Parts of this page are in Swahili. Edit translations
HOTUBA YA MKURUGENZI MTENDAJI MBARALI MHESHIMIWA GEORGE KAGOMBA KWENYE SEMINA YA MAFUNZO YA PETS YALIYYOENDESHWA NA ASASI YA MAGEA KWA UFADHILI WATHE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY TAREHE 12/11/2011, MJINI RUJEWA MBEYA.
Mhe: Mkurugenzi alianza kwa kutoa shukrani kwa mwaliko wa kuja kufunga semina na hatimaye kukabidhi vyeti vya kufuzu washiriki wa mafunzo ambao ni wananchi wa vitongoji vine(4). Pia alipongeza wananchikwa ari yao ya ushiriki wa mafunzo hayo kwani alisema sasa “mmepata fursa nzuri ya kujua haki zenu kupitia mafunzo haya.”
Akielezea na kufafanuakuhusu(PETS) mkurugenzi alisema “mafunzo ya ufuatiliaje wa fedha za umma ni muhimu kwa wananchi na tunaipongeza sana sasa Asasi ya MAGEA kwa kutuletea mafunzo haya ambayo serikali imeridhia kufanyika kisheria hali itakayowajengea wananchi uelewa wa mambo yafuatayo:-
1. Fedha zinazoingia katika sekta au miradi mbalimbali.
2. Vifaa vinavyoingia katika serikali na taasisi zake.
3. Kuhoji mpangilio wa matumizi yake.
4. Kuangalia ubora wa huduma.
5. Kuuliza maswali kwa watendaji na kutoa ushauri kwa uhuru pale inapobidi.
Kushirikiana na vyombo vya dola hususani(POLISI NA TAKUKURU) iwapo wananchi watabaini kuwa kuna ubadhirifu wa matumizi mabaya ya Rasilimali au fedha za umma zinazotengwa katika miradi husika.
Akiendelea Mkurugenzi alisema ni vizuri mafunzo haya yakafanyika mara kwa mara na MAGEA mmetusaidia sana kwa hili, kwani serikali haina watumishi wa kutosha kuendesha elimu hii hivyo kwa kuwa leo mmekuwa na mradi wa afya tunahitaji mafunzo katika mradi mingine kama ELIMU, MAZINGIRA, UTAWALA BORA, ARDHI n.k hivyo natoa wito kwa Asasi nyingine kuiga mfano huu kwa kujikita kutoa mafunzo kwa wananchi badala ya mazoea ya kutoa mafunzo na semina kwa watumishi au wafanyakazi tu.
Akiongelea suala la ushirikiano kati ya viongozi wa ngazi mbalimbali wilayani na Asasi za Kiraia Mhe Kagomba alisema “viongozi wenzangu wa Idara mbalimbali na madiwani imekuwa ni desturi baadhi yenu kuzichukia Asasi hizi kwa sababu mnaamini zinafichua mambo yenunasema na nasisitiza wapeni ushirikianohawa watu wa Asasi wanatusaidia kwani wao wapo jiwani sana na wananchi wetutujenge urafiki, tujenge mahusiano kwa kufanya hivyo tutadumisha misingi ya uwazi,Demokrasia na Maendeleo endelevu katika wilaya yetu.
Mwisho Alipongeza uwiano wa jinsia katika mafunzo hayo alisema “naona makundi yote ya jamii yamo humu, kuna walemavu, wazee, vijana na kinamama hali inayoashiria usawa kamili katika mafunzo yenu.
Alimalizia kwa kukabidhi vyeti kwa wahitimu na kuwatakia mafanikio na kuzingatia mafunzo waliyoyapata.
July 27, 2012