Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Habari wana harakati,Kijogoo Group For Community Development ya Mjini Morogoro,inatoa taarifa kwa wadau juu ya mpango wake wa kutekeleza mradi wa SAM sekta ya Afya Tarafa ya Vigoi Wilaya ya Ulanga pindi tutakapoingiziwa fedha za Mfadhili.

Mradi huo utatekelezwa kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society ya Dar es Salaam nchini Tanzania.

Utekelezaji wa mradi huo utagharimu fedha kiasi cha Tsh,44,500,300/= shilingi milioni arobaini na nne laki tano na mia tatu za ki Tanzania.

Kata zitazohusika na mradi huu ni Kata za Nawenge na Msogezi, lengo ni kuwa na upatikanaji wa huduma bora zenye tija na ufanisi sekta ya Afya kwa wakazi wa kata hizo zilizoguswa na mradi.

ukiwa ni mdau wa maendeleo tunaomba ufuatilie hatua za utekelezaji wa mradi kwa kuzisoma kwa kuwa tutakuwa tukiziweka mara kwa mara kwenye mtandao.

 

Asante

wako katika maendeleo ya jamii

 

Ramadhan Said

Katibu - Kijogoo Group

 

February 26, 2014
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.