UWAZI NA UWAJIBIKAJI
Uwazi ni njia mojawapo inayoleta mafanikio mema katika shughuli za kimaendeleo. Lakini baadhi ya Halmashari haziko wazi kutoa taarifa mabalimbali za kimaendeleo kwa raia wake. hilli inachelewesha maendeleo katika jamii. raia wengi hawajui mapato na matumizi ya fedha za umma. Tufanyeje ili kupata taarifa za shughuli za kimaendeleo ikiwa ni pamaoja na kushirikishwa katika utengenezaji wa bajeti?
Napenda kukushukuru kwa mada yako nzuri mr Jophet A Kalegeya
kutokana na mada yako nzuri ambayo mimi inanihusu moja kwa moja kutokana shughuri zangu ninazofanya
MAJUKUMU YA SERIKALI ZA MITAA. |
|
Halmashauri za Manispaa zimeanzishwa chini ya sheria za Mamlaka za Miji (Local Government Urban Authorities Act. 1982).
hivyo kutokana na majukumu hayo si hiyari kwa kiongozi hila tatazo hata baadhi ya viongozi na wananchi awatambui kabisa wajibu wao hivyo basi jukumu la kila mtu amuelimishe kujua majukumu na ya viongozi wake na ajue umuhimu wake wa kushiriki kikamirifu katika serikali ya Mtaa wake na kudai mapato na matumizi nikisema kikamilifu maana kuna watu wao uenda tu lakini awachangii kitu chochote ili tuweze kusimamia vizuri rasilimali za uma na kuwawajibisha wale viongozi wasio kuwa na madli jukumu la viongozi kuwa na wazi na uwajibikiji ni letu wananchi kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muhungano wa Tanzania ya mwaka 1982 asante sana
|
@FIKIRI MVUGARO(MWELA THEATRE GROUP) (MTONI MTONGANI TEMEKE DSM):
Asante Sana Mr.Fikiri Mvungaro kwa mchango wako nzuri wa kutuelimisha kuu ya majukumu ya Halmashauri na uanzishwaji wake.