MALENGO NA MADHUMUNI
i. Kumwondoa mtoto katika mazingira hatarishi na yaliyokandamizi mbele za jamii inayomuona mtoto kama hana thamani.
ii. Kumjengea uwezo mtoto kielimu,utamaduni na kumpa uwezo mwingine stahiki kama watoto wengine na jamii zinazowazunguka.
iii. Kuwalinda watoto dhidi ya changamoto kama ubaguzi, unyanyasaji na ukatili.
iv. Kuwalinda watoto katika mfumo wa sheria kama shuhuda wa vitendo vya jinai, mirathi n.k.
v. Kuhakikisha watoto wanapata huduma muhimu za elimu katika kuwaanzishia shule, vituo vya afya, michezo na haki za kusikilizwa na matunzo.
vi. Kuwalinda na matatizo yote hasa kwa wale waishio mtaani kwa kuwajengea kituo maalum cha kulelea.
vii. Kuwapa haki stahiki kama watoto wenye wazazi sawa na wengine kwa kuwapa chakula, malazi, mavazi, matibabu, chanjo pamoja na haki ya kucheza na kuburudika.
viii. Kuwajengea uwezo wa kuelewa mila na tamaduni zao katika nyanja zote bila kukiuka misingi na taratibu za nchi.
Latest Updates
HakiMtoto Foundation joined Envaya.
February 28, 2013
Sectors
Location
Bagamoyo, Pwani, Tanzania
See nearby organizations
See nearby organizations