Fungua
dhulusportsclub

dhulusportsclub

mwanzacity, Tanzania

Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

                       IJUE DHULU SPORTS CLUB!!!!

 UTANGULIZI:

Dhulu ni neno lenye asili ya kibantu lenye maana ya mabadiliko.

Hivyo Dhulu Sports Club ni club inayojishughulisha na kutafuta, kuendeleza vipaji pamoja na kutoa semina za afya na dawa za kulevya kwa vijana wa Tanzania.

Michezo tunayojiusisha nayo ni mpira wa miguu,kikapu,pete,wavu, riadha pamoja na muziki.

          Club ilisajiliwa mwaka 2010 na kupewa cheti cha usajiri chenye usajiri namba nsc9649

na kutambulika kitaifa kuwa ni miongoni wa clubs za michezo Tanzania. Kwasasa Club ina ofisi zake katika mkoa wa Mwanza wilaya ya Nyamagana mtaa wa Uhuru.

  MALENGO.

Malengo makuu ya Club ni kuinua na kuviendeleza vipaji pamoja na kuzuia utumiaji wa madawa ya kulevya na maambukizi ya ukimwi kwa vijana mashuleni (msingi na sekondari) na mitaani.

 MATARAJIO.

  • Kuifanya Dhulu Sports Club kuwa club kubwa yenye uwezo wa kusimamia michezo tajwa hapo juu na pia kuwa na shule ya vipaji kwa vijana kuanzia miaka 7 na kuendelea katika mikoa mbali mbali Tanzania.
  • Kutengeneza soko la ajira kwa vijana kupitia michezo.
  • Kupunguza idadi ya utumiaji wa dawa za kulevya na maambukizi ya ukimwi kwa vijana.

 

 HITIMISHO.

Uongozi wa club unahitaji mchango wako kimawazo,vitendo na mengine mengi kwa manufaa ya maendeleo ya club na taifa kwa ujumla.

                                                 Ahsante.

PAMOJA TUNAWEZA

 

 

Mabadiliko Mapya
dhulusportsclub imeongeza Habari.
Ndugu wadau...!! Uongoz wa Dhulu Sports Club unapenda kuwajuza habari zifuatazo..... – 1.Bado club inahitaji wanachama hivyo kwa mdau yeyote anayependa kujiunga nasi nafasi zipo wazi anakaribishwa.... – 2.kuanzia wiki ijayo uongoz wa club utaanza tembelea shule husika jijini Mwanza kwa ajiri ya kufanya semina na... Soma zaidi
24 Februari, 2013
dhulusportsclub imehariri ukurasa wa Historia.
HISTORIA YA DHULU SPORTS CLUB: – Dhulu Sports Club ni club inayojishughulisha na kutafuta, kuendeleza vipaji pamoja na kutoa semina za afya na dawa za kulevya kwa vijana wa Tanzania. – Michezo tunayojiusisha... Soma zaidi
20 Februari, 2013
dhulusportsclub imeongeza Habari.
Uongozi wa Dhulu Sports Club Unawakumbusha wale wote waliopatiwa barua za uwanachama wajitahidi kufanikisha uwanachama wao kwani siku za kulipia zinakaribia.... – Hivyo kutokana na wadau kuwa na shughuli nyingi za kiofisi,kishule na majukumu mengine ya kimaisha kuwabana hadi kushindwa kufika ofisini kwetu kwa sasa, Mchango wako... Soma zaidi
13 Februari, 2013
dhulusportsclub imeongeza Habari 6.
Baadhi ya wanafunzi ya sekondari ya Bismack iliyopo jijini Mwanza wakisikiliza semina ya afya na michezo iliyo fanyika shuleni kwao....mbele ni Kiongozi wa club na Mwanafunzi mwenzao akiwasomea baadhi ya kanuni za afya... Soma zaidi
12 Februari, 2013
dhulusportsclub imeongeza Habari.
kiongozi wa Dhulu sports club (aliyeshika bahasha) akiwa na wanafunzi wa Mlimani Secondary Mwanza baada ya semina fupi ya afya juu ya dawa za kulevya na ukimwi waliyo ifanya hapo shuleni.... Soma zaidi
12 Februari, 2013
dhulusportsclub imeumba ukurasa wa Miradi.
PROJECTS ZA DHULU SPORTS CLUB: – Projects kuu tunazojiusisha nazo ni – Utafutaji na Uendelezaji vipaji kwa vijana wa kitanzania. Kamati husika katika Club itashirikiana na meneja wa michezo katika... Soma zaidi
8 Februari, 2013
Sekta
Sehemu
mwanzacity, Mwanza, Tanzania
Tazama mashirika ambayo yapo karibu