UFISADI TANZANIA
BY SIMION SIMBUJILE (MTWARA KUTOKA SHIRIKA COMMUNITY BASIC EDUCATION FOR DEVELOPMENT (COBED))May 31, 2011 at 2:05 PM EAT
Kwa nini Mafisadi hawachukuliwi hatua za haraka ili watanzania wawe na imani na serikali yao sio kama sasa inavyoonekana kama wanafugwa wakati wameihujumu nchi?
BY SIMION SIMBUJILE (MTWARA KUTOKA SHIRIKA COMMUNITY BASIC EDUCATION FOR DEVELOPMENT (COBED))May 31, 2011 at 2:06 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)
@BY SIMION SIMBUJILE (MTWARA KUTOKA SHIRIKA COMMUNITY BASIC EDUCATION FOR DEVELOPMENT (COBED)):
PHAERA (ILALA)June 8, 2011 at 11:58 AM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)
kwa sababu wanaopaswa kuwawajibisha ni mafisadi wenzao.
TUSPO (PUGU ILALA, DAR ES SALAAM)June 8, 2011 at 12:01 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)
Ni kweli kwa sababu mgojwa hawezi kumtibu mgonjwa mwenzake.
Sango Kipozi (Dar es salaam)June 8, 2011 at 12:02 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)
@BY SIMION SIMBUJILE (MTWARA KUTOKA SHIRIKA COMMUNITY BASIC EDUCATION FOR DEVELOPMENT (COBED)): Nakubaliana kabisa na wewe ndugu yangu. Maana mpaka sasa suala la ufisadi limekuwa ni kama hekeya na simulizi, kwa ajili ya kuburudisha uma. Halijachukuliwa kama tatizo linalohitaji kushughulikiwa. Lazima utafutwe ufumbuzi ili kurejesha imani ya raia ambayo kwa sasa imeathirika.
Noel Mwembere (Katibu wa Elders for the prevention of Aids(EPA-UKIMWI) (MASASI, MTWARA)July 26, 2011 at 2:19 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)
Kama mapambano ya rushwa, ufisadi na Ukimwi yangepewa kipaumbele kama vile taifa lilivyopambana na ujinga(miaka ya 60), vita vya kagera (mwishoni mwa miaka ya 70),ulanguzi na uhujumu uchumi(miaka ya 80) naamini kuwa taifa letu lingekuwa mbali sana hivi sasa.