Envaya

UTAWALA BORA KATIKA TANZANIA

Mzeituni Foundation (Mwanza region,Ukerewe district)
8 Ugushyingo, 2013 at 08:34 EAT

Ukweli tumefurahishwa kwa kiasi kikubwa na HOTUBA ya mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg.Dr.J.M.Kikwete jana akiwa Ukumbi wa BUNGE mjini DODOMA.Ni hotuba iliyojibu hoja nyingi zilizokosa majibu na zilizoleta sintofahamu miongoni mwa watanzania hasa tuliozoea umoja na ushirikiano tukiwa na sifa ya pekee ya ukarimu hasa pale tulipogubikwa na hali ya kutengwa katika jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Mheshimiwa Rais pamoja na mabo mengine aliweza kulizungumzia suala hili kwa mapana yake kiasi kwamba tumejisikia AMANI hasa ukizingatia kwamba Tanzania ni nchi iliyopigana zaidi kuhakikisha kwamba nchi nyingine jirani na Tanzania zinapata Uhuru japo sisi tulishapata Uhuru mapema.

Tuzidi kuomba kwa ajili ya shirikisho salama na lenye tija kama tunavyo amini.

MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU UBARIKI UMOJA WA AFRIKA YA MASHARIKI.

Chrispine F.Mabwenga (Mwanza Tanzania)
8 Ugushyingo, 2013 at 17:53 EAT

Hi! Mzeituni kwanza hongereni kwa kazi nzuri mnayoendelea kufanya katika harakati za kuiletea Tanzania maendeleo kama wadau muhimu kutoka ASASI ZA KIRAIA.

Namimi nampongeza Rais kwa hatua hiyo nzuri kwani ametoa mwongozo na nafasi ya Tanzania kama nchi dhidi ya yale yote yaliyokwisha semwa na hata wngine wasio na nia njema na shirikisho letu lakini kwa hili atakuwa amewajibu na wamekipata.

Kuna umuhimu mkubwa wa mashirikiyo na kuwa katika jumuiya kama hii ya kwetu,inao umuhimu mkubwa sana hasa katika mambo ya kiuchumi,kisiasa n.k

Tunategemeana sana hasa nguvu ya pamoja kukabiliana na wimbi la ugaidi duniani,hatutashinda vita hii kwa migawanyiko.

Nampongeza sana mheshimiwa Rais.


Andika ubutumwa

Tumira abandi mu kiganiro