Envaya sasa imejenga uwezo unaokuwezesha kutumia Envaya kutoka kwenye simu yoyote ya mkononi, nchini Tanzania na nchi nyingine nyingi duniani, hata bila intaneti.
Sasa hivi, unaweza kufanya hatua zifuatazo kupitia SMS na MMS:
- kuchapisha habari fupi na picha kwenye tovuti ya asasi yako
- Kujiunga ili kupata habari mpya kutoka kwenye shirika utakalo lichagua kwenye envaya.
- Kutafuta mashirika kwenye envaya kwa jina au eneo
- kupata data za mawasiliano( jina,eneo,namba za simu,barua pepe, na tovuti.
- kusoma habari zilizochapishwa na mashirika yeyote kwenye Envaya
- Kuweka maoni kwenye habari yeyote iliyochapishwa na shirika lolote kwenye envaya.
- kusoma maoni kwenye habari yeyote mpya kwenye envaya/
Bei za kawaida hutumika kwaajili ya kupeleka ujumbe mfupi kwa Envaya.
(Tanzania) 0763 077,677
(Nchi nyingine) + 1 484 544 4443
Sehemu za chini zinaeleza amri ambazo unaweza kuzitumia kwenye Envaya SMS.
P: Kuweka Habari Mpya Kwenye Tovuti Yako.
Ili kuweke habari mpya kwenye tovuti yako tuma herufi:
P [ujumbe wako hapa]
Example: "P hii ni habari yangu mpya"
Kama untumia Envaya ya kimataifa utatumia namba (+1) namba ya simu na ujumbe wako unatakiwa uwe na tarakimu 160. Ikiwa unatumia namba nyengine (kama namba ya Tanzania) ujumbe wako unaweza na urefu unaoutaka wewe.
Kama ujumbe wako umetumwa vizuri Envaya itakutumia jibu lifwatalo:
Habari yako imechapishwa kwenye "N exampleorg" na http://envaya.org/testorg/news. Ukitaka kufuta tuma "DELETE 58934"
Mtu yeyote anaweza kuona habari uliochapisha aidha kwenye simu au kupita tovuti yako kwenye mtandao. Tunawasihi kusambaza tovuti za mashirika yenu na pia amri za SMS ("N [jina la mtumiaji]" ) kwa watu wengine ili waweze kusoma habari zako.
Note: herufi P ni amri itakayo takiwa ifwatiwe na kuingia kwenye akaunti yako ya Envaya. soma zaidi amri ya "IN".
U: Habari mpya
Ili kuona habari mpya kwenye mashirika yote kwenye envaya tuma herufi:
U
Amri ya 'U' itajibiwa na matokeo yafwatayo:
29Aug N NYEDACO I taswo I Fihata N TACOMO 28Aug N yesvijana N TEYODEN N zop
Kila mstari unaonyesha jina la mtumiaji na aina ya habari mpya (N kwaajili ya habari mya, I kwaajili ya data za mawasiliano), na pia amri unayotakiwa kutuma ili upate habari ziada.
Kwamfano, tuma "N NYEDACO" Ili kupata habari mpya kutoka Nyengedi Environment Development and Diseases Control, au "I taswo" ili kuona data za mawasiliano za Tanzania Support for Widows and Orphanz.
Kila unapochapisha habari mpya (aidha kupitia kwenye SMS kwa kutumia amri "P" au kupitia envay.org) shirika lako litakuwa katika sehemu ya juu kwenye orodha ya mashirika pindi mtu atakapo tumia amri ys "u" ili kupata habari mpya.
F: Kutafuta mashirika kwa kutumia majina
Ili kutafuta mashirika kwa kutumia majina tuma:
F [Jina la shirika]
mfano: "F mwanza youth children network"
mfano: "F environment" (jina la shirika lolote lenye neno environment)
Example: "F je" (mashirika yenye majina yanaoanza na 'je')
amri "F je" italeta matokkeo yafwatayo
[1/2] jeanmedia guluka ileje keca wecocpemba WEPMO moeco cadecttrust EMNet WEETU mcaee sehap-tanzania BAENET pemwa Txt "I [user]" for details
Kila mstari utaonjesha majina ya mashirika kwenye Envaya yanayo fanana na kile ulichokuwa unakutafuta( kwa sasa "F environment"). katika mfano huu [1/2] inamaanisha kwamba matikeo ni mengi sana kutosha kwenye ukurasa mmoja wa sms, na ukurasa utakao kuwa unauangalia ni wa kwanza katika matokeo yenye kurasa mbili. Ukitaka kuona matokeo mengine ya kwenye kurasa ya pili, jibu neno NEXT au 2.
Ili kuona taarifa za mawasiliano za mashirika yeyote jibu na herufi "I [mtumiaji]", kwa mfano "N jeanmedia".
FN: Kutafuta mashirka kariba kwa kutoa taarifa za eneo
Ili kutafuta mashirika kwa kutumia taarifa za eneo, tuma:
FN [eneo]
mfano: "FN pemba"
Matokeo ya amri ya FN ni sawa na yale ya amri ya F .
I: angalia taarifa za mawasiliano za mashirika
Ili kuona taarifa za mawasiliano za mashirika ya shirila lolote kwenye envaya: tuma:
I [mtumiaji]
mfano: "I jeanmedia"
Matokeo yatakayo tokea kwenye amri "I" ni jina la shirka mkoa au mji,tovuti, anuani ya barua pepe na namba ya simu za(kama ni taarifa zilizo orodheshwa kuonekza hadharani). Kwa mafano
Journalists Environment and (HIV)Aids Network Dar-es-salaam TZ http://envaya.org/jeanmedia jean_media@yahoo.com 255658053107 N=habari
S=jisajili
Note: Kama hujui jina la mtumiaji la shirika unalolitafuta, tumia amri ya "F" kulitafuta.
S: Kujisajili ili kupata habari za Mashirika.
Mtu yeyote anaweze kujisajili ili kupata habari za shirika lolote atakalo lichagua kwenye Envaya. Utakapo jisajili kupata taarifa za shirika Envaya itakutumia taarifa moja kwa moja kwa ujumbe mfupi endapo shirika hilo litachapisha habari mpya kwenye Envaya.
Ili kujisajili kupota taarifa za shirika, tuma:
S [mtumiaji]
mfano: "S jeanmedia"
Utakapo jisajili Envaya itakutumia ujumbe mfupi kama ifwatavyo:
Jisajili kwenye "N jeanmedia". Tuma "STOP 3" kusimamisha usajili. Tuma "SS" Kuona taarifa zako za usajili.
baadae endapo mtumiaji huyu atakapochapisha habari yeyote, Envaya itkutumia ujumbe mfupi ufwatao:
jeanmedia imechapisha habari. Tuma "N jeanmedia 6" au nenda http://envaya.org/jeanmedia/news. ili kusimamisha usajili huu, tuma "STOP 1"
SS: Kuonyesha taarifa za usajili
Ili kuona mashirika yote ambayo umejisali kupata habari zao tuma:
SS
Kwa mfano matokeo yanaweza yakaonekana kama ifwatavyo:
1:N jeanmedia 2:N cfp 4:N mycn Txt STOP [id] to cancel any subscription
Katika mfano huu. Mstari wa kwanza unaonyesha kwamba umejiunga kupta habari za Jeanmedia, na unaweza kutuma neno "STOP 1" Ili kuondoa usajili.
STOP: kusimamisha usajili
kama unataka kusimamisha usajili ili usipate tena habari, tuma:
STOP [id]
mfano: "STOP 2"
kama unataka kusimamsha usajili wa kupata taarifa za mashirika yote, tuma:
STOP ALL
N: Kuona Habari Mpya Kutoka Mashirika mbali mbali
Ili kuona habari mpya zilizochapishwa na shirika lolote kwenye Envaya, tuma:
N [mtumiaji]
mfano: "N jeanmedia"
Matokeo yatakayotokea ya amri 'N' yataonyesha habari mpya na tarehe ya kuandikwa kwa habari hiyo a pia idadi ya maoni.
[1/60] 2Jun 2cmt@"G[num]" Wananchi watakiwa kutunza mazingira Na ASIA KILAMBWANDA,
Mtwara Wananchi Mkoani Mtwara wametakiwa kutotupa taka
hovyo hususani katika maeneo ya pwani ya bahari ya bandari
ya Mtwara na badala yake watunze na kuhifadhi maeneo hayo
kwa kuwa ni sehemu ya vivutio vinavyoingi za
MORE
Kama habari hizo ni ndefu sana, itaanza kuonekana mwanzo t wa habari hiyo. Tuma neno "MORE " ili kuendelea kusoma taarifa hizo.
Ili kuona habari zilizo pita, tuma "NEXT" au namba ya kurasa hizo.
maneno "2cmt" linamaanisha kwamba kuna maoni mawili kwenye habari unayo iangalia. Kama hamna maoni yeyote kwenye habari hiyo itasema "0cmt" C[msg] badalayake
Ili kuona maoni, tumia amri ya "G" na "C" tutakayo ielezea hapo chini.
G: Kuona maoni yaliyowekwa kwenye habari
Wakati unaangalia habari mpya, maneno "2 cmt@G[num]" yanamaanisha kwamba kuna maoni mawili kwenye habari unayoiangalia na unaweza kuangalia maoni yeyote kwa kutuma
G[num]
mfano: G1 (show the first comment)
mfano: G2 (show the second comment)
Majibu yatarudi kama ifwatavyo:
jina la mafano
Dar es Salaam
26Aug Ahsante sana!
Note: amri "G" inatumika pale utakapo tumia amri "N" ya kuangalia habari mpya tu.
C: Kuweka maoni kwenye habari mpya
Ili kuweka maoni, tuma:
C [ujumbe]
mfano: C kazi nzuri!
Note: amri "C" inatumika pale utakapo tumia amri "N" kuangalia habari mpaya tu. Pia unaweza kuongezea maona hata kama ujumbe wa C[msg] haionekani.
Jina: Kuweka jina kwenye Maoni yatakayo tumwa.
Utakapo kuwa unaweka maoni yako, Jina lako litaonekani juu katika ujumbe wako, ili kubadili jinalako linavyoonekano, tuma:
NAME [jina lako]
mfani: NAME John Doe
LOC: kuweka taarifa za maahala ulipo
Utakapo weka maoni yako, mahala ulipo(mfano. mkoa, mji) itaonekana kwenye ujumbe wako kwa chini, ilikubadili taarifa za mahala ulipo, tuma:
LOC [mahala ulipo]
mfano: LOC Dar es Salaam
L: kubaadili lugha kwenye mfumo huu was ujumbe mfupi
Ili kubadili lugha kwenye mfumo huu wa ujumbe mfupi, tuma:
L [lang]
kwa kiswahili: "L sw"
kwa English: "L en"
kwa Kinyarwanda: "L rw"
IN: Kufungua akaunti yako ya envaya
To log in to your Envaya account, text:
IN [jina la mtumiaji] [neno la siri]
Mfano: "IN shirikalamfano nenolakolasiri"
Note: Amri nyingi kwenye Envaya hazihitaji uingie kwenye akaunti yako, lakini unahitaji kuingia ili kuchapisha habari na amri ya P. utakapoingia kwenye akaunti yako utaendelea kuwa kwenye akaunti yako mpaka pale utakapo ondoka
OUT: Kuondoka kwenye akaunti yako ya Envaya
Ili kuondoka kwenye akaunti yako ya Envaya, tuma:
OUT
NEXT/MORE/#: Kuperuzi kurasa
Kama majibu yanarudi alafu yanaanza na[#/#], hii inamaanisha kwamba kuna kurasa nyengine zaidi ya hiyo unayoiangalia. Namba ya kwanza ndio namba ya ukurasa uaouangalia na namba ya pili ndio idadi ya kurasa zote. Ili kuenda kwenye ukurasa ufwatao,tuma neno, "NEXT" (au X kwa kifupi). Ili kuruka ukurasa tuma nambari ya ukurasa huo.
kwa mfano, tuma "4" ilikuona matokea ya ukurasa wa 4.
Kama matokea ya ujumbe yanaanza na"MORE" hii inamaanisha kwamba matokeo ni marefu sana kutosha kwenye ukurasa mmoja wa ujumbe mfupi> ili kuona kurasa nyengine zaidi, tuma MORE
H: Orodha Ya amri zilizopo
Ili kuona Orodha ya amri zilizopo, tuma:
H
HELP au MENU pia italeta matokeo hayo hayo.
Matokeo yatakayo tokea baada ya amri ya masaada yataonekana kama ifwatavyo:
Envaya SMS NEXT=next page 1-2=goto page P=publish news F=find orgs I=contact info N=latest news OUT=log out
Note: Orodha iliyopo inaweza kubadilika kutokana na amri zilizopita.