Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

FOUNDATION FOR DEVELOPMENT ORGANIZATION

Wananchi wa vijiji 26 vya Tarafa ya Busega wilaya mpya ya Busega,Mkoa wa Simiyu, wamewezeshwa umuhimu wa kuhudhuria katika mikutano ya hadhara vijijini kwa mradi uliokuwa ukifadhiliwa na The Foundatio for Civil Society

Katika mafunzo haya wananchi waliweza kupata mafunzo juu ya

  • UMUHIMU WA KUHUDHURIA KATIKA MKUTANO WA HADHARA KIJIJINI.

Tanzania ni miongoni mwa nchi duniani zinazoongozwa kidemokrasia kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu inayofuata misingi ya haki za binadamu na utawala bora, katika nchi yetu serikali ilianzisha vijiji vya ujamaa na kujitegemea mwaka 1974, kwamuundo huo wa vijiji, serikali ikashusha madaraka kwa mwananchi wa Tanzania haki na madaraka ya kusimamia masuala yote yanayohusu maendeleo kijijini kwake na kupata taarifa mbalimbali za maendeleo toka ngazi ya kijijini, kata,wilaya na Taifa. Taarifa hizi zimekuwa zikipatina kwa njia redio, magazeti, mbao za matangazo na katika vijiji zinapatikana kupitia mikutano ya hadhara inayostahili kufanyika kila baada ya miezi mitatu, hivyo basi ni wajibu wa kila mtanzania kuhudhuria sehemu hizo za mikutano ya hadhara ili kutoa maoni yake, ushauri, kukubali au kukataa masuala ambayo yanastahili kutekelezwa katika eneo lake. Katika mikutano ya hadhara tunapata pia kupitia na kujadili utekelezaji wa sera za maendeleo zinazotekelezwa na kupima mafanikio yake na pia kuyatolea ushauri ili utekelezaji wake, mfano

  1. Sera ya elimu
  2. Sera ya watoto
  3. Sera ya afya
  4. Sera ya kilimo na sera zingine nyingi.

Katika mikutano hii tunashirikiana wanavijiji wote kutoa maoni yetu na kutafuta majibu juu ya changamoto/kero zinazotuzunguka hapa katika kijiji chetu,kama yapo majibu tunayapata hapahapa kijijini lakini kama hayapo tunawasiliana na viongozi wetu wa ngazi za juu kupata majibu, kubuni mikakati shirikishi ya kuendesha kusimami na hata kutoa maoni, ushauri kwa viongozi wetu tuliowachagua kutuongoza na kusimamia haki zetu.

 Tofauti na hivyo wananchi wengi tumebadilika na badala ya kuhudhuria katika mikutano sasa hatuhudhulii na tunabaki kulalamika, kulalamika huku kunasababisha serikali yetu ya kijiji/vijiji kushindwa kutimiza wajibu wake hata pia kupokea maoni yetu juu ya vipaumbele vya miradi stahili kijijini kwetu.

 Mwezeshaji alitumia maneno mengi kuelezea faida za kuhudhuria katika mikutano ya hadhara mwisho alisema, nawaomba wale wote tuliopo hapa katika mkutano huu na wale wote tuliopokea vipeperushi hili liwe deni malipo yake ni wewe kumshauri mtu ambaye unamfahamu hakuhudhulia mahali hapa kuwa mkutano mwingine utakapoitishwa wahudhurie kwa wingi ili mshirikiane kutetea na kusimamia maendeleo ya kijiji chetu, ukweli usiopingika kuwa wananchi wanayohaki ya kushiriki wao kama wao katika kuamua miradi wanayoiona ni muhimu kutekelezwa hapa kijijini kwa faida ya sasa na kwa vizazi vijavyo, huu umekuwa ni utaratibu unaotumiwa na serikali kabla ya kutengeneza bajet ya serikali kwa ujumla kwa kuzingatia vipaumele vya miradi tuliyoipendekeza hapa kijijini.

  • UMUHIMU WA KUSHIRIKI KATIKA KUIBUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WAKE.

Mwezeshaji aliwaeleza kuwa mradi bora na unaokubalika ni ule unaopitishwa katika mkutano wa hadhara wa kijiji ambao pia wananchi zaidi ya 2/3 wanakuwa wamehudhuria, lakini pia tumezidi kushauriana na viongozi wetu hapa kijijini njia nzuri ya kufanya wananchi wengi tuhudhulie ni serikali ya kijiji yenye wajumbe 25 ikiwa inawakilishwa na wenyeviti wetu wa vitongoji, wanapokutana kwa ajili ya kutoa vipaumbele vya miradi ya maendeleo ni vyema kabla ya kuitisha mkutano huo wa hadhara,yabandikwe katika mbao za matangazo kwa muda wa siku 21 na kwa uchache siku 14 ili sisi wananchi tupate nafasi ya kujadili na kutoa maoni yetu juu ya miradi walioipendekeza ili sisi tuchague mmoja wapo. Inapofika siku ya mkutano huo tunahudhuria kwa wingi huku tukijua tunachokuja kukifanya siku hiyo ya mkutano, inapofika agenda husika mtaalamu wetu hapa kijijini anasimama kwa ajili ya kutueleza faida ya kila mradi hapa kijijini, baadaye tunapewa nafasi nasi kutoa maoni yetu ya mradi tunaopendekeza mawazo yetu yasipotoa mwelekeo tunapewa nafasi ya kuyapigia kura, kura itabaini tunatekeleza mradi upi.

Mradi ulichaguliwa unapangiwa makisio ya mapato na matumizi na utekelezaji wake unakuwa wa muda gani nao uonyeshe serikali itachangia kiasi gani na wananchi watachangia kiasi kipi, na mradi huo uonyeshe kuwa umegawanywa katika vipindi 4 vya miezi 3 kama utatekelezwa kwa mwaka mmoja, katika kila kipindi ionekane thamani itakayotosha sehemu ile, mf. Ujenzi wa nyuma unaweza kugawa katika vipindi 4, kipande cha

  1. Msingi = inaweza kutathiminiwa msingi ule utagharimu kiasi cha Tshs 500,000/=
  2. Boma =inaweza kutathiminiwa utagharimu kiasi cha Tshs 500,000/=
  3. Kupaua=inaweza kutathiminiwa Tshs700000/=
  4. Finishing ( umaliziaji)= inaweza kutathiminiwa kugharimu 1Tshs 1,000,000/=

Kugawa huku kunamuwezesha mwananchi kujipangia pia namna ya kutoa michango yake ili kuepusha mradi kukwama kufikia lengo lake lililotarajiwa, kila hatua inamaliza muda wake sharti kutoa taarifa ya utekelezaji wake kuonyesha kiwango kilichofikiwa na mapungufu/mafanikio yaliyofikiwa/jitokeza.

Inaweza kuteuliwa kamati ya usimamizi wa mradi toka miongoni mwa wananchi kusaidiana na viongozi wa kijiji katika kusimamia mradi husika ili kuepusha kuamini hesabu halisi.

Na wananchi wanayohaki ya kusimamia kwa pamoja kuhakikisha kuwa ujenzi unaoendele unatimiza viwango vinavyokubalika

  • HAKI YA KUDAI KUSOMWA KWA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI KILA BAADA YA MIEZI 3

Mwezeshaji alisema katika kusimamia mradi husika na kila hatua tunayovuka uongozi unapotoa taarifa ya mradi husika pia siku hiyo tunasomewa na taarifa za mapato na matumizi ambazo kama tulivyosema mwanzo kuwa mradi wetu tunaugawa katika vipindi vya miezi 3 na taarifa hizo pia zipatikane kila baada ya miezi mitatu, ieleweke wazi siku ya kupokea taarifa hizo vyema tutaarifiwe kwa muda wa siku 21 na kwa uchache siku 14 na hata agenda zisizidi 5 nazo ni

  1. Kufungua mkutano.
  2. Kusoma muhtasali wa kikao kilichopita.
  3. Yatokanayo na muhtasali huo.
  4. Kusoma taarifa na kuupitia taarifa ya mradi.
  5. Kufunga mkutano.

Baada ya taarifa hiyo kusomwa ni vyema pia kubandikwa kwenye mbao za matangazo ili wananchi wengine kwa sababu zisizoweza kuzuilika hawakuweza kuhudhuria waweze pia kuzisoma, ili kipindi kijacho wawe na kumbukumbu zake. 

Theresi Ndaki wa kijiji cha  Mwanangi aliwaasa wananchi wa kijiji hicho kwa kusema nimemuele wa hivi mwezeshaji sisi wanankijiji tunayosababu sasa ya kushirikiana kutatua matatizo yetu hapa kijijini badala ya kuendelea kulalamika changamoto zetu hapa kijijini tunapaswa kuzichulia hatua, kwanza tuchukue jukumu la kuhamasishana, tukuhudhuria hapa mkutanoni tunaanza kujadili matatizo yetu yapi tuyatafutie ufumbuzi mf. kama tatizo letu ni maji tuitane kwenye mkutano tushirikiane wote kutoa maoni yetu tutafyte njia ili maji yaenee kote, kama ni zile ahadi tuzifanyie kazi tuwafate ,kama ni mitalo tuchimbe wenyewe kama alivyosema mwezeshaji tulilalamike tuchukue hatua kuyashughulikia matatizo yetu serikali ikiona itatuunga mkono kwa hatua yetu hiyo na wakati ni sasa.

Kama tatizo ni watoto wetu ambao tumewapendekeza kwa matatizo yao ili serikali iwasomeshe bure kama wanasumbuliwa kufukuzwa shuleni tukutane na uongozi wetu wa bodi ya shule na Mhe, Diwani ni mjumbe tumwambie tuchukue hatua tusilale. Niombe uongozi wetu itisheni mkutano haraka baada ya leo ili tuanze michakato ya kushiriki ipasavyo katika maendeleo.

Mgatu Charles Naomba aliwaomba viongozi wa shirika la FODEO hili waanze kuoa elimu hii kuanzia ngazi za vitongoji ili wananchi wengi sasa wapate elimu hii muhimu wa kuhudhuria katika mikutano ya hadhara vijijini huku akikiri kuwa hilo ni tatizo ambalo limekuwa likikwamisha maendeleo vijijini na kuongeza umaskini.

Mr Mathias Kabadi aliwashukuru mwezeshaji wetu juu ya elimu hii muhimu. huku akiwataka wananchi wenzie kujumuika pamoja katika mikutano alianza kwa kusema.  Ndugu zangu wanakijiji (ka tumishaghi) lugha ya kisukuma yenye maana tuamuke sasa tuwe kama zamani mbona tulishirikiana leo hii mbona tunashindwa FODEO wametusaidia tumetambua jambo muhimu kweli ,tuondoe sasa matabaka kama kuna makosa tusameheane tuanze upya kusaidiana kushauriana, FODEO wameliona hili nasasa wanatushirikisha na sisi tuungane tujitete tutumane hata kama ni kwa waziri twende tukiona wenyewe sasa tumefika mwisho na tumekwama.

 

November 7, 2012
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.