Envaya

Envaya

Wahusika Wakuu

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa kwa kujiendesha kupitia Google Translate. Ona asili · Hariri tafsiri

Joshua Stern Mkurugenzi Mtendaji

Joshua Stern Baada ya kupata shahada yake ya sayansi ya kompyuta kutoka chuo cha Stanford, Joshua Stern alienda kujitolea Peace Corps Tanzania ambapo alifanya kazi ya kujenga miundombinu ya kompyuta na kutoa elimu ya msingi ya teknolojia ya habari na mawasiliano yaani ICT. Joshua alianzisha shirika hili mwaka 2010 kwa lengo la kujenga jukwaa ya programu inayowezesha uhusiano kati ya wanaharakati wa ngazi ya chini na wakubwa kwenye sekta ya maendeleo. Programu ya Envaya imekuwa ni daraja kuu katika Afrika mashariki linalounganisha mashirika ya kiraia. Wadhamini wa Envaya ni pamoja na Google, Twaweza,Digital Opportunity Trust, Peace Corps, na Trust and Conservation Innovation. Joshua na Envaya wanatumika kama washauri kwa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania kwenye Incubator ya ujasiriamali. Joshua anaongea kiswahili, na ana mahusiano mengi na vyombo vya habari, mashirika ya maendeleo, na ya kiserikali katika Afrika Mashariki.

Jesse Young Afisa Mkuu wa Teknolojia 

Jesse YoungTimu ya Programu ya Envaya inaongozwa na Jesse Young, ambaye ni mwanzilishi mwenza wa Envaya. Jesse ni mhandisi wa programu ambaye hapo awali alikuwa mhandisi mkuu na mwanzilishi wa mtandao unaoitwa startup Apture, iliyonunuliwa na Google Mwaka 2009. Jesse alitambuliwa na Inc Magazine kama mmoja wa vijana wajasiriamali 30 wenye mafanikio na wenyeumri chini ya miaka 30. Jesse ana shahada ya uzamili katika Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Stanford, ambapo alijenga timu ya walimu wasaidizi kwa ajili ya kozi ya programu.

Radhina Kipozi  Meneja mradi wa Afrika Mashariki

Radhina Kipozi Radhina Kipozi ni mmojawapo wa wajasiriamali wadogo kwenye mambo ya kijamii katika ukanda wa Afrika Mashariki. Radhina alianza kujishughurisha na vyombo vya habari kama mwimbaji maarufu, kwa sasa anafanya kazi kama mwandishi wa habari za uchunguzi, na anasaidia kushauri mashirika ya kiraia ya kimaendeleo Tanzania mfano Jean Media . Kama mmoja wa waanzilishi wa Envaya na Meneja wa Programu hii katika ukanda wa Afrika Mashariki,anasimamia shughuri zote za uendeshaji wa Envaya kikanda, pia anaendesha ofisi ya makao makuu ya Envaya jijini Dar es Salaam. Hutoa mafunzo na msaada kwa ajili ya watumiaji wa Envaya, na bila kuchoka kuitangaza Envaya katika Afrika. Radhina anaongea Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha, pia anaongea lugha ya  kijapani.

Anthony Walton Mkurugenzi wa Vyombo vya Habari na Mawasiliano 

Anthony Walton ameandika mambo mengi kuhusu masuala ya haki za kijamii katika  machapisho kuanzia New York Times mpaka Harpers na The Oxford American. Repoti yake ya mwaka 1999 kwenye gazeti ya Atlantic Monthly inayoitwa"Teknolojia dhidi ya Wamarekani Wa Afrika" ilikuwa moja ya kazi iliyotambua umuhimu wa kuziba pengo la maendeleo ya dijitali nchini Marekani na dunia nzima. Pamoja na uzoefu mkubwa katika uandishi wa habari, filamu, anafanya kazi ya kusaidia Envaya kueleza malengo yake na madhumuni kwa lengo la kupanua kazi hizi ili ziwafikie wale ambao wanaweza kunufaika na kazi ya Envaya. Pia anafundisha chuo kinachoitwa Bowdoin College.

Lilian Matari Meneja Mwenza wa Programu Afrika Mashariki

Asia R. Kilambwanda Lilian Matari ni mkereketwa mkubwa sana kuhusu mabadiliko ya kijamii na maendeleo ya bara la Afrika. Kama Meneja mwenza wa programu hii ya Envaya kwa ukanda wa Afrika ya Mashariki, husaidia kuratibu mipango na shughuri mbalimbali za Envaya ili kuhakikisha teknolojia na huduma za Envaya zinaboreshwa kulingana na mahitaji ya watumiaji.Alipata shahada yake ya kwanza ya Uhusiano wa Kimataifa na Mafunzo ya Maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Sussex, pia amewahi kufanya kazi na UNESCO Tume ya Taifa ya Tanzania. Lilian anaongea Kiswahili, Kifaransa na Kiingereza kwa ufasaha.

Maryam Kazerooni Kiongozi msanifu

Maryam KazerooniAnajulikana Duniani kote kama msanii na mbunifu wa tovuti, Maryam Kazerooni kazi yake ni kubuni na kuhakikisha Envaya inatumika kiurahisi na inafaa. Yeye pia ni kiongozi msanifu wa NGO inayojihusisha na upandaji miti iitwayo Misitu ya Jumuiya ya Kimataifa .ni mzaliwa wa  Iran, Maryam sasa anaishi na kufanya kazi San Francisco, na kwingineko tovuti yake ni http://maryamkazerooni.com/ .

Ramadhan Mgaya Mratibu Shughuri Tanzania

Ramadhan Mgaya Kama mratibu wa shughuri za Envaya nchini Tanzania, Ramadhan Mgaya hutoa msaada wa kimafunzo kwa mashirika madogo ya kijamii yanayotumia tovuti ya Envaya, pia husaidia kuendesha mikutano yetu na warsha mbalimbali ili kujenga uwezo kwa mashirika ya kiraia nchini kote. Uzoefu wake wa awali ni pamoja na kufanya kazi na NGO inayoitwa Jean Media pia kufanya kazi kama mwandishi wa habari wa kujitegemea.

Ismail Muhija Tanzania ICT Mtaalamu

Ismail Muhija Ismail Muhija anafanya kazi na kuhakikisha oparesheni ya Envaya Tanzania katika kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano vinaleta ufanisi kwa mahitaji. Ana shahada ya Teknolojia ya Habari Tanzania pia anauzoefu wa kufanya kazi na makampuni makubwa ya mawasiliano ya simu kama vile Zantel , Ismail ana uelewa wa kutosha katika teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Tanzania.

Hussein Hassan Meneja Mipango Msaidizi Tanzania

Natalino Mwenda Hussein Hassan anatoa mafunzo na msaada kwa asasi za kiraia ngazi ya chini, na anafanya kazi na timu ya Envaya ili kuhakikisha programu na huduma za Envaya zinakuwa na tija zaidi kwa mahitaji ya watumiaji. Hussein ana shahada ya kwanza ya uhifadhi wa wanyamapori kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam. Kabla ya Envaya alifanya kazi katika Manispaa ya Ilala na pia shirika la uhifadhi misitu Tanzania