Envaya

Envaya

Habari

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza kwa Kiswahili. Ona asili · Hariri tafsiri

UTEKELEZAJI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI KWA MWAKA 2012

Hili ni zoezi la nne la sensa ya watu na makazi tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania mwaka 1961. Sensa hii hufanyika baada ya miaka kumi kama utaratibu ulivyo tangu kuanza kwa zoezi hili. Kwa mwaka huu zoezi lilianza tarehe 26/08/2012 kwa nchi nzima.Umuhimu wa zoezi hili ni kujua idadi ya watanzania na makazi yao ili serikali iweze kupanga mikakati yake ya maendeleo katika sekta mbalimbali kama vile afya, kilimo, elimu, miundombinu, uwekezaji na sehemu nyingine muhimu. Pia zoezi hili linaiwezesha serikali kujua namna ya kugawanya rasilimali zake kwa wananchi wake.

Watanzania waliamshwa na makalani wa sensa katika kuhesabiwa na kuulizwa maswali kama, “ni nani aliyelala na kuamkia kwenye familia hii?”.  Kabla ya serikali kuanza kutekeleza zoezi hili tulisikia juu ya kugoma kwa makalani kutokana na kwamba walicheleweshewa malipo ya posho zao kama yalivyokuwa mapatano yao na serikali, pia tulisikia migomo mbalimbali kutoka kwa raia, viongozi wa dini na wenyeviti wa vijiji katika kona mbalimbali za nchi kwa madai ya kutoshiriki zoezi la sensa.

Kufuatia hayo yote, Envaya kama shirika la kijamii liliamua kufanya utafiti ili kujua utekelezaji wa mchakato mzima. Timu yake ilifanya utafiti wake kwa asasi zifuatazo ; AWITA, BRIGHTY Destiny TANZANIA, KINONDONI NETWORK OF PEOPLE LIVING WITH HIV, TANZANIA SCIENCE JOURNALIST ASSOCIATION , WAYETA n.k utafiti  huu ulikuwa katika mundo wa dodoso na tuliwahoji wawakilishi wa asasi zote ambazo zimetajwa hapo juu ili kupata maoni yao juu ya utekelezaji wa zoezi la sensa 2012.

Mfano mmoja wa mhojiwa ambaye aliomba jina lisiandikwe, aliilaumu serikali kwa kushindwa kutoa elimu ya kutosha kuhusu sensa kwa wananchi,aliendelea kusisitiza kuwa  wananchi wengi wa Tanzania hawajui maana na madhumuni ya kuhesabia. Endapo  raia wangekuwa wameelimishwa vizuri nadhani haya maandamano na migomo isingetokea. Aliendelea kusema "baadhi ya maswali yanakuja akilini mwetu kwamba : kwani serikali ya Tanzania haijawahi kufanya zoezi kama hili kwa miaka iliyopita? Sasa mbona tunakuwa wageni wa jambo hili? Hii sasa hivi ni sensa ya nne katika nchi yetu kwanini tumeshindwa kujirekebisha? Matatizo yanajirudia yaleyale mfano; tunasikia sare za makalani hakuna, posho hakuna, vitendea kazi hakuna kwa ujumla kwanini serikali inashindwa kujirekebisha? Alisisitiza mhojiwa mbele ya timu ya Envaya kwa kusema serikali yetu inaigiza sana!”

Baadhi ya watu wanaona zoezi la sensa kwa wiki nzima ni muda mrefu na halina maana, wakati wengine wanakiri na kusema kwamba ni zoezi ambalo lina umuhimu mkubwa sana kwa nchi. Pia kuna wengine ambao wanaliona zoezi hili la sensa kama utamaduni tu wa kila baada ya miaka kumi lakini kimsingi halina maana.

Mwanamke kutoka AWITA alisema "baadhi ya watu walishiriki kikamilifu katika utekelezaji wa zoezi hili, lakini japokuwa walishiriki wala hawaoni faida yoyote ya kuhesabiwa. Alisema “hatuoni faida yoyote na wala hakuna dalili zozote za mabadiliko katika maendeleo, naona serikali inafanya zoezi hili ili labda tu kujisifia mbele ya mataifa mengine kwamba ina idadi kubwa ya watu. Baada ya sensa huwa hatuoni taarifa yoyote kurudi kwa wananchi, na kuambiwa mikakati yoyote ya kimaendeleo itakayofanyika baada ya zoezi la sensa”.

Timu ya Envaya iligundua kuwa baadhi ya maeneo kulikuwa na hali ya kutoelewana baina ya wenyeviti wa mitaa/vijiji na makalani wa sense. Eneo kama la Manzese  makalani wengine walipata shida sana kwa sababu walikuta nyumba nyingine zimefungwa na hakuna mtu. Wengine walifukuzwa kwa visu na mapanga na pia makalani wengine walishindwa kuruhusiwa kwenye familia zingine kufanya zoezi hilo kwasababu hawakuwa na sare za kazi. Alisisitiza kijana kutoka asasi ya BRIGHT DESTINY TANZANIA (BDT).

Wengi wa waliohojiwa kupitia dodoso za timu ya Envaya walisema suala la kugomea zoezi la sensa kwa baadhi ya wananchi ni kutokana na ukosefu wa elimu ya sensa. Walisema kama serikali ingekuwa imetoa elimu ya kutosha kwa wananchi wake maana ya sensa, umuhimu na faida zake hakuna mtu hata mmoja angegoma  kuhesabiwa. Walisema pia serikali haipaswi kuwashitaki wale waliogomea zoezi hili kwasababu si kosa lao bali ni kosa la serikali yenyewe kutokutoa elimu ya sensa.

Vile vile, waliohojiwa walisema ili serikali kwa siku za usoni iweze kufanikisha zoezi hili kwa ufanisi mkubwa lazima ishirikishe kwa ukaribu sana viongozi wa ngazi za chini kabisa kama wajumbe na mabalozi kwa maana hao ndo wanaishi karibu na jamii zao wanazielewa familia zote kwahiyo taarifa zitakazotolewa kwa kalani mbele ya mjumbe zinakuwa zina ukweli mkubwa. Sahivi watu hawatoi taarifa za ukweli kwa makalani kwa sababu hawawajui na kulingina na mila zetu mtu hawezi kutoa taarifa zenye ukweli kwa mtu asiyemjua.

Alisema mmoja wa mhojiwa, kwa sababu sensa ina umuhimu katika kuweka misingi ya kimaendeleo ya nchi, kama serikali itakuwa inatoa taarifa kwa wananchi ya nini kimefanyika baada ya sensa, watu wataelimika na watakuwa tayari kuhesabiwa kwa hiari kabisa na si kwa kulazimishwa kwa sababu watakuwa wameshajua umuhimu wa kuhesabiwa.

Alisema mmoja wa mhojiwa, pia natoa ushauri kwa viongozi wote wa dini lazima kuwaelimisha wafuasi wao juu ya umuhimu wa sensa katika nchi yoyote badala ya kuwahimiza kugoma, kwa sababu viongozi wa dini wana nguvu na ushawishi mkubwa sana kwa waumini wao.

Fikira iliyotawala juu ya zoezi lote hili la sensa ni kwamba wananchi wanahitaji kujua zaidi kuhusu umuhimu wa zoezi hili ambalo hufanyika kila baada ya miezi 10. Ndani ya wiki ya zoezi hili la sensa tumeona vipindi vingi kwenye runinga na kusikia kwenye maredio kuhusu umuhimu wa sensa, lakina bado jamii inahitaji taarifa zaidi ili kuelewa haswa sensa ina umuhimu gani na inamaana gani. Kwa bahati mbaya watu wengi wamegundua baadae sana umuhumu wa sensa ambapo zoezi limeshamalizika. Ni jukumu letu kama mashirika madogo na makubwa yasiyo ya kiserikali kujua umuhimu wa sensa na kuelimisha jamii zetu. Kama tunaona hata sisi wenyewe hatujaelewa tusisite kufuata taarifa serekalini hata kuomba semina kwaajila ya mashirika kama yetu ili tuweze kuelewa na kuelewesha jamii zetu kuhusu zoezi hili...

Toa maoni yako hapo chini!

25 Oktoba, 2012
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (11)

Orphans and Vulnerable Children Care (OVCC) (Puma --Singida) alisema:
About the fourth Tanzania's National Census, is that the Government should include the sub-villages leaders in the census' budget so that it would be easier for the enumerators to reach all homes being with those sub-villages leaders. This is because the sub-villages leaders know their people have even some of their phone numbers to simplify communication for the easily implementation of the practice.
There were also in our areas people who disliked to be counted reasoning that they don't see any support from the government because they still strugle with hard life since a long time without realizing any life change any longer.
So those people on the other side were challenging the government to be keen in serving its people equally.
5 Novemba, 2012
Mohammed Saleh (Zanzibar) alisema:
At least I'm now relieved that its over or is it a beggining. The census was the shortest ever experienced here in Zanzibar, Tanzania or Uganda. I have been lucky enough to have lived in the east african territories at time of census and was a big wonder to the brief queries and off packing the numerators went away just like that! Anyway I expected the census to have mainstremed literacy, nutrition, income poverty along I did never ever thing it mearely head counting?
21 Novemba, 2012
LeonardBernard (United States) alisema:

A lot of work is being done for Tanzanian citizens who are unaware of the meaning and the purpose of being counted.so many techniques have been introduced in the market.I got to read a similar related publication on buying coursework in UK that was actually amazing for me. I think everyone should read that.

23 Juni, 2020 (ilihaririwa 23 Juni, 2020)
mr seo alisema:
Thanks
6 Julai, 2020
[maoni yamefutwa]
[maoni yamefutwa]
[maoni yamefutwa]
Watson (United States) alisema:

The main challenge face we CBOs and NGOs is financial sustainability for our activities and administrations cost. Stickman Hook

21 Desemba, 2020 (ilihaririwa 21 Desemba, 2020)
skribblio (Hoa Kỳ) alisema:

Xin chào, mình là thành viên mới, mình xin giới thiệu với các bạn một trò chơi cực hay, miễn phí và không có quảng cáo. skribblio

6 Aprili, 2021 (ilihaririwa 6 Aprili, 2021)
play solitaire (United States) alisema:

Your comments on the forum are very reasonable, hope you add comments to the cookie clicker website for us to improve further, and thank you for your comments.

13 Novemba, 2021 (ilihaririwa 13 Novemba, 2021)
ayushi gupta (Alwar, ) alisema:
The engine of the Tata Prima truck models is fitted with advanced technological solutions https://trucks.tractorjunction.com/en/tata/prima that deliver high productive power and excellent fuel mileage. These trucks are built with superior quality material, a strong and safe cabin and robust suspension that make one of the safe trucks.Hello, Thanks for this post. It was really interesting to read and wonderful.
<a href="https://trucks.tractorjunction.com/en/tata/prima">tata prima </a>

9 Desemba, 2021
ayushi gupta (Alwar, ) alisema:
The Tata Prima trucks are heavy-duty trucks that Hello, Thanks for this post. It was really interesting to read and wonderful.
<a href="https://trucks.tractorjunction.com/en/tata/prima">tata prima </a>
can take one of the most challenging construction operations and mining project works.
9 Desemba, 2021 (ilihaririwa 9 Desemba, 2021)
ayushi gupta (Alwar, ) alisema:
The Tata Prima trucks are heavy-duty trucks that Hello, Thanks for this post. It was really interesting to read and wonderful.
<a href="https://trucks.tractorjunction.com/en/tata/prima">tata prima</a>
can take one of the most challenging construction operations and mining project works.
9 Desemba, 2021
Marilyn K alisema:

Not everyone loves history but I used to listen and read historical things like "Execution and the Criminal Corpse in Early Modern Europe", i'm also doing an online course of history at Findcourses recognition, but i need help about the future and market value of a person who has good knowledge of history.

9 Desemba, 2021 (ilihaririwa 9 Desemba, 2021)

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.