Envaya

Hawa ni viongozi wa dini ya kiislam walioshiriki katika kikao cha kupinga ukatili wa kijinsia.

Viongozi wa CCT Taifa wakitoa mafunzo ya ukatili wa kijinsia kwa Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini katika ukumbi wa Kisare tarehe 09/12/2020 wilayani Serengeti.

 

Wanawake wengi katika mkoa wa Mara hasa Serengeti wamekuwa na changamoto kubwa sana ya ukatili wa kijinsia, hivyo kupitia siku hii ya maadhimisho ya miaka 50 BAKWATA wanawake wa Kiislam wanapaza sauti zao juu ya kupinga ukatili wa jinsia 09 December 2018.

Ndani ya jamii yetu kuna watu wengi sana wanahitaji kusaidiwa ili wajikwamue katika matatizo yao hivyo sote kwa pamoja tuungane kuwasaidia wenzetu.

Maadhimisho ya Miaka 50 ya BAKWATA kimkoa yamefanyika Serengeti Mara 09 December 2018

Sheikh Juma akielezea mafanikio makubwa ya miradi ya maendeleo 09 December 2018

Katibu wa wilaya akitoa maelezo jinsi alivyosimamia mradi wa ujenzi wa vibanda 09 December 2018

Waumini wakigawa misaada kwa wagonjwa hospital ya Nyerere DDH tarehe 09 December 2018

Waumini wakijiandaa kugawa misaada kwa wagonjwa hospitali ya Nyerere DDH tarehe 09 December 2018.

Sheikh wa mkoa akitoa misaada ya vitu mbalimbali kwenye wodi ya wanawake na watoto hospitali ya Nyerere DDH tarehe 09 December 2018.