Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Ilianzishwa kama klabu ya viziwi ambayo watu walikuwa wanaidharau na kusema ni machizi (vichaa)

Baadae ikaanzishwa kikundi cha viziwi likijulikana kama kikundi cha viziwi kondoa (kiviko).

Baadae CHAVITA) mkoa Dodoma walitoa mafunzo ya lugha ya Alama (L.A.T)katika tawi la wilaya ya kondoa ndipo likaanzishwa CHAMA CHA VIZIWI TANZANI (CHAVITA) TAWI LA WILAYA YA KONDOAitakuwa chin ya chavita mkoa wa Dodoma.

Ilipofika 2010,kikundi likabadili jina kuita Chama Cha Viziwi tawi la Wilaya ya Kondoa.

Ilipofika 2011 Chama kilifanya uchaguzi wake na kupata viongozi wake na wanaendelea na kazi za kutetea maslahi ya wanachama wake na kuwatafutia Elimu kwa wale waliokosa elimu ya Awali na wengine kuwapeleka vyuo vya ufundi kama veta,yombo na singida ufundi.