Envaya

Habari wadau wote wa maendeleo,kwanaza poleni sana na harakati za kila siku za kuleta maendeleo hapa nchini kwetu,

Asasi yetu inatekeleza mradi wa uwajibikaji wa jamii katika kufuatilia rasilimali za umma sekta ya afya wilaya ya ulanga tarafa ya vigoi kata za msogezi na nawenge,tulianza na shuguli ya kuendesha mafunzo kwa viongozi na watendaji wa serikali,wananchi wa kawaida na wajumbe wa kamati za afya kutoka vijiji vya kata husika za mradi na baada ya mafunzo hayo tumeendesha mafunzo ya kina kwa sam timu iliyoteuliwa na washiriki na baada ya nafunzo tupo katika hatua muhimu ya utekelezaji wa mradi nayo ni kukusanya takwimu kutoka ngazi ya jamii,zahanati,vituo vya afya na kwa mganga mkuu wa wilaya.

Lakini chakusikitisha ni kwamba sehemu zote tumepata ushirikiano wa kutosha ila kikwazo kipo kwa mganga mkuu wa wilaya hataki kutoa taarifa na hana sababu yoyote ya kufanya hivyo, je kuna nini halmashauri ya wilaya ya ulanga kwenye sekta hiyo ya afya ? Tuna muomba mkaguzi wa hesabu za serikali kufanya ukaguzi maalumu kubaini kilichojificha ndani yake.

19 Mei, 2015
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (1)

kijogoo group for community development (Morogoro Manispaa) alisema:
Nawapenda wadau wote na ninashauri mjiunge na envaya
19 Mei, 2015

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.