Envaya

Baraza kuu la waislamu wa Tanzania wilaya ya Mkuranga pamoja na kujishughulisha na masuala ya Dini ya Kiislamu lakini pia linajihusisha na utoaji huduma kwa jamii katika harakati za kuleta maendeleo kwa waumini wa dini ya kiislamu na wasiokuwa waislamu. 

Hivi karibuni tumewahi kuendesha miradi miwili, wa kwanza ambao ulianzia April 2011 na kuishia March 2012 ulihusu kuhamasiha jamii katika masuala ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na rasilimali za umma wilayani Mkuranga katika idara za maji na Kilimo.

Mradi huu ulifadhiliwa na FACILITY FOR ETHICS ACCOUNTABILITY AND TRANSPARENCY (FEAT). Tumefanya kazi katika kata 7 za wilaya ya Mkuranga ambazo ni:- Mkuranga, Tambani, Mbezi, Kitomondo, Kisiju, Mwarusembe na Bupu. Tummeweza kuendesha mafunzo kwa kamti za ufuatiliji wa matumizi ya fedha na rasilimali za umma, tumefanya mikutano ya uhamasishaji jamii kwa ajili ya kuwakumbusha wajibu wao wa kufuatilia na kusimamia miradi ya maendeleo katika vijiji, tumemeweza kuandaa mikutano ya mrejesho kwa kamati za maendeleo ya kata.

Katika mradi wa pili unaohusu COMMUNITY SUPPORT TO MOST VULNERABLE CHILDREN. Mradi huu ulikuwa ukiwakumbusha wanajamii kwamba jukumu la kuwalea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ni jukumu letu sote na hata maandiko matakatifu yana tukumbusha kutokuwabagua watoto hao kwani wanatokana miongoni mwa familia zetu, watoto hawa hawakuomba kwa mwenyezimungu wakutane na hali hiyo hapa duniani, yote ni matokeo ya sisi wenyewe binadamu hivyo ni wajibu wetu kuwela na kuwatunza watoto hawa ili na wao wajisikie na amani. Kitendo cha kuwatenga ni kusababisha ongezeko la watoto watukutu na ambao huzaa vibaka wa mitaani ambao wanakuja kutudhuru sisi wenyewe. MTOTO WA MWENZIO NI WAKO.

Tushikamane kwa pamoja tuwalee watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi, hebu fikiri hali kama hiyo ndio inawakuta watoto wako. Tuondokane na fikra potofu kwamba DUNIA YA SASA IMANI IMEKWISHA, KILA MTU ANAANGALIA LAKWAKE.

MTAZAMO HUU SIO SAHIHI