Shindano la machapisho ya elimu ya afya kwa jamii-Mwisho Agosti 30
Kama umewahi kutengeneza au kuchapisha kipeperushi, brocha, posta au kijitabu katika Kiswahili chenye taarifa za elimu ya afya kwa jamii, unaweza kushinda zawadi!
Tuma machapisho yako katika Kiswahili ifikapo Agosti 30 na utaingizwa kwenye shindano na kuwania:
- seti nzima ya miongozo ya kiafya ya Hesperian katika Kiingereza (ukiwemo Mahali Pasipo na Daktari)-zawadi ya mshindi wa kwanza;
- kitita cha kiafya chenye nyenzo za kinga-zawadi ya mshindi wa pili; au
- kuingizwa kwenye blogu itakayotangaza na kuinua zaidi kazi yako ya elimu ya afya kwa jamii kwenye tovuti ya Hesperian Health Guides-zawadi ya mshindi wa tatu.
Machapisho yote ambayo yatafuzu yatatangazwa na kufikishwa kwa watu wengi zaidi kupitia hebu ya Kiswahili katika Tovuti ya Shirika la Hesperian Health Guides (www.hesperian.org)
Machapisho yatakayoshinda yatakidhi kwa hali ya juu vigezo vyote vitatu vifuatavyo:
1.Ujumbe: je chapisho limebeba ujumbe muhimu kuhusu afya , limetumia taarifa sahihi na zinazoenda na wakati ?
2. Matumizi na ufikikaji: je chapisho linatumika miongoni mwa jamii zenye kuongea Kiswahili ? Ni muhimu, linaeleweka, taarifa zake ni wazi, na rafiki kwa mtumiaji-mfanyakazi wa afya wa ngazi ya jamii au mtumiaji mwingine katika ngazi ya jamii?
3.Upatikanaji wake bila masharti-je ni kazi halali ambayo haijaghushiwa, na ambayo ipo wazi kwa ajili ya matumizi,marekebisho (ili kukidhi mahitaji), kuchapishwa tena na kusambazwa kwa jamii bila kikwazo chochote AU kwa idhini na kukiri chanzo tu ?.
Tuma chapisho lako kwa barua pepe kwa anuani hii: share@hesperian.org
Tumia kichwa cha barua : Shindano la Machapisho ya Kiafya katika Kiswahili.