Injira
MWANZA JUNIOR COUNCIL-MJC

MWANZA JUNIOR COUNCIL-MJC

MWANZA, Tanzania

Baraza la Watoto Mkoa wa Mwanza lilianzishwa mwaka 2003 kwa dhumuni la kulinda na kutetea Haki na maslahi muhimu ya watoto. Baraza la watoto linasimamiwa na ofisi ya maendeleo ya Jamii mkoa wa Mwanza. halikadhalika Baraza la watoto linamfumo wa Uongozi ambao huanzia katika ngazi ya Kamati Kuu yenye watoto kumi (wasichana watano na wavulana watano), ndani ya kamati kuu yupo Mwenyekititi, makamu Mwenyekiti, Katibu,Muhasibu na wajumbe sita. Sifa zakuwa katika baraza la wa watoto ni Mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka kumi na nane (18).Baraza la watoto ufanya chaguzi kila baada ya miaka miwili kuanzia ngazi ya mtaa, Kata, wilaya, Mkoa na Taifa.

Tangu kuanzishwa kwa Baraza la Watoto wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2002, mkoa wa Mwanza tumeweza kushikiria nafasi ya Mwenyekiti kwa kipindi chote hadi sasa:

  1. Onesmo Mkama                   2002-2004

  2. Shaban Ramadhan               2004-2006

  3. Isaya yunge                         2006-2008

  4. Nyabuchwenza Methusela      2008-2010

  5. Sekela Richard                      2010-2012

  6. Ummy Jamaly                        2012-2014

Licha ya kushika nyazifa ya Mwenyekiti Taifa lakini pia tumeweza kushika nafasi ya katibu taifa kuanzia mwaka 2010:

  1. Jasmine Jamaly         2010-2012

  2. Charles Elisante         2012-2014