Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

vijana wa zanzibar wakosa maadili

A S KASONGO (Zanzibar)
May 27, 2011 at 11:55 AM EAT

Vijana wengi wa Zanzibar wanakosa maadili mema, kabla ya hapo vijana walikuwa na maadili mazuri

Je? kifanyike nini

 

Capt Hamza M. Omar (Rtd) (CODECOZ)
May 30, 2011 at 8:52 AM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

Wazee wawajibike. Kukosa maadili kwa vijana kunatokana na kutowajibika kwa wazee. Hao vijana wa zamani ambao walikua na maadili mema ni kutokana athari ya maadili mazuri ya wazee wao.

Mfano vijana wanaovaa vibaya na kwenda nusu uchu hawakii mapangoni wanaishi majumbani pamoja na wazee wao. Jee wazee hawayaoni hayo. Mtoto wako anapokuaga kwamba anakwenda disco usiku nakurudi saa nane au tisa usiku nawe ukamngojea kumfungulia mlango jee ni nani aliyekosa maadili ni kijana au mzazi. Nani alaumiwe

Kuna haja kubwa kwa wazazi kujirekebisha na kurudi katika malezi bora ambayo wazazi wetu walitupa ili kurekebisha maadili ya vijana wetu.

fikiri mvugaro (temeke)
June 8, 2011 at 12:41 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

kutokana na utandawazi uliopo sasa umekuja na vijana ndio walio upokea kwa kasi zaidi na kujikuta vijana wanafahamu mambo mengi zaidi kuliko wazee misemo na maneno yale ya kificho yaliokuwa yakitumika zamani kuwakanyia wa watoto sasa uwezi tena kumwambia mtoto akakuelawa au kina  kwa mfano zamani kijana wa miaka kumi na nane ajui  kuhusu maswala ya ngono wakati mwengine mpaka anaoa lakini ajui umo ndani afanye nini lakini sasa hivi mtoto wa mika mnne tayari anajua hata staili mbalmbali za kufanya ngono kwa hiyo ndugu yangu Hamza M.Omar swala ni kuomba mashirika ya kijmii taasisi mbalimali kutoa taalifa sahihi kuhusu utandawazi sasa kila kitu kina faida yake na asara yake 

asanteni sana

HAJI MWADINI (ZANZIBAR)
June 8, 2011 at 7:28 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

VIONGOZI NDIO WALIOTAKA VIJANA WAAPOTOKE KIMAADILI. FIKIRIA KILA KIONGOZI KWA NINI ANJIHALALISHIA KUNUNUA ARDHI NA BAADAE AMA KUIUZA KWA WAWEKEZAJI AU/NA KUJENGWA HOTELI ZA KITALII.....NA UFUSKA UNAOFANYIKA HUMO MH! USO HUWEZI KUFUNUA KAMA UTAONESHWA. KWA JAMII NAO KUWAPENDA WATOTO NA VIJANA WAO KIASI CHA KUWANUNULIA SIMU ZENYE MTANDAO HUKU WAKITAZAMA PICHA CHAFU WAELEWE WANAWAPOTOSHA KIMAADILI. HEE WAZAZI HATA WATOTO WAKIKATAZWA KUTOCHUKUA SIMU SHULE MNAGOMBA....MAPENZI GANI HAYO?

 HALI HII ITAENDELEA HADI PALE VIONGOZI KUANZIA NGAZI YA SHEHIA (KIJIJI) HADI TAIFA NA WAZAZI NDANI YA JAMII WATAPOJISAFISHA.

 

fikiri mvugaro (mwela theatre group temeke)
June 11, 2011 at 10:17 AM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

Asante sana Haji Mwadini kutoka Zanzibar kwa majibu yako mazuri lakini utakubaliana na mimi kuwa kila mtu ana haki ya kufanya biashara yeyote lakini bila kuvunja sheria ya Nchi.  kununua na kuuza Ardhi ni haki ya kila raia bila kujali kiongozi au mtu binafsi na kuhusu kujengwa Hoteli za kitalii sio tatizo sababu ni moja ya maendeleo swala la kutumia simu za gharama kwa wanafunzi wa shule hilo lipo wazi kuwa hapaswi kutumia  simu wakati wa akiwa shuleni lakini hukumbuke kuwa sasa shule nyingi wanafundisha Computer .

mimi na fikiria kuwa viongozi katika utandawazi  sio tatizo, tatizo jinsi tulivyo upokea uho utandawazi,hili ni jukumu la kila mmoja wetu katika jamii kuakisha vijana wanapewa taalifa sahihi kuhusu utandawazi na ukitaka kuwaficha unaweza usikie lengo asante fikiri mvugaro mwela theatre


Add New Message (Hide)

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.