Envaya

Envaya

Utambulisho kwa Envaya

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza, lakini tamko la Kiswahili ni la zamani. Ona asili · Hariri tafsiri
Msaada

Utambulisho kwa Envaya

Envaya inatoa huduma kwa mashirika ya jumuiya ya kiraia kupata tovuti bila malipo yoyote, kuchapisha habari, picha, na hati mpya, kuwasiliana na wafadhili, na kushirikiana na mashirika mengine na watu duniani kote.

Sasa, zaidi ya mashirika 600 ya kiraia yanatumia Envaya, kutoka asasi ndogo kwa NGOs kubwa. Mashirika juu ya Envaya yanafanya kazi ya aina mbalimbali, kama kutetea mabadiliko, kuendeleza mipango mipya ya kupunguza umaskini, na kuendesha miradi kuhusu elimu ya VVU/UKIMWI na kupanda miti.

Hapo chini, ipo baadhi ya faida kuu ya kutumia Envaya kwa shirika lako:

Ni Rahisi ya Kutumia: Ili kufungua tovuti yako kupitia Envaya, si lazima uwe na ujuzi mkubwa sana wa kompyuta au kifaa chochote. Kwa muda wa dakika tano tu, unaweza kutengeneza ukurasa mkuu wewe mwenyewe.

Ni Bure: Kuajiri mtu kukutengenezea tovuti na kuihudumia ni ghali sana. Zingatia, Envaya ni bure kabisa.

Inapatikana kwenye Simu: Tovuti yako katika Envaya inapatikana katika simu za mkononi zenye intaneti. 

Envaya kwenye simu yenye intaneti

Inayoonekana:  Envaya inaunganisha tovuti yako katika mtandao wake ili watu waweze kuona tovuti yako kwa urahisi wakati watafutapo mashirika ya jumuiya ya kiraia (kama lako).

Imetafsiriwa: Envaya imetafsiriwa kwa Kiswahili na Kiingereza, ili uweze kutumia lugha yoyote unayoipenda. Mtu yeyote asiejua kusoma lugha yako anapotembelea tovuti yako, Envaya itatafsiri maandiko yako kwa lugha anayotumia.

Ni Shirikishi: Kwenye Envaya, unaweza kuona kazi zinazofanywa na mashirika mengine, kuwapeleka ujumbe, na kuna majadiliano pamoja nao. Kama shirika ambalo liko mbali sana likiwa na mradi mzuri na likiandika katika Envaya kuhusu mradi huo, unaweza kuisoma na kupata mawazo kwa shirika lako.

Upatikanaji

Kwa sasa, Envaya inapatikana kwa mashirika ya kiraia katika Tanzania na Rwanda. Ikiwa wewe ni mwakilishi wa shirika la jumuiya ya kiraia Tanzania ambalo halijajiandikisha kwa Envaya, jiunge sasa ! Kwa maelekezo zaidi juu ya kujiandikisha kwenye Envaya, endelea kwa ukurasa unaofuata.