Kujiandikisha Shirika lako kwenye Envaya
Katika dakika chache tu unaweza kuandikisha shirika lako la kijamii jamii kwenye tovuti ya Envaya, bure kabisa, kwenye kompyuta yenye mtandao. (Kwa mashirika ya kiraia yaliopo Tanzania na Rwanda, si lazima kuomba kibali kabla ya kusajili Envaya.)
Kusajili shirika lako, nenda kwanza http://envaya.org kwa kutumia browser yoyote ya mtandao na bonyeza Jiunge Sasa au Sign up now, kama ilivyo hapa chini:
Sifa
Kisha utaulizwa maswali kadhaa ili kuhakikisha kwamba shirika lako lina sifa za kutumia Envaya. Chagua majibu yanayolingana na shirika lako, kisha bonyeza kifungo cha bluu chini ya ukurasa.
Kujenga Akaunti Yako
Kama asasi yako ina sifa ya kutumia Envaya, ukurasa unaofuatia utakuwezesha kujenda akaunti ya asasi yako. Katika ukurasa huu, unahitaji kuingiza jina la asasi yako na namba za mawasiliano, na kuchagua jina la mtumiaji na neno la siri kwa shirika lako.
Jina la mtumiaji linatakiwa liwe fupi au kifupi cha asasi yako. Jina la mtumiaji litatumika kwenye anwani ya mtandao wa asasi yako. Kwa mfano, kama jina lako ni jeanmedia, anwani ya mtandao wako itakuwa http://envaya.org/jeanmedia.
Neno la siri au password yako inatakiwa iwe neno au sentensi fupi ya kisiri, iwe angalau na herufi 6. Jina la mtumiaji na neno la siri litakuwezesha kuingia na kuhariri tovuti la shirika lako. Kumbuka neno lako la siri na kulitoa kwa watu ambao wanaruhusiwa hariri tovuti ya asasi yako tu.
Kama asasi yako ina anwani ya barua pepe au namba ya simu, Envaya inaweza kuzitumia kuwasiliana na wewe, kwa lengo la kuthibitisha shirika lako, kusaidia kama umesahau neno la siri, na kuwasiliana na wewe kuhusu mabadiliko mapya na Envaya.
Utakapokuwa umeweka taarifa zote, bonyeza kifungo cha bluu chini ya ukurasa ili uendele. Kama ujumbe mwekundu utatokezea juu ya ukurasa , sahihisha makosa na kisha bonyeza kifungo cha bluu tena.
Hariri Ukurasa wako Mkuu
Hatua ya mwisho katika kusajili asasi yako ni kuingiza taarifa ambazo Envaya itatumia kujenga Ukurasa wako mkuu yaani homepage ya awali kwa ajili ya tovuti ya asasi yako.
Fuata maelekezo katika ukurasa huu kuingiza malengo ya asasi yako, chagua hadi sekta 5 zinazohusiana na shirika lako, ingiza mji na mkoa ambapo shirika linapatikana, na chagua muonekano wa tovuti yako.
Utakapomaliza bonyeza kifungu cha bluu chini ya ukurasa. Kama kuna kosa lolote ujumbe mwekundu utajitokeza. Sahihisha makosa na bonyeza batani cha bluu tena.
Hatimaye, Envaya itakupeleka kwenye tovuti ya asasi yako mpya. Watendaji wa Envaya watajulishwa kuwa shirika lako limesajiliwa, na wanahitaji kuikubali tovuti yako kabla ya kuonekana hadharani kwenye mtandao, ili kuhakikisha kwamba shirika lako lina sifa za kutumia Envaya. Kama uliingiza anwani ya barua pepe ya shirika lako, Envaya litakutumia barua pepe ya tovuti ya asasi yako ikikubaliwa.
Hata wakati unashubiri tathmini ya watendaji wa Envaya, unaweza kuendelea kuhariri tovuti yako na kuongeza kurasa nyingine na habari kuhusu shirika lako, kama itakavyoelezwa katika kurasa zifuatazo.