Envaya

Envaya

Kuumba Ukurasa wa Majadiliano

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza kwa Kiswahili. Ona asili · Hariri tafsiri
Msaada : Kuhariri Tovuti Yako

Kuumba Ukurasa wa Majadiliano

Katika tovuti yako ya Envaya, unaweza kuunda ukurasa wa majadiliano, ambayo inaruhusu mtu yeyote - kutoka shirika lako au mashirika mengine, au kutoka katika jamii yako au mahali popote duniani - kushiriki na kujadili mada inayohusiana na asasi yako na kazi zake.

Kuunda ukurasa wa majadiliano, ingia kwenye akaunti yako ya Envaya na nenda kwenye ukurasa Hariri Tovuti ( ). Nenda chini kwenye sehemu ya Hariri Ukurasa, na bonyeza Majadiliano.

Kuanzisha majadiliano yako, bonyeza majadiliano

Chini ya mada, andika mada unayotaka kujadili. Kisha, andika ujumbe wako katika sanduku kubwa, na ingiza jina lako na eneo unapoishi. Kisha, bonyeza kitufe cha bluu kuchapisha mjadala wako mpya katika tovuti yako.

Hii itajenga ukurasa wako wa majadiliano katika orodha ya tovuti ya asasi yako, na kiunganishi cha majadiliano ulioanzisha.

Mtu yeyote ambaye atasoma majadiliano yako ataweza kujibu na kuongeza ujumbe mpya katika mjadala. Si lazima kuwa na akaunti ya Envaya ili kuongeza ujumbe kwenye majadiliano.

Kuwakaribisha watu kwenye majadiliano yako

Ponyeza Waalike watu kushiriki chini ya mjadala wako kutuma kiunganishi cha barua pepe kwa watu wengine na mashirika yanayoweza kuwa na nia ya kuchangia katika majadiliano.

Kisha, ingiza anwani ya barua pepe ya wale unotaka kuwakaribisha kutoa maoni. Unaweza pia kubonyeza ongeza watumiaji wa Envaya au ongeza mashirika ya ubia ilikuongeza moja kwa moja anwani ya barua pepe ya mashirika mengine yaliojiandikisha Envaya. Andika ujumbe kuwaambia watu kuhusu mjadala huu, na bonyeza kitufe cha bluu chini ya ukurasa kutuma mwaliko.