Envaya

Ludende Development Association

FCS Narrative Report

FCS Narrative Report

Utangulizi

Ludende Development Association
LUDA
Haki ya mwanamke kumiliki Ardhi
FCS/RSG/3/10/062
Tarehe: January 1,2011Kipindi cha Robo mwaka: April1,2011
Laban Shagama,
P.O.Box 133,
LUDEWA.
Mob. No. 0754 634 580
shagama2001@yahoo.com

Maelezo ya Mradi

Sera
Mradi wetu unakidhi Malengo ya eneo tulilolichagua hapo juu kama ifuatavyo:-
1. Mradi wetu umefanikiwa kuongeza uelewakwa wanawake juu ya haki ya mwanamke kumiliki ardhi sambamba na matakwa ya sera ya maendeleo kwa wanawake kifungu cha 3(2) na 4.2(b) kwamba mwanamke anahaki ya kumiliki na kutumia ardhi kama ilivyo kwa mwanaume.
2. Pia mradi wetu umeongeza uelewa kwa wanawake juu ya sheria ya ardhi Namba 5 ya 1999 ya ardhi ya vijiji.
MkoaWilayaKataVijijiIdadi ya Wanufaika
IringaLudewaLugarawa Shaurimoyo,Lugarawa,Lupefu na Mdilidili22,000
MundindiAmani,Mundindi,Njelela,
 Walengwa wa moja kwa mojaWalengwa wasio wa moja kwa moja
Wanawake41508626
Wanaume30636318
Jumla721314944

Shughuli na Matokeo ya Mradi

Wanawake wa kata ya Lugarawa na Mundindi wanauelewa wa kutetea na kudai haki ya kumiliki ardhi
1. Kuandaa vipeperushi 4250 vinavyoelezea umilikishaji wa ardhi kwa wanawake.
2. Kuendesha mikutano ya uhamasishaji juu ya haki ya mwanamke kumiliki ardhi kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya vijiji No. 5 ya mwaka 1999 kwa vijiji saba(7) vya kata ya Lugarawa na Mundindi kwa watu wapatao 4250
3. Kuendesha semina kwa wajumbe sabini (70) waliochaguliwa (majukwaa) kutoka katika vijiji vyao juu ya umuhimu wa umilikishaji ardhi na kutetea haki ya kumiliki ardhi kwa muda wa siku tatu.
4.Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mradi
1.Vipeperushi vya kufundishia vipatavyo 4260 viliandaliwa na wakufunzi watatu na mratibu wa mradi huu kuanzia tarehe 1/1/2011 hadi 4/1/2011
2. Mikutano ya uhamasishaji juu ya haki ya mwanamke kumiliki ardhi iliyojumuisha wanajamii wote ilifanyika katika vijiji vyote saba kama vilivyopangwa kwa kufuata ratiba iliyopangwa tangu tarehe 26/1/2011 hadi tarehe 1/2/2011 kwa kupitia kila kijiji.
3. Iliendeshwa semina kwa wanawake kumi kutoka kila kijiji ambao waliteuliwa na wenzao kutoka katika kundi la jamii husika(waliitwa Majukwaa) juu ya haki ya mwanamke kumiliki ardhi kwa kuzingatia sheria namba 5 ya ardhi ya mwaka 1999 na sera ya ardhi ya mwaka 2002 kwa muda wa siku tatu (3) kuanzia tarehe 02/02/2011 hadi tarehe 04/02/2011
4. Kufanya ufuatiliaji kwa muda wa siku saba kwa kupitia kila kijiji kilichoshiriki mafunzo.
Hakuna tofauti
1. Shughuli No. 1. Maandalizi ilitumika Tshs. 733,000
2. Shughuli No. 2. Mikutano ya uhamasishaji ilitumika Tshs.1,050,000
3. Shughuli No. 3. Semina ya majukwaa yaliyoundwa ilitumika Tshs. 3,449,000
4. Shughuli No. 4. Tathmini na ufuatiliaji ilitumika Tshs. 984,000
5 Shughuli No. 5. Utawala ilitumika Tshs.1,267,320

Mafanikio au Matunda ya Mradi

1. Semina na mikutano imeendeshwa vyema na hivyo wanawake wa kata ya Lugarawa na Mundindi wanuelewa wa kutetea na kudai haki yao ya kumiliki ardhi
1. Wanawake wameelewa na wametambua haki yao ya msingi ya kumiliki ardhi
2. Wanajamii wa kata ya Lugarawa na Mundindi wameanza kumilikisha ardhi kwa watoto wote sawa wa kike kama wanaume
1. Jamii nzima imeanza kutambua haki muhimu za wanawake zaidi ya umiliki wa ardhi
Hakuna tofauti

Mambo Mliyojifunza

Maelezo
Licha ya mila potofu kutoa mchango mkubwa kwa wanaume wengi kuwanyima wanawake haki zao, wanaume wengi walikuwa kikwazo kikubwa katika kuwapa wanawake haki yao ya kumiliki ardhi na hivyo tulipofika kijiji cha Amani wanawake waliomba kuwa katika timu itakayoendelea kutoa elimu wanaomba wanaume wahusike pia
Wanasemina waliomba semina hiyo isiishie kutoa elimu juu ya haki ya mwanamke kumiliki ardhi pekee bali iende hadi kumilikisha mali nyingine na haki za wajane pale waume zao wanapokuwa wamefariki
Tumejifunza kuwa baadhi ya viongozi wa serikali ya vijiji hawaungi mkono jitihada za Asaasi za kiraia, kwani kila tulipowashiorikisha hawakuwa karibu sana nasi kama Asasi.
Wanajamii na viongozi wa vijiji hawana uelewa juu ya sheria ya ardhi na. 5 ya mwaka 1999 sera ya maendeleo ya mwanamke ya mwaka 2002

Changamoto

ChangamotoNamna mlivyokabiliana nazo
Wanajamii wengi walikuwa wamebanwa sana na majukumu yao ya kila siku hasa ukizingatia msimu wenyewe ni msimu wa kilimo kwa eneo hili na hivyo kushindwa kufanya mikutano nyakati za kawaida yaani asubuhi au mchana.Mikutano ilifanyika nyakati za jioni wakati watu waliowengi wamesharudi kutoka mashambani
Kuna kijiji kimoja kulitokea na msiba wa mtu muhimu hapo kijijini na hivyo watu wote walienda kwenye msiba huo na hivyo tukashindwa kuendesha mkutano.Tulilazimika kutumia siku ya jumapili ya tarehe 31/1/2011 kufanya mikutano vijiji viwili badala ya kijiji kimoja
Baadhi ya viongozi wea vijiji viwili hawakutupa ushirikiano wa kutosha katika kutoa taarifa kwa wanajamii kuhusu kufanyika kwa mikutano ya hadharaTuliwasiliana na viongozi wa ngazi ya kata ili wawahamasishe hao viongozi kutoa matangazo ya ratiba ya mikutano kwa wanajamii wote
Kutokana na myumbo wa uchumi baadhi ya bidhaa zilikuwa zimeongezeka bei km. daftari na nauli za sehemu nyingine zilikuwa zimepanda zaidi kuliko zile tulizopangia bajetiKwenye bidhaa kama daftari Asasi ililazimika kutumia pesa kutoka kwenye mfuko wa Asasi. Lakini pia suala la Nauli tulikubaliana na wajumbe kuwa wajumbe wachangie kiasi kinachoongezeka kwenye nauli iliyopangwa

Mahusiano

WadauNamna mlivyoshirikiana nayo
Halmashauri ya wilaya (Idara ya maendeleo ya jamii)walishiriki nasi Kuendesha mikutano ya uhamasishaji, semina na maandalizi
Halmashauri ya wilaya (Idara ya Ardhi)walishiriki nasi Kuendesha mikutano ya uhamasishaji na semina
Mseti Development Asssociation (MDA)walishiriki nasi kutoa semina na maandalizi
Katibu Tarafa Alishirikiana nasi katika kuhamasisha

Mipango ya Baadae

Shughuli ZilizopangwaMwezi wa 1Mwezi wa 2Mwezi wa 3
Hakuna shughuli zilizopangwa kwakuwa mradi wetu ulikuwa wa miezi mitatu tu! na hivyo shughuli zake zimeisha

Walengwa Waliofikiwa

    Walengwa wa moja kwa mojaWalengwa wasio wa moja kwa moja
Wajane na WaganeWanawake116560
Wanaume320312
Jumla436872
Watu wanaoishi na VVU/UKIMWIWanawake2062
Wanaume2134
Jumla4196
WazeeWanawake310631
Wanaume416821
Jumla7261452
Watoto YatimaWanawake46180
Wanaume8460
Jumla130240
WatotoWanawake323704
Wanaume171284
Jumla494988
Watu wenye UlemavuWanawake48128
Wanaume4486
Jumla92214
VijanaWanawake668400
Wanaume462380
Jumla1130780
Watu wengineWanawake579219
Wanaume540201
Jumla1119420
(Hakuna jibu)

Matukio Mliyoyahudhuria

Aina ya TukioLiniMambo uliyojifunzaHatua zilizochukuliwa
Mafunzo ya usimamizi wa RuzukuDecember 20101. Utunzaji na usimamizi bora wa fedha
2. Kuandaa miradi kwa mti wa matatizo na mti wa suluhisho
Kutengeneza mfumo mzuri zaidi wa matumizi ya fedha katika shirika
Tamasha la asasi za kiraiaMei 20101. Vigezo vilivyotumika katika kupata mshindi wa Tuzo ya Asasi bora.
2. Maonesho ya shughuli za Asasi mbalimbali
Kujipanga kwa ajili ya kupata tuzo ya Asasi bora 2011

Viambatanisho

« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.