@Timothy W. Philemon (Zanzibar):
Timothy umewaza vizuri saana juu ya kuwa na jengo la mashirika , ila tatizo Tanzania hadi sasa hatuna Mtandao wetu ambao utatuwakilisha ndani na nje ya nchi. kwanini nasema hivi tuliitegemea saana TANGO na NACONGO lakini mabo yapo kimya saana juu ya hili. FSC, UNGO na Mtandao wa Mkoa wa Arusha walianza safari ya kuanzisha mtandao/Apex kwa lengo la kuwa Mtandao wa NGO zote Tanzania hata hivyo shughuli hizo ziliishia na kuzimwa na baadhi ya NGO kuwa na waswasi kuwa watamezwa na mtandao huo na badala yake tukasema kuwa NACONGO iwe ndiyo Apex lakini kasoro yake ni kuwa inaishia ngazi ya mkoa tu na mapendekezo ya NACONGO kuanzia chini yalifanyika lakini hakuna kinachoendelea mpka sasa.Hivyo mimi naamini FCS bado ina nafasi ya kuendeleza Ule mchakato wa APEX ili tupate uwakilishi wa kweli katika ngazi za Kikata, kiwilaya,kimkoa, kitaifa na kiamataifa juu ya mambo yanayohusu maendeleo uwanaharakati Tanzania.