Mwezi wa 12 chuyodo iliweza kupata mashelfu na mafunzo ya siku mbili kutoka kwa Book Aid International kupitia mradi uliobwa na mjukiza ,hata hivyo tumeweza kusambaza barua za wito kwa masheha ,wabunge na wawakilshi wa shehia ya chumbuni
kutokana pia na kujishuhulisha na maktaba tumeweza kupokea vitabu vya fani mbalimbali kutoka maktaba kuu ya zanzibar ambavyo vinasaidia kwa kiasi kikubwa katika maktaba yetu.
pia tumeweza kuandika barua ya maombi katika idara ya mawasiliano na lesseni iliyipo mwanakwerekwe kwa ajili ya kuomba eneo la ardhi lililopo karibu na karakana kuu lakini kwa bahati mbaya tumekosa eneo hilo,hata hivyo tulifanya juhudi ya kuongea na mlezi wa jumuia ambae ni sheha wa shehi ana kutuambia tusubiri mpaka itakapo kamilika upitishaji wa waya za umeme unaotokea kidatu na kuangalia nafasi iliyowazi ili kupewa kwa kujengea ofisi
Vilevile vikao vya kila mwezi vimeweza kuamua kwamba tuombe kupitia mashirika ya nyumbani mfano ZANTEL,BENKkwa ajili ya kutununulia kiwanja kilichopo karibu na ofisi yetu kwa ajili ya kuboreshwa kwa jumuia yetu ambapo hadi hivi sasa tunasubibi majibu kutoka mashirika hayo
pia chuyodo imeweza kuandika mradi kipitia 'the foundation for civil sosiety' kwamara ya mwanzo kwa ajili ya kuijengea uwezo jumuia ya chuyodo ambapo hadi hivi sasa tunasubiri majibu kutoka kwao
mwezi waferbuary chuyodo iliweza kuunga uhusiano wa karibu na jumuia ya 'zanzibar youth foram iliyopo mlandege na kufanya mazungumzo mafupi katika ofisi ya chuyodo na mwenyekiti wa jumuia hiyo
mwezi huohuo chuyodo ilipata fomu ya maombi ya mafunzo kwenye shirika la FEES lililopo jijini dares salam kwa ajili ya mafunzo ya uongozi kwa muda wa mwaka mmoja ambapo mitihani ya majaribio ilifanyika umoja wa walemavu ambapo katika watu 30 kwa zanzibar walipatikana watu kumi akiwemo mwenyekiti wa chuyodoambae ni laila abdalla mansour na kutakiwa kuhudhuria mafunzo tarehe 30 na 31 katika jengo la fees upanga dares salam