Envaya

Ifuatayo ni historia ya asasi iitwayoIpembe orphans children care support (IPEOCCASU) kwa mara ya kwanza kabisa mnamo mwaka wa 2004 wazo la la kuanzishwa lilitolewa na mwl Gabriel T Bee ambaye alikuwa mratibu wa elimu kata ya ipembe wakati huo 

Na baadae Februali 2005 ikaanzishwa rasmi ikiwa na wanachama kumi na mbili wakiwemo 1 Gabriel T Bee mwenyekiti 2 Yesaya Ramadhani katibu 3 Gregori N Manimo Mtunza hazina 4  Mwl Pauli M/Kiti msaidizi 5 Mwl Agnes Nnko Katibu Msaidizi 6 Emmanuel Nono 7 Fatuma B Yusufu 8 Daudi Msonsa 9 Chalz Kilimba 10 Grace Mwaluka 11 Mwl Yesaya Kawiche 12 Mwl Samsoni  13 Lailath Mtafa  

Hawa ndio wadau na waasisi wa organisation hii waasisi hawa kitaaluma ni walimu kama mjuavyo ualimu ni kazi ya wito ikilenga kumwelimisha mtoto kijamii.kimazingira .kiafya na kimwili na kiroho pia .

 Kikundi hiki cha IPEOCCASU Ilipofanya utafiti wa awali juu mambo yanyoshusha taaluma kiligundua kuwa tatizo kubwa lilikuwa ni utoro wa jumla na wa rejareja Mashuleni unaosababishwa na mazingira duni ya watoto hao ambao wengi wao ama ni yatima au kafiwa na mzazi wake moja ambaye anamtegemea.

 pia tukagundua kuwa liko wimbi kubwa la watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi na ndipo tukaanzisha asasi hii yenye  lengo la kuwasaidia  tulitengeneza mfuko wa kuwasaidia ambao kila mwanachama kwa hiari aliuchagia tsh 2000/- kutoka katika mshahara wake wa kila mwezi

 na pia kuwatafutia misaada nje na ndani ya nchi na kwa  kutoa mafunzo kwa jamii ili iweze kujua ni kwa namna gani wataondokana na janga hii la watoto wa mitaani na walio katika mazingira hatarishi pamoja na kundi lile ambalo kwa njia moja au nyingine ama wameathirika au wameathiriwa na VVU