Envaya
Parts of this page are in Swahili. View in English · Edit translations
Asasi ya kijamii "COLD" limeadhimisha siku ya mwanamke kwa kutoa mafunzo ya namna ya kutengeneza jiko la maajabu kwa wanawake wa kikundi cha Mwamko wa kata ya Igoma, jijini Mwanza. Jiko hili hutumia kuni au mkaa kidogo sana Lengo la mafunzo hayo ni kupunguza mzigo kwa wanawake waliokuwa wakilazimika kutumia muda mwingi kutafuta kuni milimani. Mafunzo hayo yameendeshwa na raisi ambaye pia ni afisa mtendaji mkuu wa asasi hii bwana Kisumva Mathew Maziku. Wakati hayo yakiendelea Mwanza, huko Dar, makamu wa raisi wa shirika hili bi Esther Mbedule aliliwakilisha katika maadhimisho hayo kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja.
March 10, 2012
« Previous Next »

Comments (1)

R.J. Chatta (Kisarawe District) said:

Kazi nzuri sana ya kutengeneza jiko la ajabu ili kumpunguzia mwanamke mzigo mzito na mkubwa ambao mwamke hubeba kila siku. Tunawaunga mkono na kazi yenu hiyo nzuri.

February 23, 2013 (edited February 23, 2013)

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.