Fungua
dhulusportsclub

dhulusportsclub

mwanzacity, Tanzania

Ndugu wadau...!! Uongoz wa Dhulu Sports Club unapenda kuwajuza habari zifuatazo.....

1.Bado club inahitaji wanachama hivyo kwa mdau yeyote anayependa kujiunga nasi nafasi zipo wazi anakaribishwa....

2.kuanzia wiki ijayo uongoz wa club utaanza tembelea shule husika jijini Mwanza kwa ajiri ya kufanya semina na wanafunzi pamoja na upigaji picha kwa ajiri ya utengenezaji wa vitambulisho vyao.

3.Kwa wale waliolipia ada ya uwanachama uongozi unawaomba waje ofisini kupigwa picha kwa ajiri ya vitambulisho...Kwa wale wa mbali watume passport zao kupitia email ya club(dhulusports@yahoo.com).

4.Ikiwezekana mwezi wa nne Club  itaandaa tamasha la michezo (ROCK CITY INTERSCHOOL SPORTS FESTIVAL)

                              AHSANTE

                        PAMOJA TUNAWEZI

Uongozi wa Dhulu Sports Club Unawakumbusha wale wote waliopatiwa barua za uwanachama wajitahidi kufanikisha uwanachama wao kwani siku za kulipia zinakaribia....

Hivyo kutokana na wadau kuwa na shughuli nyingi za kiofisi,kishule na majukumu mengine ya kimaisha kuwabana hadi kushindwa kufika ofisini kwetu kwa sasa,   Mchango wako unaweza utuma kwa njia ya M-PESA /TIGO-PESA kwenye namba za ofisi ambazo ni 0767260480 na 0658160480 nasi tutaipokea...

  Wadau tujitahidi kutimiza mchango huo ili hatua ya kutengeneza vitambulisho vya Uwanachama ifanyike haraka iwezekanavyo. Uongozi umeongeza siku za kupokea mchango hadi tarehe 28/02/2013 itakuwa mwisho wa kupokea michango.

       PAMOJA TUNAWEZA

Ahsanteni...

 

Baadhi ya wanafunzi ya sekondari ya Bismack iliyopo jijini Mwanza wakisikiliza semina ya afya na michezo iliyo fanyika shuleni kwao....mbele ni Kiongozi wa club na Mwanafunzi mwenzao akiwasomea baadhi ya kanuni za afya...

large.jpg

kiongozi wa Dhulu sports club (aliyeshika bahasha) akiwa na wanafunzi wa Mlimani Secondary Mwanza baada ya semina fupi ya afya juu ya dawa za kulevya na ukimwi waliyo ifanya hapo shuleni....

 

large.jpg

Katika pozi  Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bugarika iliyopo jijini Mwanza wakitafakari  baada ya kupata semina ya Afya na michezo iliyotolewa na viongozi wa Dhulu Sports Club....

large.jpg

Mwenyekiti wa Dhulu Sports Club akiwa shule ya Mwanza Sekondari jijini Mwanza akitoa elimu ya michezo na madawa ya kulevya....

 

 

large.jpg

Kushoto wa kwanza na kulia wa kwanza ni mwenyekiti(HABIBU HASSAN) na katibu (DONALD) wa Dhulu Sports Club wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya mkolani iliyopo jijini Mwanza wakiwa wamemaliza semina ya michezo na afya shuleni hapo....

 

large.jpg

Viongozi wa Dhulu Sports Club wakitoa semina ya michezo na afya mbele ya wanafunzi wa sekondari ya Buhongwa  iliyopo jijini mwanza...

large.jpg

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Islamiya wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Dhulu Sports Club....