Injira
Handeni Development Group

Handeni Development Group

Handeni, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

 

HANDENI DEVELOPMENT GROUP (HDG)

Ni kikundi kipya kinachoundwa mwaka April 2011 chenye wanachama zaidi ya 30 na wote ni wazawa wa Handeni bila kujali makazi yao yalipo,

Kikundi kinajumuisha wafanyakazi na wafanyabiashara mbalimbali wa Handeni.

Kikundi kitafahamika kisheria na kufuata kanuni zote husika.Pia kitajumuisha jopo la wanachama wenye fani husika katika Uongozi,wafanyabiashara,wanasheria,Saikolojia,Dokta(Mifugo/Binadamu),Ualimu,wanauchumi,wahasibu ambao tutashauriana jinsi yakupiga hatua zaidi kimaendeleo kati yetu kama wakazi wa Handeni.

Kikundi hicho kimeundwa kusaidiana kuongeza mwendokasi wa maendeleo mbalimbali kwa wananchi wa Handeni,haswa wanachama wake kupitia mbinu mbalimbali kama wafanyavyo sehemu nyingine duniani.kama;-

i)                    Kuanzisha HDG SACCOS ili wanachama waweze kuweka na kukopa kwa utaratibu maalum kati ya kikundi,bank au taasisi mbalimbali za kifedha.

ii)                  Ushauri malimbali wa kibiashara,sheria,makazi kupitia vikao maalum na website itakayoanza mapema April 2011 hii.(www.handenidg.org)

iii)                Kuwapatia ajira vijana wa Handeni kupitia miradi ya kikundi hiki kutokana na kiwango cha elimu yake.

iv)                Kumsaidia mwanachama katika dharula kama kilio,ugonjwa kwakutoa na kukusanya michango kwa matibabu au mazishi kwa haraka na ikiwezekana hata kwakumkopesha ili kumuondolea tatizo kwanza.

v)                  Kupeana taarifa mbalimbali za matukio ya Handeni kama sherehe(Harusi),na majanga(vifo) kwa walio nje na ndani ya mji wa Handeni.(Nani.Lini,Wapi,Saa ngapi)

vi)                Kusaidiana kwa mikopo kupitia HDG SACCOS na ushauri katika Mipango binafsi kama ujenzi,biashara,ndoa.

vii)              Kurudisha mshikamano/muungano “network” kwa wakazi wa Handeni waliotawanyika sehemu mbalimbali Tanzania na nje ya nchi.

viii)            Website itakuwa na sehemu yamatangazo kwaajiri yatakayo tangaza nafasi za kazi zinazotokea Handeni na itatoa nafasi yakujitangaza kwa kuweka CV yako na maelezo mafupi.(labour market).

ix)                Kufanya kitu chochote cha maendeleo ya wilaya bila kujari faida ya kikundi kila mwaka.

 

MALENGO YA BAADA YA MWAKA MMOJA WA KIKUNDI.

Kufungua miradi mikubwa yakukuza kipato cha kikundi kama;-

 

            KIUCHUMI,

  • o   Kununua eneo kubwa kwa ufugaji wa kisasa na kufungua “butcher” letu binafsi.
    • §  Kuku wakienyeji na kisasa (Mayai na Nyama)
    • §  Mbuzi na G`ombe (Nyama na Maziwa)
    • §  Mifugo mingine kama Bata, Kanga
  • o   Kufungua miradi mbalimbali katikati ya jamii kutokana na mahitaji.
    • §  Pikipiki na Bajaji nje na ndani ya Handeni
    • §  Stationary na internet ya kisasa
    • §  Salon yakisasa kwa jinsia zote
    • §  Maduka mbalimbali
  • o   Kuanza mkakati wa kuomba mkopo mkubwa kwaajir ya mradi mmoja mkubwa.

 

KIJAMII,

  • o   Kuwa na siku ya mazingira Handeni kwa kugharamia au kufanya usafi wenyewe na viongozi wawilaya.
  • o   Kuwa na timu ya mpira wa miguu na pete.
  • o   Kutafuta mdhamini mkuu wa kikundi ndani au nje ya nchi.
  • o   Kutengeneza vitambulisho na mikataba

 

 

*Agenda za kikao cha kwanza tarehe 24 April 2011;-

ü  Kukubaliana na kuiangalia kiundani mikakati kama ilivyotajwa na kuongeza mawazo

ü  Kugawana majukumu yakuandaa katiba na “business plan”,mipango ya SACCOS na kukiandikisha kikundi na lini tuanze rasmi.

ü  Mheshimiwa nani anafaa kuwa mlezi wa kikundi.

ü  Nani anafaa kuwa mwanachama na hayupo kwenye orodha.

ü  Kiasi gani tuweke kila mwezi kwaajir ya kikundi na SACCOS.

ü  Kushuhurikia permanent Address yetu.(Dirisha,Box,Simu na secretary)

ü  Lini iwe “deadline” na kikundi kitangazwe rasmi.

ü  Kukusanya mawazo na kuyagawa kwa wahusika ili yafannyiwe kazi.

ü  Mengineyo.