YA JADI ILI KUIBUA UTAMADUNI WA MTANZANIA NA
KUWA SEHEMU YA UTALII WA NDANI NA NJE YA TANZANIA NA KWA SEHEMU YA
KIPATO.
4.9 KUJITANGAZA KWA MASHIRIKA MENGINE NA KUUNGANA KAMA MTANDAO ILI
KUJENGA MAHUSIANO YA KARIBU KATIKA KUPAMBANA NA UMASKINI,
MAGONJWA, USAWA NA HAKI ZA BINADAMU HUSUSANI JINSIA NA WATOTO.
4.10 KUTANGAZA FURSA ZA VIVUTIO VINAVYOPATIKANA KATIKA MAENEO MBALIMBALI
NCHINI NA KUKARIBISHA WATALII TOKA NJE KWA KUTANGAZA:- VYOMBO VYA
HABARI, MAGAZETI, VIPEPERUSHI, MTANDAO N.K.
4.11 KUFANYA UTAFITI WA MALI ASILI KAMA VILE:- MIMEA AU UOTO WA ASILI,
MADINI, WANYAMA PORI, WADUDU, NDEGE, JAMII YA NYOKA; HASA MAENEO
YANAYOHIFADHIWA NA ASASI YA MFAWICA NA MAENEO MENGINE NDANI YA
TANZANIA.
4.12 KUSHAWISHI NA KUSHIRIKIANA NA JAMII KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA
KUJITOLEA KUJENGA SHULE, ZAHANATI, BARABARA, MADARAJA NA KILIMO.
4.13 KUANZISHA VITALU VYAKUOTESHA MICHE YA MITI ITAKAYOPANDWA KATIKA
MAENEO MBALIMBALI KAMA VILE MAKAZI, MASHAMBANI, KANDOKANDO YA
MITO ILI KUBORESHA MAZINGIRA NA KUWA ENDELEVU ILI KUPUNGUZA UKAME
NA HEWA CHAFU NA HATIMAYE MITI HIYO KUWA KITEGA UCHUMI KAMA VILE
MBAO ZITAZARISHWA.
4.14 KUTOWA ELIMU YA KUPAMBANA NA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VVU NA
UNYANYAPAAJI WA WAATHIRIKA WA UKIMWI NDANI YA JAMII YA WATANZANIA .
4.15 KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KWA
KUWAPA MISAADA KAMA VILE ELIMU, MATIBABU, VIFAA VYA SHULE, CHAKULA
PALE INAPOWEZEKANA NA KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU, WAFADHILI NA
SERIKALI.
4.16 KUTOA ELIMU JUU YA MADHARA YA KUTUMIA MADWA YA KULEVYA KWA VIJANA
JINSIA YAKIUME NA KIKE NA JAMII KATIKA MAENEO YOTE YANAYOFIKIWA NA
ASASI (IKIWA NI PAMOJA NA KUPAMBANA NA UINGIZAJI AU UZALISHAJI WA
MADAWA YA KULEVYA.
4.17 KUBORESHA ELIMUKWA WANA ASASI KWA KUGHARAMIA ELIMU SHULENI,
SEMINA, WARSHA, KONGAMANO, VYUONI N.K. KWA GHARAMA ZA ASASI,
WADAU NA PIA WAFADHILI WENYE KUPENDA MAENDELEO ILI ASASI KUWA NA
UFANISI BORA, KIUTENDAJI
4.18 KUWA NA MFUMO WA ULINZI WA MALIASILI NA MALI ZA ASASI KWA KUFUATA
SHERIA ZA NCHI KILA ITAKAVYOHITAJIKA.
SEHEMU YA TANO
5.0 IDARA:
SHIRIKA LITAKUWA NA IDARA AMBAZO ZITASIMAMIWA NA WAKUU WA IDARA KAMA IFUATAVYO:-
5.1 ELIMU NA MAFUNZO
5.2 AFYA
5.3 MAZINGIRA, MISITU NA VIUMBE HAI
5.4 MAHUSIANO, UTALII NA UTAFITI
5.5 MIPANGO KAZI, USHAWISHI NA UWAKILISHI
5.6 FEDHA
5.7 MAENDELEO YA JAMII
5.8 ULINZI NA UTETEZI WA SERA YA TAIFA YA MALIASILI
SEHEMU YA SITA
6.0 UANACHAMA
6.1 ASASI ITAKUWA NA WANACHAMA WA AINA MBILI MAKAO MAKUU NA MATAWI
(i)WANACHAMA WAANZILISHI
(ii)WANACHAMA WAPYA KWA KUOMBA
SEHEMU YA SABA
7.0 MASHARTI YA UANACHAMA
7.1AWE ANAJUA KUSOMA NA KUANDIKA
7.2 AWE NA UMRI KUANZIA MIAKA 18 NA KUENDELEA
7.3 AWE NA AKILI TIMAMU, TABIA NZURI NA NGUVU YA KUFANYAKAZI KIKAMILIFU
7.4ASIWE MWEHU, KICHAA, MWENDAWAZIMU N.K.
7.5AWE MLIPAJI ADA, MICHANGO INAYOPANGWA NA ASASI ILI KUIMARISHA MAJUKUMU YA MRADI/MIRADI KATIKA MUDA ULIOPANGWA.
7.6 AWE NA NIDHAMU NA MAHUSIANO MAZURI KWA WANACHAMA WENZAKE, WAFANYAKAZI NA WASIO WANACHAMA NDANI YA JAMII.
7.7 AWE MTIIFU KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YANAYOTOLEWA NA VIONGOZI WAKE, KAMATI TENDAJI, MKUTANO MKUU WA ASASI HATA KWA KUTUMIA GHARAMA BINAFSI.
7.8 ASIWE MCHOCHEZI,VURUGU, MAJUNGU, UONGO, NDUMILAKUWILI AMBAPO AKIBAINIKA HATUA KALI ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
SEHEMU YA NANE
8.0 MASHARTI YA KUJIUNGA KWA WANACHAMA WAPYA NA KATIKA MATAWI YA ASASI
8.1 (i) MTU ANAYETAKA KUWA MWANACHAMA MPYA WA MFAWICA ATAANDIKA
BARUA KWAKATIBU MTENDAJI, AMBAPO KAMATI ITAANDAA MAOMBI YOTE
NA KUYAPELEKA KATIKA MKUTANO MKUU KUPATA MAJIBU YA MAOMBI
YAKE.
(ii) MAOMBI YALIYOFANYIWA UHAKIKI NA MKUTANO MKUU NA KUPITA WATATUMIWA FOMU YA MAOMBI NA WALE WALIOANGUKA WATATUMIWA TAARIFA YA POLE.
(iii)MWANACHAMA HUYO ATATAKIWA KULIPIA ADA, KIINGILIO KITAKACHOPANGWA NA MKUTANO MKUU WA ASASI.
8.2 ASASI ITAFUNGUA MATAWI TANZANIA BARA
(i) ASASI ITAFUNGUA MATAWI MAPYA KATIKA KUPANUA WIGO WA SHUGHULI ZAKE.
(ii) TAWI LITAFUNGULIWA KWA KUANZA NA WANACHAMA KUMI (10)
(iv) KILA MWANACHAMA ATALIPA ADA YA KILA MWEZI SHILINGI 5,000/= NA KIINGILIO CHA SHILINGI 100,000/=
(v)WATACHAGUA VIONGOZI WAO KAMA VILE:- MWENYEKITI, MAKAMU M/KITI, KATIBU, KATIBU MSAIDIZI, MHASIBU NA WAJUMBE WAWILI. LAKINI UONGOZI WA TAWI LOLOTE UTAKUWA CHINI YA UTAWALA WA VIONGOZI WA MAKAO MAKUU YA SHIRIKA.
8.3 UTARATIBU WA SHUGHULI
(i)TAWI LITAFUNGULIWA NA MWENYEKITI WA MFAWICA AKIWEPO KATIBU MTENDAJI NA MHASIBU NA MGENI RASMI ATAKAYEOMBWA KUHUDHURIA KAMA MFUNGUZI WA TAWI HILO N.K
(ii)TAWI LITAFANYAKAZI KWA MAELEKEZO YA MAKAO MAKUU TU, NA SI VINGINEVYO.
(iii) VIKAO VITAFANYIKA KAMA ILIVYO KATIKA SEHEMU YA NNE YA KATIBA YA MFAWICA
8.4 MASHARTI YA KUJIUNGA UANACHAMA
(i)KUJIUNGA ITAKUWA KAMA ILIVYO SEHEMU YA NANE YA KATIBA KIF. 8.0; 8.1 (i) – (iii) NA 8.2 (iii)8.5 MASHARTI MENGINE
(i) KILA MWANACHAMA ATAZINGATIA VIPENGELE HUSIKA NDANI YA KATIBA YA MFAWICA
SEHEMU YA TISA
9.0 HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA
9.1 KUCHAGUA / KUCHAGULIWA KUWA KIONGOZI KWA WADHIFA WOWOTE KATIKA ASASI
9.2KULINDA NA KUTETEA KATIBA, MALI, MIONGOZO NA KWA KUTUMIA SHERIA YA NCHI.
9.3KUPATA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA ASASI
9.4KUWA NA MOYO WA KUJITOLEA KIFEDHA, MALI NA NGUVU PALE INAPOBIDI BILA KULAZIMISHWA.
9.5 KUWA MWADILIFU NA MKWELI KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YA ASASI.
9.6 KUHUDHURIA VIKAO VINAVYOKUHUSU KWA MUJIBU WA KATIBA
9.7KUTOPOKEA RUSHWA AU KUTOA RUSHWA KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MFAWICA
9.8 KUSHIRIKIANA NA WENZAKE, VIONGOZI NA JAMII KATIKA KUTENDA SHUGHULI ZA MFAWICA KAMA ZILIVYOAZIMIWA.
9.9KUSHIRIKISHWA KATIKA JAMBO LA MAAMUZI KWA MUJIBU WA KATIBU, KAMATI TENDAJI NA MKUTANO MKUU
9.10 KUHESHIMU MAONI, MAWAZO, USHAURI, MAPENDEKEZO YA KILA
MWANACHAMA NA KUYAFANYIA KAZI.
9.11KUTAFUTA MISAADA YA KIFEDHA NA MALI AU VIFAA KUTOKA KWA WAHISANI,
SERIKALI, WADAU NDANI NA NJE YA NCHI KWA MANUFAA YA ASASI NA JAMII.
9.12 KUPATA/KUPEWA NAFASI YA KUJITETEA KWA KIONGOZI, KAMATI TENDAJI,
MKUTANO MKUU NDANI YA ASASI TOKANA NA KOSA AU TUHUMA PALE
INAPOBIDI KWA MAELEZO, USHAHIDI NA VIELELEZO.
9.13 KUKOSOA NA KUKOSOLEWA KATIKA VIKAO KWA MUJIBU WA KATIBA YA
MFAWICA NA HATIMAYE KUONYWA, KUSHITAKI AU KUSHITAKIWA
MAHAKAMANI.
9.14 KUEPUKA MALUMBANO KATIKA ASASI KWA UONGO, UZUSHI, UMBEA,
UCHOCHEZIKWA NAMNA YOYOTE ILE.
9.15.KUHESHIMU MAAMUZI YANAYOTOLEWA NA VIONGOZI, KAMATI TENDAJI, NA
MKUTANO MKUU.
9.16.KUTANGAZA KAZI ZA ASASI NA KUZITETEA SEHEMU MBALIMBALI I.E. MASHIRIKA,
SERIKALINI, TAASISI ZA DINI, WARSHA, MAFUNZO NA SEMINA N.K.
9.17.KUSAMBAZA VIPEPERUSHI VYA MATANGAZO YA MFAWICA KATIKA MAENEO
MBALIMBALI NA KUTOLEA MAELEZO/UFAFANUZI.
9.18. KUITAMBUA KATIBA KWA KUISOMA MARA KWA MARA
9.19.KUBEBA DHAMANA KWA JANGA LOLOTE LITAKALOTOKEA KATIKA ASASI.
SEHEMU YAKUMI
10.0 UKOMO WA UANACHAMA
10.1 KUHAMA ENEO LA MBALI NA ASASI ILIPO NA KUSHINDWA KUWAJIBIKA.
10.2 KUSHINDWA KULIPIA ADA MIEZI MITATU MFULULIZO BILA TAARIFA/SABABU ZENYE USHAHIDI WA KUTOSHA.
10.3.KUSHINDWAKULIPA MICHANGO YA KIMAENDELEO KWA MUJIBU WA KATIBA NA MAAGIZO YA MIKUTANO HUSIKA.
10.4.KUANDIKA BARUA KUOMBA KUJIUZULU KWA MWENYEKITI AU KATIBU
10.5.KUTOHUDHURIA VIKAO VITATU MFULULIZO VINAVYOKUHUSU KWA MUJIBU WA KATIBA
10.6.KUFUKUZWA
10.7 KWA HUJUMA AU WIZI WA MALI ZA ASASI NA KUSHITAKIWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
10.8 KUUGUA UGONJWA WA AKILI, KICHAA, WEHU NA KIFO
10.9 KUFUNGWA BAADA YA VYOMBO VYA SHERIA KUTHIBITISHA KIFUNGO TOKANA NA JINAI NA SHIRIKA
10.10 KUUGUA MARADHI YA MUDA ZAIDI YA MIEZI SITA NA YALE YASIYOPONA KAMA UKIMWI (PALE ASIPOWEZA KUFANYA KAZI
10.11 KWA MUJIBU WA KIF.10.1 HADI 10.10 HAKUNA MWANACHAMA YEYOTE MWENYE HAKI YA KUDAI KITU CHOCHOTE TOKA KATIKA ASASI HATA HAKI YA KUOMBA UANACHAMA TENA.
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
11.0 UCHAGUZI NA MUDA WA UONGOZI
11.1UCHAGUZI UTAFANYIKA CHINI YA USIMAMIZI WA KAMATI RASMI YA UCHAGUZI
ITAKAYOPANGWA NA KUTEULIWA NA MKUTANO MKUU WA ASASI.
11.2UCHAGUZI UTAFANYIKA KWA WAGOMBEA WALIOTIMIZA MASHARTI KATIKA FOMU NA KUREJESHWA KWA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI NDANI YA MWEZI MMOJA TU.
11.3 FOMU ZA KUOMBA KUGOMBEA UONGOZI WA NAFASI ZITAKAZOTANGAZWA ITAKUWA SIKU KUMI NA NNE TU.
11.4 UCHAGUZI UTAFANYIKA KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI HADI SAA 10:00 JIONI NA KUTOLEWA MATOKEO YA UCHAGUZI KUTANGAZWA NA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI.
11.5 NAFASI YA MWENYEKITI WA ASASI MSHINDI NI LAZIMA APATE ZAIDI YA NUSU YA KURA ZILIZOPIGWA NA ZIKILINGANA ZITARUDIWA TENA ILI KUPATA MSHINDI.
11.6 KIONGOZI AMBAYE MUDA WAKE WA UONGOZI UNAELEKEA KUISHA ANAWEZA KUOMBA TENA HIYO NAFASI AU KUBADILISHA.
11.7 KIONGOZI AKIONEKANA KUFAA ANAWEZA KUGOMBEA TENA NA TENA KWA KIPINDI KINGINE KWA MANUFAA YA ASASI.
11.8 MUDA WA UONGOZI KATIKA ASASI UTAKUWA MIAKA MITANO TU, BAADA YA HAPO MPAKA ACHAGULIWE TENA.
11.9 NAFASI YA UONGOZI ITAKAYOACHWA WAZI KABLA YA MUDA KUISHA KAMATI YA UCHAGUZI ITATANGAZA KUFANYA UCHAGUZI BAADA YA UTARATIBU WA KIF. 11.3 NA 11.2KUTIMIA
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
12.0 MUUNDO WA UONGOZI
12.1 MKUTANO MKUU NDIYO WENYE MAAMUZI YA MWISHO YA ASASI NA MIPANGO
YA UENDESHAJI
12.2 KAMATI TENDAJI NDICHO CHOMBO PEKEE CHENYE KUANDAA NA KUITISHA
MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WOTE, ½ AU 2/3
12.3 WASHAURI WA KUTEULIWA WATAKUWA WATATU NA WA KUAJIRIWA AU
KUJITOLEA KULINGANA NA TAALUMA ZAO KATIKA UTENDAJI WA SHUGHULI ZA
ASASI IWEZE KUFIKIA MALENGO.
12.4 KAMATI TENDAJI NA WAKUU WA IDARA ITASIMAMIWA NA KATIBU AU
MKURUGENZI MTENDAJI WA ASASI.
12.5 WAKUU WA IDARA WATAKUWA SABA, NAO NI:-
(i) ELIMU NA MAFUNZO
(ii) AFYA
(iii) MAZINGIRA, MISITU NA VIUMBE HAI
(iv) MAHUSIANO, UTALII NA UTAFITI
(v) MIPANGO KAZI, USHAWISHI NA UWAKILISHI
(vi) FEDHA
(vii) MAENDELEO YA JAMII
(viii) ULINZI NA UETETEZI WA SERA YA TAIFA YA MALIASILI
SEHEMU YA KUMI NA TATU
13.0 MUUNDO WA ASASI NA UONGOZI
13.1 MUUNDO WA ASASI UTAKUWA KAMA IFUATAVYO :-
(i) MKUTANO MKUU
(ii) KAMATI TENDAJI
KATIKA MAKAO MAKUU NA MATAWI
SEHEMU YA KUMI NA NNE
14.0 VIKAO
14.1 MAJUKUMU YA MKUTANO MKUU, MAKAO MAKUU NA KATIKA MATAWI
(i) MKUTANO UTAFANYIKA MARA MOJA KWA MWAKA
(ii) KUSOMA MUHTASARI WA MKUTANO ULIOPITA
(iii) KUSOMA YATOKANAYO YA MKUTANO ULIOPITA
(iv) KUTHIBITISHA TAARIFA YA UTENDAJI NA YA FEDHA YA MWAKA JANA
(v) KUPOKEA NA KUPITISHA MAKISIO/BAJETI YA MWAKA UJAO
(vi) KUTHIBITISHA NA KUPITISHA MAJUKUMU YOTE YA KAMATI TENDAJI, SERA NA MIONGOZO YA ASASI
(vii) KUPOKEA TAARIFA YA WANACHAMA WAPYA NA WALIOPO
(viii) KUTHIBITISHA KAMATI YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA ASASI
(ix) KUHAKIKISHA KUWA MAAMUZI/MABADILIKO YOTE YA ASASI YANAFANYWA NA MKUTANO MKUU TU
(x) KUPITIA NYARAKA NYETI, MIKATABA, TAARIFA NYINGINE ZINAZOHUSU ASASI.
14.2.0 KAMATI TENDAJI
14.2 UWEZO NA MAJUKUMU YA KAMATI TENDAJI MAKAO MAKUU NA KATIKA MATAWI
(i) KUFANYA KIKAO CHA KILA MWEZI
(ii) KUSOMA MUHTASARI WA KIKAO KILICHOPITA
(iii) KUSOMA YATOKANAYO YA KIKAO KILICHOPITA
(iv) KUWEKA MPANGO WA SHUGHULI KWA MALENGO NA MGAWANYO
(v) KUANDAA MIKATABA, NYARAKA NYETI, SERA, MIONGOZO, TARATIBU KWA MANUFAA YA ASASI.
(vi) KUANDAA TAARIFA YA FEDHA YA KILA ROBO MWAKA HADI MWAKA 1
(vii) KUANDAA MAKISIO/BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA MWAKA
(viii) KUBUNI VITEGA UCHUMI
(ix) KUANDAA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WOTE WA MWAKA
(x) KUANDAA TAARIFA YA WANACHAMA WANAOOMBA KUJIUNGA
(xi) KUANDAA TAARIFA YA WANACHAMA WALIOONDOKA KWA MUJIBU WA SEHEMU YA KUMI YA KATIBA KIF. 10.1 - 10.10
(xii) KUFANYA MAAMUZI YALIYO NDANI YA MAMLAKA NA UWEZO WAO
(xiii) KUFANYA KAZI ITAKAYOAGIZWA NA MKUTANO MKUU.
(xiv) KUPIGIA KURA MAJINA MAWILI YA KUPATA WAJUMBE WAWILI KATI YA MAJINA MANNE YALIYOPENDEKEZWA NA KAMATI TENDAJI: WATAKUWA JINSIA YA KE (1) NA ME (1)
(xv) KUPIGIA KURA MAJINA MAWILI KATI YA MANNE YA JINSIA YA KE (1) NA ME (1) AMBAO NI WASTAAFU AU TAALUMA, HEKIMA NA BUSARA ILI KUPATA WASHAURI NDANI YA ASASI AMBAO SI WANACHAMA WA MFAWICA KUTOKA KATIKA JAMII.
14.3.0 MKUTANO WA DHARURA
14.3 UTAKUWA WA MKUTANO MKUU TU
(i) UTAANDALIWA NA KAMATI TENDAJI NA KUTOLEWA WITO KWA WANACHAMA NDANI YA SIKU (5) TANO TU
(ii) UTAZUNGUMZIA JAMBO LA DHARURA TU
(iii) UTAONGOZWA NA MWENYEKITI KAMA HAYUPO ATACHAGULIWA MWENYEKITI TOKA MIONGONI MWAO KUONGOZA
(iv) USIPOFANYIKA MKUTANO HAUTAITISHWA TENA, ILA VIONGOZI WAANDAMIZI WA ASASI WATACHUKUA JUKUMU LA DHARULA HIYO
14.4 MUUNDO WA UONGOZI
(i) MWENYEKITI
(i MAKAMU MWENYEKITI
(iii)KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI
(iv)KATIBU MSAIDIZI
(v) MHASIBU/MWEKA HAZINA
(vi)MRATIBU
(vii)WAKUU WA IDARA
(viii) WAJUMBE WAWILI – WANA ASASI
(ix) WASHAURI WAWILI – KUTOKA KATIKA JAMII (WENYE MAARIFA, WENYE UJUZI)
(x) WAKUU WA IDARA NANE (8) ZA ASASI
KATIKA MATAWI HAKUTAKUWEPO MKURUGENZI MTENDAJI NA,MRATIBU BALI KATIBU TU NA MWENYEKITI KWA MAJUKUMU MENGINE YANASALIA KUWA KAMA ILIVYO KATIKA KATIBA HII
SEHEMU YA KUMI NA TANO
15.0 MGAWANYO WA MAJUKUMU YA VIONGOZI
15.1 MAJUKUMU YA MWENYEKITI
(i) MSEMAJI MKUU WA ASASI KATIKA MAAMUZI YALIYOTOLEWA NA MKUTANO MKUU.
(ii) MWENYEKITI WA VIKAO VYA KIKATIBA VYA ASASI
(iii) ATAKUWA NA KURA YA TURUFU
(iv)KUTIA SAINI KATIKA:- MIKATABA, NYARAKA NYETI, MAMBO YA SERA, SHERIA N.K. ZIHUSUZO ASASI
(v) KUTIA SAINI KATIKA HUNDI NA NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI
(vi) KUKASIMU MADARAKA PINDI HAYUPO ENEO LA ASASI.
15.2 MAJUKUMU YA MAKAMU MWENYEKITI
(i) ATAFANYA KAZI ZOTE ZA MWENYEKITI PINDI HAYUPO
(ii) ATASHUGHULIKIA MASUALA NA MAJUKUMU YA KILA SIKU KAMA WANACHAMA WENGINE.
(iii) ATAFANYAKAZI ATAKAYOAGIZWA NA MKUTANO MKUU NA KAMATI TENDAJI
(iv) HATAKUWA NA MADARAKA YA KUTIA SAINI KATIKA HUNDI NA NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI TOKANA NA TARATIBU ZA KIBENKI.
15.3 MAJUKUMU YA KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI
(i) MSIMAMIZI MKUU WA SHUGHULI ZOTE ZA UTENDAJI NA UTAWALA WA ASASI
(ii) ATASIMAMIA UANDAAJI WA MIRADI YOTE YA ASASI
(iii)ATASHIRIKIANA NA WAKUU WA IDARA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA ASASI.
(iv) ATAANDAA NA KUTOA TAARIFA YA SHUGHULI ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI NA ZA UTENDAJI KWA MKUTANO MKUU NA KAMATI TENDAJI.
(v) KUANDIKA MIHTASARI YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA ASASI.
(vi) KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA MIHTASARI YOTE YA ASASI.
(vii) KUSHIRIKIANAN A WAKUU WA IDARA KUANDAA:- MIKATABA, NYARAKA NYETI, SERA, MIONGOZO, TARATIBU, KANUNI N.K. ZA ASASI.
(viii) ATASHUGHURIKIA AJIRA NA KUONDOA AJIRA NDANI YA ASASI
(ix)KUWA NA MAHUSIANO MAZURI KWA WADAU, WAFADHILI, WAHISANI, WATAALAM, WASHAURI, SERIKALI KATIKA NYANJA ZA KUKUZA NA KUBORESHA UTENDAJI WA ASASI KWA KUPATA FEDHA, MALI, USHAURI N.K.
(x) KUJIBU BARUA ZOTE ZA MAWASILIANO YANAYOHUSU SHUGHULI NA UTEKELEZAJI WA ASASI.
(xi) MSHAURI MKUU WA MWENYEKITI WA ASASI.
(xii)KUTOA TAARIFA YA MKUTANO KWA WANACHAMA SIKU SABA (7) KABLA YA KIKAO.
(xiii)MSIMAMIZI MKUU WA FEDHA NA MALI ZA ASASI.
(xiv) KUIDHINISHA MALIPO YA SHUGHULI ZOTE ZA ASASI.
(xv)KUTIA SAINI KATIKA HUNDI NA NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI.
(xvi) ATAKUWA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI.
(xvii)MTIA SAINI KATIKA NYARAKA NYETI, MIKATABA, SERA, SHERIA, VYETI NA VITAMBULISHO VYA ASASI.
15.4 MAJUKUMU YA KATIBU MSAIDIZI
(i) ATAFANYA KAZI ATAKAZOAGIZWA NA KATIBU AKIWA YUPO NJE YA ASASI AU AKIWA NA MAJUKUMU MENGINE.
(ii) ATAFANYA SHUGHULI YOYOTE ATAKAYOAGIZWA NA MKUTANO MKUU NA KAMATI TENDAJI
(iii) ATAFANYA SHUGHULI ZA KILA SIKU ZA ASASI KAMA WANACHAMA WENGINE.
15.5 MAJUKUMU YA MHASIBU / MWEKA HAZINA
(i) KUTOA STAKABADHI YA FEDHA INAYOPOKELEWA.
(ii) KUPELEKA FEDHA BENKI KATIKA AKAUNTI YA ASASI.
(iii) KUTUNZA KUMBUKUMBU YA MAPATO NA MATUMIZI.
(iv)KULINGANISHA MAPATO NA MATUMIZI KILA SIKU.
(v) KULINGANISHA BENKI STATEMENT NA VITABU VYA ASASI KILA MWEZI.
(vi)KUANDAA TAARIFA YA MWEZI, ROBO, NUSU, MIEZI 9 NA MWAKA; TAARIFA YA FEDHA.
(vii)KUTOA TAARIFA YA FEDHA YA MAPATO NA MATUMIZI KATIKA VIKAO VYA KIKATIBA NA UTENDAJI.
(viii)ATAWAJIBIKA KATIKA MASWALA YOTE YA FEDHA KWA KUTUMIA MWONGOZO WA FEDHA.
(ix) ATAANDAA MAKADIRIO/BAJETI YA ASASI YA MWAKA
(x) ATAIDHINISHA MALIPO/MATUMIZI YA FEDHA PINDI KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI AKIWA SAFARINI/NJE YA KITUO KWA BARUA RASMI.
(xi) KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA TAASISI ZA FEDHA, SERIKALI NA ASASI NYINGINE ZA KIFEDHA
(xii)ATAKUWA MSHAURI WA MWENYEKITI NA KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI KATIKA MASWALA YA FEDHA
(xiii) ATASIMAMIA FEDHA YA MATUMIZI MADOGO MADOGO KUPITIA PETTY CASH SYSTEM
(xiv) KUTIA SAINI KATIKA HUNDI NA NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI
(xv) ATAFANYA KAZI NYINGINE KAMA ATAKAVYOELEKEZWA NA MKUTANO MKUU, MWENYEKITI, KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI
(xvi) ATAKUWA KATIBU WA KAMATI TENDAJI
(xvii) ATATUNZA MIHTASARI YA VIKAO VYA KAMATI TENDAJI NA KUANDAA MIKUTANO
15.6 MAJUKUMU YA MRATIBU
(i) KUANDIKA MICHANGANUO YA MIRADI YA ASASI
(ii)KUTAFUTA/KUIBUA MIRADI NA KUIFUATILIA ILI KUPATA FEDHA KWA KUENDESHEA SHUGHULI ZA ASASI
(iii)KUSHIRIKIANA NA KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI KUFANYA MAWASILIANO NA UHUSIANO WA KARIBU NA WAFADHILI AMBAO ASASI ITAKUWA IMEPATA FEDHA YA MRADI AU INAPOTAFUTA FEDHA KWA WAFADHILI.
(iv) KUSHIRIKIANA NA MHASIBU NA MKURUGENZI MTENDAJI KATIKA UANDAAJI WA BAJETI YA MRADI UTAKAOKUWA UNAOMBEWA FEDHA KWA MFADHILI.
(v)KUANDAA SHUGHULI ZA MRADI AMBAO UTAKUWA UMEPATA FEDHA YA RUZUKU.
(vi)KUFANYA MREJESHO WA SHUGHULI ZA MRADI ULIOTEKELEZWA KWA MKURUGENZI MTENDAJI KATIKA MUDA WA SIKU 5 BAADA YA KUFANYIKA.
(vii)KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA MRADI
(viii)KUTOA USHAURI KWA MKURUGENZI MTENDAJI JUU YA MASWALA MUHIMU YA KUFANIKISHA LENGO MAHUSUSI, LENGO KUU NA SHUGHULI ZA MRADI.
(ix)KUTOA TAARIFA YA SHUGHULI ZAKE KATIKA KIKAO CHA KAMATI TENDAJI.
(x)KUFANYA KAZI YOYOTE ATAKAYOELEKEZWA NA MKURUGENZI MTENDAJI
(xi)KUTIA SAINI KATIKA HUNDI NA NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI.
15.7 MAJUKUMU YA WAKUU WA IDARA
(i) YATOKANAYO NA SEHEMU YA NNE YA KATIBA
(ii) YATOKANAYO NA MAELEKEZO YA MKUTANO MKUU
(iii) YATOKANAYO NA MAELEKEZO YA MKURUGENZI MTENDAJI
(iv) ATAWAJIBIKA KUANDAA MAJUKUMU YA IDARA YAKE
(v) MJUMBE WA KAMATI TENDAJI
15.8 MAJUKUMU YA WAJUMBE NA WASHAURI
(i)KUTOA USHAURI KWA MWENYEKITI, MKURUGENZI MTENDAJI, MHASIBU NA MRATIBU KWA UFANISI WA ASASI.
(ii)KUKUTANA NA KAMATI TENDAJI KWA MWAKA MARA MBILI KWA LENGO LA KUONA UFANISI NA UTENDAJI WA SHUGHULI ZA ASASI KWA MIEZI SITA NA MWAKA MZIMA.
(iii) WATAKUWA CHOMBO CHA KUSULUHISHA MIGOGORO, MIGONGANO NA DHANA YOYOTE POTOFU KWA MANUFAA YA ASASI.
(iv)WATAKUWA NI WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA ASASI.
SEHEMU YA KUMI NA SITA
16.0 WAJUMBE WA KAMATI TENDAJI
16.1 MWENYEKITI
16.2 MAKAMU MWENYEKITI
16.3 KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI
16.4 KATIBU MSAIDIZI
16.5 MHASIBU/MWEKA HAZINA
16.6 MRATIBU
16.7 WAKUU WA IDARA
16.8 WAJUMBE (2)
16.9 WASHAURI (2)
SEHEMU YA KUMI NA SABA
17.0 UTAWALA WA ASASI
17.1 UTAWALA WA ASASI UTAKUWA CHINI YA KAMATI TENDAJI
17.2 VIONGOZI WAANDAMIZI WATAKAO WAJIBIKA SIKU KWA SIKU KUANDAA NA KUJIBU SHIDA MBALIMBALI WATAKUWA NI :-
(i) KATIBU / MKURUGENZI MTENDAJI
(ii) MHASIBU / MWEKA HAZINA
(iii) MRATIBU
17.3 KATIKA NGAZI YA TAWI VIONGOZI WATAKAO WAJIBIKA SIKU HADI SIKU NI :
(I) KATIBU WA TAWI
(II) MWEKA HAZINA WA TAWI
NA VIONGOZI HAO WATA WAJIBIKA MOJA KWA MOJA KATIKA KAMATI TENDAJI YA
TAWI KWA SHUGHULI ZA KILA SIKU
SEHEMU YA KUMI NA NANE
18.0 MIIKO YA UONGOZI
18.1 KUTOTOA SIRI ZA ASASI JUU YA JAMBO LOLOTE AMBALO HALITATOLEWA
MAAMUZI NA VIKAO
18.2 KUTOSABABISHA, KUCHOCHEA , KUFANYA VURUGU, KUGOMBANA, N.K. NDANI
YA MAENEO YA ASASI NA NJE PIA.
18.3 KUTOTUMIA MALI, FEDHA NA RASLIMALI YA ASASI KWA MANUFAA BINAFSI.
18.4 KUTOTOA RUSHWA AU KUPOKEA RUSHWA WAKATI WA SHUGHULI ZA ASASI.
18.5 KUTOHESHIMU MISINGI YA IMANI YA DINI, MILA NA DESTURI, JINSIA NA UTU.
18.6 KUTOJIHUSISHA NA MAMBO YA ITIKADI ZA KISIASA NA DINI
18.7 KUTOHESHIMU VIONGOZI WA ASASI PIA WANACHAMA
18.8 KUTOTIMIZA NA KUMALIZA KAZI ULIYOPANGIWA/AGIZWA NA MKUTANO MKUU,
KAMATI TENDAJI, MKUU WA IDARA AU WAJUMBE NA WASHAURI KWA MUDA
MAALUM.
18.9 KUTOTUMIA NEMBO YA ASASI, MIHURI NA KIELELEZO CHOCHOTE KILE CHA ASASI
KWA MANUFAA BINAFSI.
SEHEMU YA KUMI NA TISA
19.0 MIPANGO NA MIKAKATI YA ASASI KUFIKIA MALENGO YAKE
19.1 KUAJIRI WATU WAZOEFU NA WENYE TAALUMA ILI KUBORESHA SHUGHULI ZA ASASI
19.2 KUTAFUTA FEDHA KUTOKA KWA WAFADHILI, WADAU, SERIKALI, WATU BINAFSI, MASHIRIKA, TAASISI ZA KIBENKI ILI KUENDESHEA MIRADI YA ASASI.
19.3 KUKUSANYA FEDHA YA ADA, MICHANGO NA VIINGILIO KWA KUTEKELEZA KAZI ZA ASASI.
19.4 KUWA NA MIPANGO YA MUDA MFUPI NA MUDA MREFU NA INAYOELEWEKA KWA UTEKELEZAJI.
SEHEMU YA ISHIRINI
20.0VYANZO VYA MAPATO
20.1 ADA, VIINGILIO NA MICHANGO
20.2RUZUKU NA UFADHILI KUTOKA KWA SERIKALI, MASHIRIKA, WATU BINAFSI NDANI YA TANZANIA NA NJE YA TANZANIA.
20.3 MIKOPO YA WAHISANI, SERIKALI, BENKI, MASHIRIKA YA DINI, MASHIRIKA YA UMMA NA WATU BINAFSI
20.4 UFUGAJI NYUKI NA KUUZA ASALI
20.5 UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MABWAWA NA KUUZA
20.6KILIMO CHA MAZAO YA BIASHARA NA CHAKULA
20.7MICHANGO YA UTUNISHAJI MFUKO
20.8 MALIPO YA HUDUMA KWA WATALII
20.9MAZAO YA ASILI YATOKANAYO NA UHIFADHI WA MALI ASILI.
20.10 MALIPO YATAKAYOTOLEWA NA WATAFITI WA MALI ASILI MAENEO
YANAYOHIFADHIWA NA ASASI
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
21.0 MATUNZO YA FEDHA NA KUMBUKUMBU
21.1 FEDHA YOTE ITAPOKELEWA KWA KUTOA STAKABADHI
21.2 KUPELEKA FEDHA BENKI KWENYE AKAUNTI YA ASASI
21.3 KUWEKA KUMBUKUMBU KATIKA VITABU VYA KIHASIBU
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
22.0MATUMIZI YA FEDHA
22.1 UCHAPAJI, KURUDUFU, SHAJARA N.K.
22.2PANGO LA OFISI, UMEME, MAJI, VIFAA VYA OFISI N.K.
22.3 MAWASILIANOKAMA : SIMU, EMS, INTERNET, POSTA SANDUKU LA BARUA, EMS N.K.
22.4 GHARAMA ZA USHAURI WA SHERIA NA UHASIBU
22.5 POSHO KWA WATENDAJI WENYE TAALUMA N.K.
22.6MATIBABU YA WANACHAMA/WAFANYAKAZI
22.7SAFARI ZA KIKAZI ZA ASASI
22.8 KUNUNUA SAMANI, RASLIMALI, ARDHI, MITAMBO N.K.
22.9UJENZI WA SHULE, OFISI YA ASASI, BARABARA, ZAHANATI N.K.
22.10 KUFUATA MAKISIO/BAJETI YA ASASI
22.11 MALIPO KUANZIA LAKI TANO YATATUMIA UTARATIBU WA MANUNUZI KWA UGAVI NA KAMATI TENDAJIITAPITIA MAOMBI YA UGAVI KUANZIA 3 NA KUENDELEA.
22.12 MISAADA YA DHARULA PANAPOTOKEA MAJANGA YANAYOATHILI JAMII KILA INAPOBIDI.
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
23.0 UTARATIBU WA MALIPO
23.1 KUWEPO KWA HATI ZA MATUMIZI KAMA ; ANKARA, MADAI YA AWALI, BARUA, STAKABADHI N.K.
23.2 HATI YA MALIPO – PAYMENT VOUCHER YA ASASI
23.3 VIAMBATANISHO KWENYE PAYMENT VOUCHER
23.4 MAELEZO KAMILI KATIKA HATI YA MALIPO :- MTAYARISHAJI, MKAGUZI,
MUIDHINISHAJI MALIPO N.K.
23.5 JINA KAMILI NA ANUANI YA MLIPWAJI NA AINA YA MALIPO KAMA NI TASLIMU AU HUNDI / NA KIASI KILICHOLIPWA
23.6 HATI YA MALIPO NA VIAMBATANISHO KUPIGWA MUHURI WA ASASI
ULIOANDIKWA « PAID »
23.7 STAKABADHI AU SAHIHI YA MLIPWAJI KUSAINI KATIKA VOUCHER ILIIYOKAMILIKA
23.8 KUINGIZA HATI YA MALIPO / PV KATIKA CASH BOOK KWA TAREHE MALIPO YALIPOFANYIKA NA KUIWEKEA NAMBA NA KUIFAILI.
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
24.0 WAWEKA SAINI KATIKA HUNDI/NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI
24.1 KUNDI : A :
(i) MWENYEKITI
(ii) MKURUGENZI MTENDAJI
24.2 KUNDI : B :
(i) MHASIBU/MWEKA HAZINA
(ii) MRATIBU
NB : MALIPO YATAFANYIKA KWA MTU MMOJA ; KUNDI ‘’A’’ WA PILI ‘’B’’ NA SIO TOKA KUNDIMOJA TU ie. ‘’A’’ TU / ‘’B’’ TU
24.3 KATIKA NGAZI YA TAWI :
WATIA SAINI : KUNDI A. (I) MWENYEKITI WA TAWI
( II) KATIBU WA TAWI
WATIA SAINI : KUNDI B ; (I) MWEKA HAZINA WA TAWI
(II) MJUMBE MMOJA WA TAWI
NB : MALIPO YATAFANYIKA KWA MTU MMOJA ; KUNDI ‘’A’’ WA PILI ‘’B’’ NA SIO TOKA KUNDI MOJA TU ie. ‘’A’’ TU / ‘’B’’ TU
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
25.0 ELIMU NA MAFUNZO KWA WANACHAMA WAAJIRIWA
25.1 ASASI ITAWALIPA WANACHAMA NA WATAALAM WATAKAOONYESHA BIDII YA
KUFANIKISHASHUGHULI ZAO KWA MANUFAA YA MFAWICA
25.2 ASASI ITAGHARAMIA MAFUNZO YA MUDA MREFU, MFUPI, SEMINA, WARSHA, ILI KULETA UFANISI.
25.3 WALE WATAKAOFANIKIWA KUIPATA HIYO ELIMU WATAITUMIA KUFUNDISHA WENGINE KWA MANUFAA YA ASASI.
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
26.0WAJIBU NA MAADILI YA WAFANYAKAZI WAAJIRIWA
26.1 WATATENDA KAZI ZAO CHINI YA MKURUGENZI MTENDAJI
26.2WATAKUWA WASHAURI WA MKURUGENZI MTENDAJI
26.3 WATAFANYA KAZI KWA TAALUMA ZAO
26.4 WATAPASWA KUJENGA HESHIMA WAO KWA WAO, KWA VIONGOZI,
MKURUGENZI MTENDAJI, WANACHAMA NA WANA JAMII WOTE.
26.5 HATUA ZA KINIDHAMU ZITACHUKULIWA WAKATI WOWOTE KWA YULE
ATAKAYEONESHA UTOVU WA NIDHAMUKWA MUJIBU WA SEHEMU YA KUMI NA NANE YA KATIBA
26.6WATAJAZA MIKATABA YA AJIRA/KAZI NA KUSAINIWA PANDE ZOTE MBILI
26.7MAOMBI YAO YATATUMWA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA ASASI AMBAYE ATAYAFANYIA KAZI NA KUTOA MAJIBU NDIYO/HAPANA.
26.8 TUNU/ZAWADI ITATOLEWA KWA MWAJIRIWA NA MWANACHAMA YEYOTE ATAKAYEONESHA JUHUDI NA UFANISI WA KAZI KWA FAIDA YA ASASI NA JAMII KWA UJUMLA KATIKA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI.
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
27.0UUNDAJI WA KAMATI YA UCHUNGUZI/UKAGUZI
27.1 Kamati Ya Uchunguzi/Ukaguzi Itatoka Nje Ya Asasi
27.2Mkutano Mkuu Ndio Wenye Uwezo Wa Kuamua Hili
27.3 Itafanya Kazi Kwa Muda Wa Majuma Mawili Tu Kwa Kulipwa Gharama Zao Kwa Kazi Husika Kwa Makubaliano.
27.4 Hazitakuwa Za Kudumu
27.5 Taarifa Ya Kazi Yao Itatumwa Kwa Mwenyekiti Wa Asasi Ambaye
Ataitisha Kamati Tendaji Kuipitia Kabla Ya Kwenda Mkutano Mkuu Kwa Hatua Nyingine
27.6Baada Ya Mkutano Mkuu Taarifa Hiyo Itabaki Kwa Mkurugenzi
Mtendaji Kwa Kazi Ya Asasi (Kiutawala)
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
28.0 MAWASILIANO
28.1 asasi itafanya mawasiliano sehemu mbalimbali kwa ajili ya shughuli zenye manufaa na maendeleo kwa njia kama vile:-
(i) posta - rejesta
(ii) ems
(iii) barua pepe
(iv) sanduku la barua
(v) mtandao(Website)
(vi) fax
(vii) simu ya mezani
(viii) simu ya mkononi n.k
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
29.0UBIA
29.1 Kufanya Ubia Kwa Uhuru
29.2Kufanya Ubia Na Serikali, Asasi, Cbo, Mdau, Mfadhili, Mtu Binafsi,
Shirika, Taasisi Ya Dini, Benki.
29.3 Kutuma Barua Ya Maombi Kwa Mkurugenzi Mtendaji Wa Asasi
29.4 Kujaza Fomu Ya Makubaliano Pande Mbili Ambayo Itakuwa Na
Utaratibu Wa Mkataba Wa Muda Mrefu Au Mfupi
29.5 Kutoa Kiingilio Cha Ubia Sawa Na Itakavyojadiliwa Na Mkutano Mkuu.
29.6Ubia Utakuwa Na Muda Ambao Ni Makubaliano Ya Asasi Na Mbia
29.7Kukubali Kutoa Michango Ya Hiari Kwa Kazi Ndani Ya Ubia
29.8 Ubia Unaweza Kufutwa Wakati Wowote Endapo Masharti Yaliyomo
Ndani Ya Mkataba Yatakiukwa
29.9Mkataba Wa Ubia Utafutwa Kwa Makosa Ya Jambo La Jinai – Hatua Za
Kisheria Zitachukuliwa Kwa Kufungua Kesi Na Utaratibu Wote
Utafuatwa. Kama Yatakavyokuwa Makubaliano.
29.10 Mkataba Utawekewa Saini Na Muhuri Toka Pande Zote Mbili
Zinazokubaliana.
29.11 Mkataba Wowote Utakaofanywa Kati Ya Asasi Na Mbia, Patakuwa Na
Mashahidi, Ikibidi Wa Kisheria Za Mahakama.
SEHEMU YA THELATHINI
30.0 KUHESHIMU MAAMUZI YA MKUTANO MKUU, KAMATI TENDAJI NA KATIBA YA ASASI NA MIONGOZO NA KATIBA YA NCHI.
30.1 Mambo Ambayo Hayakuandikwa Ndani Ya Katiba Na Miongozo/Kanuni
Yataamuriwa Na Mkutano Mkuu.
30.2 Mkutano Mkuu Utachukua Hatua Ya Jambo Lolote Lenye Utata Baada
Ya Kuwa Limeanzia Katika Idara Kupitia Kamati Tendaji Ambayo Ni
Chombo Kikubwa Katika Utendaji Wa Asasi.
30.3 Jambo Ambalo Litaonekana Kuleta Athari Katika Asasi Ruhusa
Itatolewa Na Kupeleka Jambo Hilo Mahakamani Baada Ya Taratibu
Kukamilika Na Kusimamiwa Na Mkurugenzi Mtendaji Wa Asasi.
SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
31.0 KUVUNJIKA KWA ASASI
31.1 Mkutano Mkuu Utaitishwa
31.2 Agenda Ya Kuvunja Asasi Itatolewa
31.3 Viongozi Wa Serikali Na Mtandao Wa Wilaya Ya Kigoma Wataalikwa
Katikamkutano
31.4 Kabla Ya Uamuzi Wa Kuvunja Madeni Yote Yatalipwa Kwanza
31.5 Mali Zitakazosalia Hazitagawiwa Kwa Mwanachama Yeyote.
31.6 Wajumbe Wapatao Theluthi Mbili Ndiyo Watakuwa Na Uamuzi Wa
Mwisho Kwakupiga Kura Za Siri.
31.7 Kamati Ya Kusimamia Na Kulinda Mali Itaundwa
31.8 Mali Zote Zitagawiwa Mashirika Yenye Lengo Sawa Na Mfawica
31.9 Kuvunjika Kwa Asasi Kutatolewa Taarifa Katika Serikali Mtandao (W)
Kigoma, Pia Kutangazwa Katika Vyombo Kama Vile:- Radio, Gazeti, Mbao
Za Matangazo N.K.
31.10 Zoezi Litakamilika Ndani Ya Siku 30 Tu.
SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI
32.0 ORODHA YA WANACHAMA WAANZILISHI – MWAKA 2005
MAJINA YAO KAMILI
- RAMADHANI NYUNDO SIKA
- BARAKA PETER NZOVU
- SILINDILA ATHUMAN KALIMBA
- SALUM SHABAN KITOPENI
- AKSA ANDREA CHAGAMBA
- MOHAMED HAMIS KALIMANZILA
- 0MAKELELE MASANYUKE KIKOMO
- MOSHI HARUNA MADIGIDI
- UHURU HAMIS BUTATI
- RAULENTI RICHARD GABRIEL
33.0 ORODHA YA WANACHAMA WAPYA WA KUJIUNGA MWAKA 2009/12
MAJINA YAO KAMILI SAHIHI ZAO TAREHE
1. MWAMBA A. KIEMENA …………………….. ………………………..
2. Hamisi Almasi …………………………... ……………………….
3 ALEX EKAMA MNENE …………………………… ………………………
4 Simoni Patilo Bwilo …………………………… ……………………
5 Imani Richard Gabriel …………………………… ………………….
6 Simon Petro ……………………………. …………………..
7 Laimond Simon ……………………. ...................
8 Rajabu Juma Madolla …………………………….. …………………….
9 Rajabu Kakumo ……………………………. …………………….
10Shabani Mussa Kibanga …………………………… ……………………..
11Mashaka Almas …………………………… …………………….
12Shabani Kijungi ………………………….. ……………………..
13 Goodnes Issak Baziyaka ……………………………. ……………………
14 Issa Lufwifwi. ……………………………. ……………………
15 Abdallah Mussa. …………………………….. …………………..
MWISHO
Maoni (2)