Envaya
Parts of this page have been translated from Swahili, but the English version is out of date. View original · Edit translations

Foundation for development organization.(FODEO) ni shirika lisilokuwa la kiserikali na lisilozalisha faida lililoanzishwa mwaka 2004 kama CBO iliyokuwa ikifanya kazi zake katika kata ya Mwamanyili, shirika lilipata usajili wa ngazi ya NGO mwaka 2009 chini ya sheria ya usajili wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kifungu cha 12(2) of Act No 24 of 2002.na kupewa cheti chenye N0.00003431.

Nia ya kuanzishwa kwa shirika hili kusaidia kutoa utetezi wa changamoto za maendeleo kwa jamii zilizochini kabisa ,mfano jamii za vijijini, ili kuleta unafuu katika maisha na changamoto zinazokabili maendeleo yao na mbinu za kukabiliana nazo, FODEO imekuwa ikihamasisha na kuunganisha jamii mbalimbali vijijini katika kujiunga katika vikundi vidogo vidogo na shirika kusaidia kutoa mafunzo na mbinu za kusimamia vikundi vyao ili kuwa imara vinavyotambua umuhimu na wajibu wao katika kusimamia maendeleo.

Katika kuhakikisha nia hii inafikiwa FODEO imekuwa ikizunguka katika vijiji mbalimbali katika wilaya na kusimamia uanzishaji wa vikundi vya akina mama wajane, wazee wanaoishi na watoto walio katika mazingira hatarishi, vijana wanaomaliza elimu za msingi na  sekondari na kushindwa kuendelea na masomo ya juu, wote hawa wanashauriwa umuhimu wa kujiingiza katika vikundi na kuanzisha miradi midogo midogo ya maendeleo katika maeneo yao.

FODEO inaendelea hadi hivi sasa na hatua zake za maendeleo katika kuhakikisha wananchi vijijini na viongozi wao wanashirikiana katika kusimamia miradi ya maendeleo vijijini na viongozi wa vijiji kuzingatia misingi ya utawala bora na haki za binadamu katika kauri mbiu  (WAJIBIKA KWA NAFASI YAKO ILI KUCHOCHEA MAENDELEO) mradi huu ulitokana na migogoro mingi baina ya wanavijiji na viongozi wao, viongozi  wa vijiji kaatika eneo la Magu wamekuwa wakiwamulia wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo bila kupokea maoni yao ya vipaumbele vipi vya maendeleo na viongozi kutokusoma taarifa za mapato na matumizi baada au kabla ya kukamilika kwa miradi husika kijijini kwa wakati kama inavyoamuliwa na serikali, serikali katika sera yake ni kusomwa kwa taarifa hizo kila baada ya miezi mitatu.