Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza kwa Kiswahili. Ona asili · Hariri tafsiri
Envaya inakuwezesha kuwasiliana na mashirika mengine ambayo wana akaunti ya Envaya.
Wakati umeingia kwenye akaunti yako ya Envaya, kutembelea tovuti ya shirika lingine,bonyeza kiungo juu cha kutuma ujumbe.
Kisha, andika ujumbe wako na bonyeza Tuma Ujumbe kutuma ujumbe wako kwa shirika kupitia barua pepe.
Kupata Mawasiliano ya mashirika mengine
Kama shirika limechapisha anwani za barua pepe au namba ya simu kwenye tovuti yao, unaweza kupata mawasiliano yao kwa urahisi na kuwasiliana nao moja kwa moja.
Wakati unaangalia tovuti ya shirika lolote kwenye Envaya, bonyeza Mawasiliano katika orodha ya tovuti yao:
Ifuatayo: Kutoa Maoni juu ya Habari
Iliyotangulia: Kuchangia kwenye Majadiliano