Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations


         ilikuwa ni tarehe 20/12/201, usiku na kuamkia tarehe 21/12/2011 wananchi wa jiji la Dar es salaam walijikuta katika wakati mgumu mara baada ya kukumbwa na mafuriko,ambayo yaliwaacha baadhi ya wakazi wa jiji hili wakiwa hawana makazi ya kuishi huku wengine wapatao 41 wakipoteza maisha.

Kutokana na hali hiyo,serikali,taasisi,mashirika na watu binafsi walijitoa kwa hali na mali kuhakikisha kuwa wahanga wa mafuriko wanasaidiwa,kwa kupatiwa malazi,mavazi na chakula.Maeneo yaliyoathirika zaidi kutokana na mafuriko hayo ni pamoja na kimara,mbezi,tabata,msewe na jangwani.

  Nyumba,miundo mbinu ya barabara na madaraja,viliharibiwa kabisa hali iliyopelekea kukatika kwa mawasiliano kati ya eneo moja na lingine. Kutokana na kuharibiwa kwa miundo mbinu hiyo,baadhi ya maeneo ya  kazi  yalikosa ufanisi,kutokana na ama wafanya kazi kuchelewa kufika kazini au kutofika kabisa.

  Athari ya mafuriko itaendelea kuwa kubwa iwapo hatua za makusudi hazitachuliwa hasa kwa wananchi wanaoishi sehemu za bondeni kwa kuwa idara ya hali  ya hewa nchini imeelezea kuendelea kuwepo kwa mvua kubwa kati ya mwezi Februari na Machi.Baada ya mvua kusimama kwa muda baadhi ya changamoto mbalimbali zimeonekana kujitokeza.Moja ya changamoto hizo ni pamoja na uwezekano wa kuibuka kwa magonjwa ya mlipuko kama vile kuhara,kipindu pindu na magonjwa ya tumbo.

 Hali hii inatokana na uchafu uliokithiri katika maeneo hayo ya bondeni.Baadhi ya maeneo yameonekana kuwa na vinyesi ambavyo vilitapishwa wakati  mvua ilipokuwa inanyesha.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine,wana jukumu la kuhakikisha kuwa elimu ya mazingira inatolewa ili kuepuka madhara ambayo yatatoke baadae,iwapo hatua za makusudi hazitachuliwa kudhitibiti hali hiyo.Daima kinga ni bora kuliko tiba,ni vema utaratibu wa kudhitibi matatizo uzingatiwe kabla ya kutokea kwa tatizo,hali ambayo itasaidia kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Pamoja na serikali kuwataka wananchi wanaoishi sehemu za bondeni kuhama na kutafuta maeneo yaliyosalama kwa maisha na mali zao,bado  uchunguzi unaonesha kuwa itakuwa ni vigumu kwa baadhi yao kuhama kutokana na ukweli kwamba,wananchi wengi hali zao za kimaisha ni duni sana.Mfano mkazi mmoja wa jangwani B amenukuliwa akisema kuwa yuko tayari kufia bondeni na hawezi kuhama kwa kuwa hana uwezo  wa kufanya hivyo.

 wananchi  hao ambao wengi wao huendesha maisha yao kwa kuokota makopo na kuyauza,inaonesha itakuwa ni vigumu kuwaondoa maeneo hayo kwa kuwa hawana njia nyingine mbadala ya kuwafanya wajikimu kimaisha.

Katika kipindi hiki cha mpito,serikali,mashirika na watu binafsi wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa upatikanaji wa huduma za afya unazingatiwa,kwa kutoa dawa za kutibu maji,vyandarua,sabuni pamoja na vyombo vya kupikia pale itakapobidi.

 Daima umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu,hivyo wadau kwa pamoja tuungane ili kuhakikisha kuwa tatizo lililojitokeza linakabiliwa.

 

ANTON MWITA KITERERI.

 

January 8, 2012
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.