Envaya

JE NI MHIMU KWA SASA WAZEE WOTE TANZANIA KUPEWA PENSION JAMII BILA KUJALI ALIFANYA KAZI SERIKALINI AU LA?

NABROHO SOCIETY FOR THE AGED (MAGU,MWANZA,TANZANIA)
6 Juni, 2011 10:30 EAT

IDADI YA WAZEE WOTE TANZANIA INAKADIRIWA KUWA NI ASILIMIA 5.7 KATI YA WATU MILION 38, WAZEE HAWA WANATUNZA MAYATIMA ASILIMIA 53 YA MAYATIMA WOTE NCHINI NA KWAMBA ASILIMIA 90 YA WAZEE WOTE WANAKADIRIWA KWAMBA WANAISHI VIJIJINI  HELPAGE INTERANATIONAL KWA KUSHIRIKIANA NA NABROHO SOCIETY FOR THE AGED YA MAGU MWANZA-TANZANIA TUNAKAMPAINI KUBWA YA KUISHAWISHI SERIKALI IANZE KUWAPATIA PENSION JAMII (SOCIAL PENSION) WAZEE WOTE BILA KUJALI MZEE HUYO ALIFANYA KAZI SERIKALINI AU LA,NA HII NI KWA SABABU WOTE WAMECHANGIA KATIKA MAENDELEO YA TAIFA HILI. WEWE UNADHANI HILO NI JAMBO JEMA NA LINASTAHILI KWA WAKATI  HUU AU LA, NINI MCHANGO WAKO ILI KUFANIKISHA KAMPAINI HII.

Zephaniah M. Musendo (TNJ+) (Dar es Salaam)
8 Juni, 2011 12:19 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

@NABROHO SOCIETY FOR THE AGED (MAGU,MWANZA,TANZANIA): 

Wazee ni vijana wa zamani ambao walitumikia taifa hili katika nyanja mbalimbali za uzalishaji mali au katika kutoa huduma kwa jamii. Bila wao taifa hili lisingefika hapa lilipo leo na bila mchango wao tusingeweza kuwa na jeuri tuliyonayo leo au maendeleo tuliyofikia leo. Hivyo basi ni jukumu la vijana wa leo katika taifa hili kulinda mafanikio haya yaliyopatikana kutokana na wazee ambao ni vijana wa zamani. Ni haki kabisa kwamba wazee wanapaswa kulipwa bila kujali kama walikuwa waajiriwa wa serikali ama la. Nchi hii ina idadi ndogo sana ya watu walio katika ajira ya serikali au mashirika ya umma, lakini bado asilimia kubwa zaidi ya wazee wanalitoa mchango mkubwa katika taifa kwa kufanya shughuli zao binafsi, au katika kujiajiri wao wenyewe. Mchango huu usisahauliwe ama kutupwa eti kwa kuwa hawa watu ni wazee sasa. Wananastahili malipo kama shukurani kwa yale waliyoyafanya na ili kuwawezesha kuendelea na maisha yao na shughuli zao kabla Mwenyezi Mungu hajawachukua.

agatha kisaka (Dar es salaam)
8 Juni, 2011 12:30 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

Ni kweli kabisa wazee wa Tanzania ni muhimu wapewe pension kwa sababu zifuatazo:wazee wengi ni maskini na wengi wao wanaishi maisha ya chini ya dola moja na waishi vijijini.Wengi wao wanakufa kwa kukosa matibabu,pia wazee wameachiwa yatima kitu ambacho kinawafanya waishi maisha ya shida hivyo ni muhimu wapewe pension hata kama hawajawahi kufanya kazi.

NABROHO SOCIETY FOR THE AGED (MAGU,MWANZA,TANZANIA)
25 Juni, 2011 14:57 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

JE UNADHANI SERIKALI YA TANZANIA INAWEZA KULIPA WAZEE WOTE PENSION JAMII KILA MWEZI HASA UKIZINGATIA IDADI YAO HAIZIDI HATA %5.7 YA WATU WOTE

NABROHO SOCIETY FOR THE AGED (MAGU,MWANZA,TANZANIA)
25 Juni, 2011 15:03 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

 NI SABABU GANI ZINAZOCHELEWESHA WAZEEE WA TANZANIA KUPATIWA PENSION JAMII NA SERIKALI YETU WAKATI IDADI KUBWA YA WATOA MAAMUZI NI WAZEE WA KESHO NA WANAELEWA FIKA KABISA MAISHA YA WAZEE WENGI NI DUNI MUNO HATA KAMA WALIWAHI KUWA WATUMISHI WA SERIKALI MIAKA YA NYUMA?

NABROHO SOCIETY FOR THE AGED (MAGU,MWANZA,TANZANIA)
25 Juni, 2011 15:10 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

IKITOKEA LEO AU KESHO RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA MRISHO KIKWETE AKATANGAZA KWAMBA SERIKALI YAKE INAANZA KUTOA PENSION JAMII YA TSH 20,000/TU KILA MWEZI KWA WAZEE WOTE HAPA NCHINI JE UMAARUFU WAKE UTASHUKA AU UTAPANDA MARADUFU NA HAKUNA MTU ATAKAYE MSAHAU MAISHANI MWAKE

NABROHO SOCIETY FOR THE AGED (MAGU,MWANZA,TANZANIA)
25 Juni, 2011 15:16 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

UNADHANI SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IKIANZA KUTOA PENSION JAMII KWA WAZEE WOTE HAPA NCHINI KAMA ILIVYO KWA NCHI NYINGINE KAMA BOTSWANA,AFRIKA YA KUSINI,MAULITANIA N.K ITAPOTEZA NINI?

CHUI (Ilemela-Mza)
10 Julai, 2011 20:31 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)
Isiwe mjadara,sana serikali makini uelewa na kusikia vilivyo busara na hata kuvi timiza kwa vitendo.Mimi 2010..nilikwisha anza kampeni wazee walifarijika sana,tuwatume wawakilishi(wabunge)
FRANCIS,TIBENDAKWINGANA (SOKOINE UNIVERSITY, MOROGORO)
18 Februari, 2013 19:47 EAT

WAZEE NI CHUMVI YA TAIFA HILI, KUPEWA HAKI STAHIKI NI WAJIBU WA TAIFA HILI (TANZANIA). MSINGI WA VIJANA WA LEO UNAASHIRIWA NA KAZI ILYOFANYWA NA WAZEE WA SASA.

Hubert (Moshi)
10 Machi, 2013 13:46 EAT

Inawzekana kabisa serikali inatakiwa kuanza utekelezaji wake mapema hata wakianza kwa sh 30000 za kitanzania itapendeza maana nchi yetu sio masikin.


Ongeza Ujumbe Mpya

Karibisha watu kushiriki