Envaya

Envaya

Habari

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza kwa Kiswahili. Ona asili · Hariri tafsiri

Ushiriki wa asasi za kiraia katika kuachana na mila hatarishi katika Tanzani

Tanzania ni nchi yenye utajiri wa mila na utamaduni na hujivunia hazina za urithi wao.Utamaduni wa kitanzania ni mzuri sana wenye heshima na adabu katika jamii. lugha rasmi nchiniTanzania ni Kiswahili lakini pia watu wengi huzungumza Kiingereza. Watu wa Tanzania wanajulikana sana kwa ukarimu na upole.

Kuna uelewa ambao unaendelea kukua nchini Tanzania wa madhara yanayosababishwa na tamaduni si tu kwa ajili ya watoto na vijana bali pia kwa wanawake. Uelewa huu umesababishwa kwa kuibuka asasi mbalimbali za kiraia ambazo zimekuwa zikifanya kampeni kwa ajili ya kukomesha tamaduni mbaya katika jamii.Asasi hizi ni pamoja na TAMWA, WAMA, AFRICAN Upendo GROUP, TAWA na TUNAWEZA WOMEN GROUP ambazo zinapinga unyanyasaji dhidi ya wanawake. TGNT na SWAAT hupambana na ubaguzi wa kijinsia na wanawake walio katika hatari ya kuambukizwa VVU / UKIMWI. KULEANA ambayo inakabiliana na kukomesha adhabu ya viboko kwa watoto na TANZANIA ALBINO SOCIETY ambayo inatetea mauaji dhidi ya binadamu wenye ulemevu wa ngozi (albino).

Sehemu kubwa ya jamii za kitanzania wana utaratibu wa kurithi wajane, mwanaume aliyefiwa na mke wake anaweza "kuoa" ndugu wa marehemu mke wake kwa lengo la kutunza watoto wa dada yake ambao pia huonekana kama watoto wake. Familia ya mwanamke aliyefariki huwa ni jukumu lao kumpatia mkwe wao mbadala wa kumrithi mke wake aliyefariki, na familia inaweza kumchagua binti yeyote kutoka kwenye familia bila hata makubaliano kati ya mume na binti anayemrithi dada yake. Utamaduni huu ni wa hatari sana maana unaweza kuleta maambukizi ya ukimwi kwa mwanamke anayerithiwa na mume aliyefiwa na mke, inawezekana dada yake alikufa na VVU naye pia atapata maambukizo hayo.


Ukeketaji-Katika mikoa kadhaa nchini Tanzania jambo hili limekuwa ni la kawaida, ambapo jamii hizo zinaelezea kwamba ukeketaji unadhibiti kujamiiana kwa mwanamke na kwa hivyo inapunguza nafasi ya mwanamke kuwa na wapenzi wengi. Ukeketaji ni hatari katika afya ya uzazi kwa sababu huathiri haki ya mwanamke kufurahia tendo la ndoa na zaidi inaweza kumsababishia ugonjwa wa fistula wakati wa kujifungua endapo makovu ya kidonda kitakapochanika na kusababisha kutokwa na damu nyingi ambayo pia inaweza kuwa mbaya. Nchini Tanzania vitendo hivi vinafanywa na baadhi ya makabila machache, hivyo hata kampeni ya kukomesha vitendo hivi inaonekana kufanikiwa sana.
Mauaji ya Albino. Mauaji ya albino yanasababishwa na fikra potufu katika jamii kama vile (uchawi, mali, siasa nk) na ubaguzi wa rangi.Utokomezaji wa mauaji haya umekuwa ni mgumu sana, hii inatokana na kukosekana kwa sheria ya uchawi, ukosefu wa utayari wa serikali, na kuongezeka kwa ubaguzi wa rangi katika nyanja ya utamaduni. Kwa kutaja baadhi ya hayo machache hufanya mbinu za kuzuia mauaji kushindwa na hatimaye kuongezaka kwa mauaji hayo. Ni mpaka matatizo haya yote yashughulikiwe haraka ndipo wenzetu albino nchini Tanzania watakuwa salama.

Ndoa za mapema. Wasichana bado wanabaguliwa katika jamii nyingi za kitanzania, kwasababu wasichana wadogo wenye umri kuanzia miaka 11 wanaachishwa shule na wazazi wao ili waolewe. Kwa upande wa afya jambo hili ni ni hatari, kwa sababu viungo vya msichana huyu havijakomaa kwa hivyo wengi viungo vyao hupasuka wakati wa kujamiiana, na hivyo kusababisha maambukizi ya VVU au mimba za mapema. Utafiti unaonyesha wasichana wengi wameachishwa shule ili kuolewa au kujiingiza mapema katika vitendo vya ngono ili kujitegemea kifedha hasa ukosefu wa ajira na umaskini miongoni mwa wasichana, ukosefu wa taarifa kuhusu masuala ya ngono na ujinga na ukosefu wa elimu miongoni mwa wasichana.

Unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na kumtolea matusi mwanamke, kumshika na kumgusa mwili wake bila ridhaa mfano kwenye nywele, makalio, au matiti. Kuonyesha picha za utupu za wanawake, kumwonyesha mwanamke picha za ngono bila ridhaa yake na kumwongelesha maneno ya kashifa mwanamke wakati anapopita mbele ya wanaume, kumbaka na kumpiga mke wako kama ishara ya upendo katika baadhi ya makabila.

Mahudhurio ya Mwanaume kliniki. Katika jamii nyingi za kitanzania kina mama tu ndio huwa wenye jukumu la kuhudhuria kliniki. Wakati pia ni jambo la muhimu sana kwa kina baba kuwasindikiza wake zao kliniki ili kupata ushauri na nasaha mbalimbali, pia kupata elimu juu ya masuala muhimu sana yahusuyo uzazi wa mpango na VVU. Pamoja na hayo yote serikali inapaswa kujaribu kuzifanya kliniki ziwe rafiki kwa wanaume kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake ambao wanahudhuria kliniki na waume/wapenzi zao na pia wanaume ambao huleta watoto wao.

Mauaji ya wanawake wenye macho mekundu.  Cha kushangaza mamia ya wanawake wazee wanauawa kila mwaka kwa tuhuma za uchawi baada ya kupata wao wanachokiita ukweli kutoka kwa baadhi ya waganga wa jadi.Wengi wa wanawake wazee wenye macho mekundu wanauawa hasa katika ukanda wa ziwa victoria, watu hushindwa kuelewa kwamba wanawake wenye macho mekundu wameathiriwa na moshi wakati wa kupika. Wanapopika kila siku kwa kutumia majiko ya kuni wanavuta hewa yenye kiasi cha gesi ya sumu. Kutokana na uhaba wa kuni, wakati mwingine mavi ya ng'ombe hutumika kama mbadala kwa kuni. Hivyo kwa kutumia nishati za kupikia ambazo hazina ubora husababisha macho kuwa mekundu.

 

 

a

 

4 Julai, 2012
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (8)

frank (Dar es salaam) alisema:
I appreciate the job that you doing, and not only that there is a place like iringa in kilolo i saw people are living hard life and students walk without shoes i like to be one of the volunteer in this organisation contact me though e mail frankjose11@yahóo.com
19 Julai, 2012
beatrice (Dar es salaam) alisema:
hi..i just completed my university degree and am looking for a place to volunteer can you be of help please..bittytianoi@yahoo.com
14 Agosti, 2012
Envaya alisema:
If you are looking to Volunteer with an Ngo please visit our Volunteer Page : http://envaya.org/pg/volunteer and contact these Ngo's directly. Thank you.
16 Agosti, 2012
Thank you for this, please be informed that we are involved
21 Agosti, 2012
Adam Daudi (Kibaha) alisema:
More and more Tanzanians now believe in witchcraft. The country has become notorious for albino killings( lake zone), killing of elderly women(Lake zone),skinning of human beings( Mbeya)... the list of witchcraft based human rights violations is increasing. Now even Bishops, Imams and political leaders are believed to be superstitious. In this era of science and technology, we are moving backwards as others are moving forward! Shame on us Tanzanians!
3 Septemba, 2012
ABHASU( Agency for Better Hope and Social Unity) (Mbeya City) alisema:

We need liberal education that can set our nation free of all these superstitious mindset. People should be well informed that only hard working can make socioeconomic development a reality. No shortcuts in life. I wish all Tanzanian good work not goo luck.

4 Septemba, 2012 (ilihaririwa 4 Septemba, 2012)
Justin T.E (Arusha.) alisema:
Basically that is awesome work done!
But still,we us society needs program expansivity to reach more victims of social-cultural practices..
18 Oktoba, 2012
Ed Scipio (New York) alisema:

Kids can train brain with 2048 game.

19 Machi, 2021 (ilihaririwa 19 Machi, 2021)

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.