Envaya
Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Morogoro,limekamilisha zoezi la kuunda uongozi wa Wilaya katika Wilaya mpya ya Gairo. Zoezi hilo likisimamiwa na viongozi wa Mkoa akiwemo Kaimu Sheikh wa mkoa Morogoro ambae pia ni Sheikh wa mkoa wa Dodoma Ulamaa Sheikh Mustafa Shaabani, lilisimamiwa kwa mujibu kanuni za uchaguzi zilizoainishwa katika katiba ya (BAKWATA). Mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uchaguzi Katibu wa mkoa Bw.Zubeir Hamisi Majaliwa aliwataja washindi katika uchaguzi huo kuwa Sheikh wa Wilaya Gairo ni Sheikh Twaha Salehe Kilango, Mwenyekiti Shehe Makame Athumani. na Katibu wa wilaya ni Sadi Miraji Msita hata hivyo katibu huyo aliwataja wajumbe 10 wa halmashauri na watano wa Baraza la masheikh wilaya. Uchaguzi ulifanyika tarehe 29/09/2013 Ukumbi wa Alsaed Gairo Unguu-Road.
23 Ugushyingo, 2013
Ahakurikira »

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.