Envaya

TUSEME KUHUSU KATIBA MPYA

Mzeituni Foundation
13 Juni, 2013 17:59 EAT

Mzeituni Foundation,tunatambua umhimu wa katiba mpya yenye kujibu mambo ya msingi yanayojibu kero za wananchi na kugusa maisha yao ya kila siku moja kwa moja,ili mwisho wa siku tuwe na Tanzania tunayoihitaji,Tanzania yenye Amani inayonufaika na uwepo wa rasilimali zake.

Tumefurahi pia kwa rasimu ya katiba ambayo walau imejaribu kugusa na kuyasemea mambo mhimu ambayo kwa muda mrefu watanzania wamekuwa wakiyapigia kelele.

Ni wito wet kuwa kila mmoja wetu ashiriki kwa namna ya pekee na kwa masilahi ya nchi na Taifa kwa ujumla

Wanasheria na wataalamu wa mambo ya katiba pia wachukue fursa ya kutosha kupitia rasimu hii ya kwanza na kutoa inputs zao hasa kwa wananchi wa kawaida ili waelewe ni kipi kinaendelea na wakati ufikapo wa kupiga kura ya maoni basi wawe tayali kuikubali au kuikataa kwa sababu za msingi.

Tukikosea kutumia nafasi yetu hii vizuri kupata katiba nzuri yenye manufaa kwa mtanzania itatugharimu miongo kadhaa.Kwa hiyo "Chondechonde" watanzania katiba ndiyo sheria mama za nchi,tusipuuze kuendelea kutoa maoni yetu huku tukiweka uzalendo wetu mbele badala ya itikadi za kisiasa/dini/rangi/kabila au kipato.

Prisca edward sanga (Iringa)
12 Julai, 2013 01:09 EAT
Maoni yangu ni kuhusu suala la uraia wa nchi zaid ya moja,likubalike kikatiba,hii itasaidia kutunza asili zetu na uzalendo,pia itasaidia kuleta maendeleo,,kwa mfano kuna watu wana profesions zao za maana tu wakapata bahat za kufanya kaz nje ya nchi,hawa wakienda kule wanachukua uraia huko,na kwasabab nchi yetu haina suala la uraia wa nchi zaid ya moja hawa wanakua sio wa kwetu tena,ama wanakua kama wagen tu ambapo hawawez kuisaidia nchi kama wenye nchi yao so hawapo huru kuisaidia nchi kivyovyote wawapo nje wala ndani....pia ktk suala la michezo itasaidia haswa pale inapotokea kua tuna watu wanavipaja vyao wapo nje uraia huku tushawanyima kisa wana uraia mwingne,,,,wakat wangeruusiwa anacheza uko nje anapohtajka kimashindano ya nchi vile anakuja anachezea nchi yake then anarud kwe timu ya nchi alonunua uraia......kama tunawaswas tutajfunza wenzetu wanawezaje pia tutaweka sheria ztakazosaidia kuendesha hili......tutaweza tu kwa manufaa ya nch et......MUNGU IBARIKI TANZANIA
Mzeituni Foundation (via email)
12 Julai, 2013 12:43 EAT
Hi!
Akasante kwa Comments zako.
Regards,
Chrispine.

Ongeza Ujumbe Mpya

Karibisha watu kushiriki