Envaya

Envaya

Kutumia Envaya katika Lugha yako

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza, lakini tamko la Kiswahili ni la zamani. Ona asili · Hariri tafsiri
Msaada

Kutumia Envaya katika Lugha yako

Envaya imetafsiriwa kwa lugha mbalimbali, na unaweza kutumia lugha yoyote unayotaka kuitumia.

Ili kubadili lugha ya Envaya, bonyeza menyu ya Lugha au Language juu ya ukurasa wowote wa Envaya, halafu chagua lugha kutoka kwenye orodha.

Vile vile, unaweza kubadili lugha ya Envaya kwa ku-scroll mpaka chini ya ukurasa, na kubonyeza jina ya lugha pale chini kushoto.

Kutafsiri maandiko Kutoka Lugha nyingine

Mashirika yanayotumia Envaya yanaweza kuchapisha maandiko kwa lugha yoyote yapendayo. Kama unasoma tovuti ya shirika jingine kwenye Envaya, maandiko yao yanaonekana kwa kawaida kwa lugha yao, ambayo labda ni tofauti na lugha unayoitumia kwenye Envaya.

Inapowezekana, Envaya itachunguza lugha ya ukurasa wa sasa na kukuruhusu kutafsiri ukurasa kwa lugha yako. Kama inawezekana, kutakuwepo sehemu karibu ya juu ya kurasa yenye kiungo kitachotafsiri ukurasa kwa lugha yako, kama inavyoonekana hapo chini:

Unaposoma kurasa kupitia Google Translate, huduma ya kujiendesha ya tafsiri ya kompyuta, labda tafsiri itakuwa pungufu au na makosa.

Kuboresha Tafsiri ya Envaya

Mtu yeyote anakaribishwa kusaidia kuboresha tafsiri za Envaya kwenye tovuti ya Tafsiri ya Envaya, http://envaya.org/tr . Kwenye tovuti ya Tafsiri, unaweza kusahihisha maneno yoyote yalio ya tafsiri ya kimakosa. Pia, unaweza kuongeza tafsiri mpya, na kupiga kura na kuandika maoni juu ya tafsiri zilizopo.

Kwa maelekezo ya kuchangia kwa tovuti ya Tafsiri ya Envaya, nenda http://envaya.org/tr/instructions .