ALIYEVUNJWA TAYA AFANYIWA OPARESHENI, NDUGU WAOMBWA KUJITOKEZA
Emmanuel Nelson Chitepete akiwa hospitalini.
Wandishi wa Global TV Online & Mtandao, Gabriel Ng’osha, akikabidhi fedha kwa msimamizi wa wodi, Sista Masumbuko kutoka kwa Wasamaria wema waliochanga ili kumtibu mgonjwa huyo.
KIJANA Emmanuel Nelson, mkazi wa Tabata-Relini, jijini Dar es Salaam, ambaye aliokotwa na polisi wa kituo cha Pangani, Ilala, wiki kadhaa zilizopita akiwa amevunjwa taya na watu wasiojulikana, wiki iliyopita alifanyiwa oparesheni na kufungwa waya taya lililovunjika.
Akizungumza na mtandao GPL, mmoja wa maofisa Ustawi wa Jamii jijini (hakutaka kutajwa jina lake) ambaye amekuwa akifuatilia kwa karibu matibabu ya kijana huyo alisema mgonjwa huyo anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa oparesheni.
Hata hivyo, aliongeza kwamba bado hajatulia kiakili kwani kuna wakati anazungumza vizuri na wakati mwingine anakuwa kama anarukwa na akili. Pamoja na hali hiyo, alisema, bado watoa huduma wanajitahidi kuendelea kumsaidia.
Ofisa huyo alisema Emmanuel ameweza kumtaja baba yake mzazi anayejulikana kwa jina la Nelson Andrew Chitepete, mkazi wa Chamwino, Area ‘’A’’ Dodoma ambaye pia ni mfanyakazi mstaafu wa Tanzania Railway Company (TRC) Dodoma.
Alitoa wito kwa yoyote anayemfahamu Emmanuel, akiwemo mzee Chitepete wawasiliane na namba ya simu 0655207156 au kufika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wodi ya Sewa Haji namba 23.
(Habari/Picha: Gabriel Ng’osha/GPL)
MAISHA NI CONNECTION HAIJALISHI UMEPATA AU LAAH!
Picha hii inanikumbusha mwaka 2012, nikiwa jijini dar, nikapendekezwa na vijana wa kuchukuliwa fomu ya kugombea uwakilishi wa baraza kivuli wa vijana wa Wilaya ya Magu mjini.
Napenda kuwashukuru vijana wote walionipendekeza na kunichagua, hakika ni upendo wa dhati sana.(mimi ni wa tatu kutoka waliokaa upande wa kushoto ukutani)
KAMPENI YA AFYA YA MAMA NA MTOTO YAJA
Sehemu ya harakati za taasisi ya MAISHA PA1, katika maandalizi ya wimbo wa kampeni ya afya ya mama na mtoto.
Mmoja wa mama mjawazito pamoja na watoto wakiwa katika wodi ya wajawazito katika hospitali ya Amana, jijini Dar es Salaam