Log in
Foundation for Civil Society

Foundation for Civil Society

Dar es Salaam, Tanzania

Respondent: Morogoro Development Organization (MODEO)
Time Submitted: March 31, 2011 at 11:36 AM EAT

Introduction

Morogoro Development Organization (MODEO)
MODEO
Kuelimisha jamii ya watu wenye ulemavu juu ya sera ya watu wenye ulemavu,malengo na utekelezaji wake
FCS/RSG/2/10/099
Dates: 15 Jan-30 Mach,2011Quarter(s): Robo ya Kwanza
TIMOTH Y ACHIMPOTA

Project Description

Policy Engagement
Mradi unakidhi malengo kwani watu wengi wa jamii ya walemavu hasa walioko vijijini haiwaitambui sera ya walemavu wala haki zao za msingi wanazostahiki kupata.,ikiwemo haki za kupata elimu,fursa za kiuchumi, fursa za huduma rafiki za miundo mbinu ya shule,hospitali na ofisi za umma kwa ujumla hazitoi fursa sawa kwa watu wenye ulemavu. Lakini pia kwa kukosa uwelewa juu ya sera ya watu wenye ulemavu na haki zao imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya jamii ya watu wenye ulemavu kiuchumi,kisiasa,kitamaduni na kukosa fursa za kushiriki na kushirikishwa katika vyombo vya maamuzi. Hivyo basi Mradi kwa dhati kabisa unakidhi malengo tuliyo yachagua.
RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
MorogoroKilosaDumila-Mkundi,Dumila,Kumbe,Magole state35
MagoleMagole A,Mandela,35
Msowero-Mvumi,Mwambega,35
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female5592
Male80124
Total135216

Project Outputs and Activities

1.1.Walemavu wameanza kunufaika na fursa mbali mbali za kijamii zilizopo katika maeneo yao ifikapo june,2011
1.2 Jamii ya watu wenye ulemavu wameanza kushirikiana katika kupanga,kutekeleza na kufuatilia miradi ya maendeleo katika jamii ifikapo,2011
1.3 Kero na sauti za watu wenye ulemavu zimesikilizwa na kupatiwa ufumbuzi katika vyombo vya kutunga sheria na maamuzi1.1.1.UTAMBUZI WA KUMBI NA MAENEO YA MKUTANO
1.1.2 MAANDALIZI YA KUTAYARISHA MADA ZA KUFUNDISHIA NA STATIONARI
1.2.3 KUTOA MAFUNZO JUU YA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU
1.2.1KUCHAPISHA MACHAPISHO NA KUYASAMBAZA KWA JAMII YA WATU WENYE ULEMAVU YANAYOONYESHA HAKI ZAO
1.1.2
KUHAMASISHA JAMII YA WATU WENYE ULEMAVU KUWA NA FURSA ZA KIUCHUMI (MIRADI)
1.3.1 KUENDESHA TATHIMINI YA MRADI
1.3.2 KUPANGA MIPANGO YA MAENDELEO INAYO HUSU JAMII YA WATU WENYE ULEMAVU.
MFANO ELIMU AFYA NA VYOMBO VYA MAAMUZI.
1.Tarehe 17/01/2011 Kufanyika kwa kazi ya utambuzi wa maeneo ya kuendeshea semina katika kata zote tatu za Dumila, Magole na Msowelo
2.Tarehe 18/01- hadi Tarehe 19/01/2011 kazi ya kutayarisha mada za kufundishia na vitini kwa ajili ya washiriki wa mafunzo
3.1 Tarehe 24/01 hadi Tarehe 26/01/2011 Kufanyika kwa semina ya kwanza juu ya haki za watu wenye ulemavu katika kata 2 za Dumila na Magole. Semina iliyoendeshwa kwa muda wa siku tatu.Chini ya wawezeshaji 2 ; (Evena Massae na Nd, Joram Peter Mhanyo). Washiriki waligawanywa katika Makundi 2. Kundi la kwanza ni washiriki kutoka kata ya Dumila (35) kati ya hao wanaume walikuwa 20 na wanawake 15,Kundi la pili washiriki kutoka kata ya Magole (35) kati ya hao wanaume 18 na wanawake walikuwa 17. Jumla ya washiriki wote walikuwa 70.

3.2 Mafunzo yalifunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Kijiji cha Dumila ND.DAGILAS MGUMIA na kufungwa na ND.ADAM MBONYE katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kilosa, ambaye ameweza kutupa risala yake kama shukurani zake kwa ufadhili huu wa mafunzo kutoka the Foundation.

3.3 Vijiji vilivyotoa washiriki ni kama ifuatavyo:-
Kata ya Dumila –vijiji vya Mafuru,Magole state na Dumila.
Kata ya Magole ni vijiji vya Mirama na Magole

3.4 Washiriki waliweza utoa ushuhuda mkubwa kwamba hawajawahi kupata mafunzo mazuri nay a aina yake kama haya na hii ni mara yao ya kwanza na walipenda yaendelee kutolewa ili kufikia watu wengi zaidi tuliopo vijijini. Na walitoa shukrani zao kubwa kwa ufadhili wa shirika la the Foundation.

3.5Tarehe 27/01 hadi Tarehe 29/01/2011 kuendesha mafunzo ya siku tatu katika kata ya Msowero,Jumla ya washiriki 35 walishiriki mafunzo ambao walitoka katika vijiji vya Mvumi,Mwambega na Msowero, wanaume walikuwa 16 na wanawake walikuwa 19.
4.Hatukuweza kuchapisha machapisho kwani budget ya mradi ilikuwa ni finyu na haikutosheleza kufanya kazi hii,isipokuwa tulicho fanya tulibahatika kaputa vipeperushi kutoka kwa mwanachama mwenzetu alivyo vipata SHIVIWATA –Morogoro na HUMAN RIGHTS CENTRE FOR DISABILITY-Dar es salaam. Zaidi ya vipeperushi 346 tuliweza kuvigawa kwa wana semina na baadhi kuvisambaza vijijini
5-Waliopata mafunzo kupitia ofisi za serikali za vijiji na vitongoji tayari wame kwisha unda kamati za watu wanne(4) wanne katika kila kijiji kwa ajili ya kufanya kazi ya kahamasisha jamii kwa kupita nyumba hadi nyumba na magulio. Kazi hii tayari imekwisha anza kutekelezwa kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji na vitongoji
6.-Tarehe 09/01/2011
MODEO ilifanya kazi ya kufuatilia kuona kama kamati za kuelimisha zimekwisha undwa ,kama ilivyo azimiwa katika mafunzo. Hadi sasa jumla ya kamati 8 zimekwisha undwa kila moja yenye jumla ya wajumbe wasio pungua wanne (4). Kamati hizi zimeundwa miongoni mwa washiriki waliopata mafunzo zimeanza kutembelea ofisi za serikali za vijiji na vitongoji, ofisi ya mbunge na kupatiwa idadi halisi ya watu wa jamii yenye ulemavu na kupita majumbani kuelimisha jamii juu ya haki za watu wenye ulemavu.pia kamati hizi zina endelea kusambaza
vipeperushi mbali mbali vyenye ujumbe wa haki za watu wenye ulemavu.
7.Katika vikao vya majadiliano vinavyo fanyika kati ya kamati zinazo elimisha ,wananchi na wadau mbali mbali kumekuwepo na mapendekezo yanayo tolewa na wadau kwamba ;
• Halmashauri ya wilaya Kilosa itenge fungu maalum kwa kusaidia watu wenye ulemavu km. mikopo ya kuanzisha biashara ili kujitegemea.
• Halmashauri kupitia idara ya mipango na uchumi itenge fursa za kiuchumi kwa watu wenye ulemavu Mfano. Kuwalipia ada katika shule zote za sekondari za kata na vyuo vya ufundi vya VETA.
• Kutoa fursa sawa kwa jamii ya watu wenye ulemavu,kushiriki na kushirikishwa katika mipango ya maendeleo ya Halmashauri
• Kupewa nafasi sawa katika vyombo vya maamuzi.
• Kupatiwa matibabu bure na elimu bora inayo stahiki
• Kusaidiwa vyombo vya usafiri Kama vile baiskeli, stratchers n.k.
-Kumbi zilianishwa kama ilivyo pangwa na hapa kuwa na tofauti yoyote
-Mada 6 na manual 135 kwa washiriki zilitayarishwa
-Hakuna tofauti yoyote iliyotokea isipokuwa tu mafunzo yalichelewa kuanza ,badala ya kuanza saa 2.00 kamili asubuhi kama barua za mialiko zinavyoonyesha yalianza saa 3.00 kamili asubuhi, Sababu kubwa ni kwamba washiriki walikuwa wana tafuta Hela za Kiingilio katika semina wakidhani kwamba ili waweze kuingia katika semina lazima walipie ada, kwa uzoefu kwamba siku za nyuma walipokuwa wanaitwa kuja kwenye mafunzo ama semina na ,mashirika au taasisi zingine wamekuwa wakilazimishwa kuchangia ghara za Mafunzo kwa kutozwa pesa.
-Mada zilizo wasilishwa ni pamoja na:

Sera ya watu wenye ulemavu
Mipango ya maendeleo kwa watu wenye ulemavu
Mkataba wa haki za watu wenye ulemavu
Fursa za kiuchumi kwa watu wenye ulemavu
Vikwazo vya maendeleo na kero kubwa kwa watu wenye ulemavu
-Rasilimali fedha zilizo tumika ni kiasi cha sh. 200,000/= kwa ajili ya usafiri kwa watendaji wa mradi na posho ya Chakula,
--Rasilimali fedha zilizotumika ni Sh.8,100/=
--Rasilimali zilizotumika ni kiasi cha Sh. 4,255,500/= kwa ajili ya chakula,vifaa vya kufundishia,posho kwa wawezeshaji,nauli ya usafiri kwa washiriki kutoka vijijini kuja makao makuu ya kata kwenye mafunzo


Project Outcomes and Impact

1.Walemavu wamemaliza kunufaika na fursa mbali mbali za kijamii zilizipo katika maeneo yao ifikapo june,2011
2.Jamii ya watu wenye ulemavu wameanza kushirikiana katika kupanga kutekeleza na kufuatilia miradi ya maendeleo katika jamii ifikapo, june 2011
3. Kero na sauti za watu wenye ulemavu zimesikilizwa na kupatiwa ufumbuzi katika vyombo vya kutunga sheria,maamuzi
1.Ingawaje ni mapema ,Zipo ishara za kupata mafanikio makubwa kwani tatizo kubwa ilikuwa ni uwelewa mdogo kwa wananchi,viongozi na watendaji wa serikali juu ya haki na fursa za kiuchumi kwa watu wa jamii yenye ulemavu. Baada ya Mafunzo kutolewa na MODEO,zipo ahadi nyingi juu ya kutoa fursa sawa kwa watu wenye ulemavu,ikiwemo kuwapatia mikopo ,kuwalipia ada katika shule za sekondari na vyuo vya ufundi –VETA kuendeshea biashara zao. Kupitia Halmashauri ya wilaya Kilosa mfuko wa kusaidia wasio jiweza

1.1 Halmashauri ya wilaya kilosa imeahidi kusaidia mikopo kwa vikundi vyote vya wajasiriamali ya jamii ya watu wenye ulemavu.
2.-Hadi sasa zaidi ya miradi mipya 4 ya jamii ya watu wenye ulemavu imekwisha ibuliwa: a) Mradi wa ufugaji wa mbuzi na kuku katika kata ya Msowelo, Mashamba darasa ya kilimo cha matunda na mboga mboga chini ya dhana ya kutekeleza kilimo kwanza katika kata ya Magole tayari vimeanzishwa.

2.1 Zaidi ya walemavu 6 wamekwisha ibuliwa kutoka majumbani ,ambapo walikuwa wamefichwa kutokana na hali zao za ulemavu,hali iliyo changiwa na mila potofu
3.Idadi ya kero za watu wenye ulemavu zinaendelea kushughulikiwa moja ikiwa ni ahadi zilizo tolewa na MH.Mbunge wa Jimbo la Kilosa kupitia katibu wake Nd.ADAM MBONYE, ame ahidi kusaidia vikundi vyote vya jamii ya watu wenye ulemavu kupitia fedha za mfuko wa Jimbo CDF.
3.1 Serikali za vijiji na vitongoji zimeahidi kutoa kipao mbele kwa jamii ya watu wenye ulemavu.Sasa hivi kila kamati katika muundo wa kamati za vijiji na vitongoji walau mjumbe mmoja sharti awe ni mlemavu
3.2 Upo muhutasari wa kero wa jamii za watu wenye ulemavu uliowasilishwa kwa viongozi wa serikali za vijiji,vitongoji,Diwani na kwa MH.Mbunge wa jimbo la Kilosa.


1.Kamati 8 zenye jumla ya watu 32 zimekwisha undwa kwa ajili ya kusaidia kuelimisha jamii juu ya haki za watu wenye ulemavu.
1.1 Mbunge wa Jimbo la Kilosa ameonyesha nia ya kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu kupitia mfuko wa CDF

2.Hakuna mabadiliko mengine kwa sasa
3Bado ni mapema mno kwa kero zote kushufghulikiwa kwa wakati mmoja,isipo kuwa zipo dalili nzuri za kero zote kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.


1.Hakuna tofauti isipokuwa bado ni mapema mno ni matarajio makubwa mradi kutoa matunda makubwa kutokana na mapokeo ya mradi kwa wananchi
2.Hakuna tofauti
Hakuna tofauti
3.Hakuna tofauti

Lessons Learned

Explanation
Uzoefu wa kwanza ni kwamba watu wengi wa jamii ya watu wenye ulemavu hususani waishio vijijini hawajui haki zao za msingi na hivyo kupelekea kukosa fursa nying za kiuchumi,kisiasa na kitamaduni
Hakuna mipango mathubuti ya serikali ya kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu ,na hata muundo wa sera ya watu wenye ulemavu haukuwa shirikishi. Sera yenye haitambuliki kwa walemavu., na baada ya sera kuundwa bado serikali haijatunga sheria juu ya utekelezaji wa sera husika
Tume jifunza kwamba walemavu wengi hawapati fursa za kiuchumi kutokana na wao wenyewe kuwa na elimu duni juu ya haki zao nyingi za msingi.Hawapati elimu ya kutosha,Hawawezeshwi na mafunzo mengi yamekuwa yakitolewa kwa jamii isiyo kuwa yenye ulemavu na walemavu kubakia kutengwa kama omba omba. Ipo haja ya serikali na wadau wengine mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali kutenga na kupanga mkakati wa mipango yao kwa kuzingatia fursa na nafasi ya jamii ya watu wenye ulemavu kimaendeleo.
Mafunzo kama haya yanahitajika sana kwa jamii ya watu wenye ulemavu,hivyo basi ipo haja yaendelee kutolewa maeneo mengi kwani yana nufaisha haja na matakwa ya watu wa jamii yenye ulemavu

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Jamii nyingi ya watu wenye ulemavu walipenda kushiriki mafunzo haya,na walipeleka maombi yao ya kushiriki kupitia viongozi wao wa serukali za vijiji na vitongoji ,baada ya MODEO kuombwa kuwapokea ili washiriki mafunzo tuliweza kukataa kutokana na idadi ya washiriki kuwa imekamilikiTuliwashauri viongozi wa vijiji na vitongoji kwamba wana weza kuwaeleza wananchi wao kusubiri awamu nyingine kama tutapata ufadhili
Washiriki waliweza kutoa malalamiko yao kwamba hii ni maajabu makubwa kupata sema kama hii na kuwezeshwa nauli ya kuwarudisha watokako majumbani,wakati semina zingine walizokuwa wakipata wamekuwa wakichangishwa pesa kugharamia mafunzo.MODEO tuliwaeleza na kuwaelimisha kwamba sisi hatutozi pesa wala ada yoyote na endapo mfadhili wetu akitambua hili mara moja tunafutiwa ufadhili,kwa hiyo ni kosa kumchaji mwananchi ada ya aina yoyote. Baada ya maelezo haya walifurahi sana na kutupa ushirikiano mkubwa.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
SHIVIWATA-MorogoroTulipata vipeperushi
Halmashauri ya wilaya KilosaWawezeshaji
Viongozi wa vijiji na Vitongoji Utambuzi wa washiriki wa mafunzo
Wenyeviti wa vijijijKufungua mafunzo
Mbunge wa Kilosa Kunga mafunzo

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Kuendelea kutoa elimu juu ya sera na haki za watu wa jamii yenye ulemavu katika kata sita nyingine za wilaya ya Kilosa ,ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidiJuni,2011Julai,2011Agosti,2011

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale23
Male49
Total612
People living with HIV/AIDSFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ElderlyFemale915
Male1326
Total2241
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ChildrenFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
DisabledFemale5592
Male80124
Total135216
YouthFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OtherFemale1847
Male3655
Total54102
(No Response)

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Mafunzo ya usimamizi wa ruzuku-Namna ya usimamizi wa mradi
-Utunzaji wa mahesabu na kumbu kumbu
-Uandishi wa taarifa ya utekelezaji mradi
-Tume andaa vitabu kwa ajili ya utunzaji wa mahesabu na kumbu kumbu
-Utayarishaji wa voucher za malipo kwa jina la Asasi

Attachments

(No Response)
« Previous responseNext response »

« Back to report