Kusambaza na Kutangaza Tovuti yako
Tunakusisitiza kusambaza tovuti ya asasi yako na watu wengine wengi - wanajamii, mashirika ya ubia, na wanachama wako wenyewe! Tovuti ya asasi yako itakuwa muhimu zaidi kama watu zaidi waijue, na waitumie ili kushirikiana na asasi yako. Kwa hivyo, waambie watu kuhusu tovuti yako! Vile vile, tunapendekeza uongeze anwani ya tovuti ya asasi yako kwa alama na barua za asasi yako.
Kupitia Envaya, ni rahisi kusambaza ukurasa wowote wa tovuti yako na watu wengine kupitia barua pepe, au kwenye tovuti nyingine maarufu kama Facebook au Twitter. Kwa kawaida, tovuti yako ya Envaya ina viungo juu ya ukurasa, kama hapo chini:
Ili kupeleka kiungo kwa tovuti yako, nenda kwenye ukurasa ambao ungependa kuusambaza, kisha kubonyeza Sambaza kupitia email. Dirisha jingine litaonekana ambapo unaweza kuingia anwani za barua pepe na kuchapa ujumbe wa mwaliko:
Ili kuongeza anwani za email za mashirika mengine kwenye Envaya kwa urahisi, bonyeza Ongeza watumiaji wa Envaya. (Angalia: Uwezo huu unapatikana tu baada ya asasi yako kukubaliwa na wasimamizi wa Envaya.) Halafu, tafuta mashirika mengine ambayo ungependa kuyakaribisha na bonyeza kila moja. Bonyeza Close wakati ambapo umemaliza.
Pia unaweza kuwakaribisha kwa urahisi mashirika yote ya ubia ya shirika lako kwa kubonyeza Ongeza mashirika ya ubia.