Kuhariri Tovuti Yako
Baada ya tovuti ya asasi yako kukubaliwa na Envaya, mtu yeyote kwenye intaneti watakuwa na uwezo wa kuona tovuti yako bila kuhitaji kujiandikisha kwenye Envaya.
Hata hivyo, wewe tu, na mtu yeyote mwingine ambaye anajua jina la mtumiaji na neno la siri ya asasi yako, wanaweza kuhariri kurasa kwenye tovuti yako wakati ambapo wamefungua ("logged in") kwenye Envaya.
Kwa kuangalia rangi ya nyuma ("background") ya ukurasa wowote, unaweza kujua kama ukurasa unaonekana hadharani, au unapatikana wakati ambapo umefungua kwenye Envaya. Kurasa zote zenye rangi ya nyuma ya kijivu zinapatikana tu wakati ambapo umefungua kwenye Envaya.
Kila mara umefungua kwenye Envaya, eneo la rangi ya bluu lenye picha lipo juu kulia wa ukurasa, kama hapo chini:
Kila moja ya picha hizi ni kiungo unachoweza kubonyeza:
-
ni ukurasa Mkuu wa asasi yako.
-
ni ukurasa wa Hariri Tovuti, ambapo unaweza kuchapisha taarifa za habari na picha na kuhariri kurasa zozote kwenye tovuti yako.
-
ni ukurasa wako wa mipangilio ya akaunti ya Envaya, ambapo unaweza kupanga upya data ya mawasiliano ya shirika lako, na mipangilio mingine.
inaondoka ya akaunti yako Envaya.
Mahali kuu ya kuhariri tovuti yako ni ukurasa wa Hariri Tovuti. Katika ukurasa huo, unaweza kuandika taarifa ya habari na kuhariri kurasa zozote kwenye tovuti yako. Wakati ambapo umefungua Envaya, unaweza daima kwenda ukurasa huo kwa kubonyeza picha .
Ili kujifunza jinsi ya kufanya kazi maalum kwenye tovuti yako, chagua sehemu kutoka kwenye orodha hapo chini.