Envaya

                              

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

        

Taarifa ya Shughuli za Mradi Robo Mwaka

 

Sehemu ya 1.Utangulizi

A.Jina Kamili la Asasi-Kama lilivyo kwenye Mkataba wenu na Foundation for civil Society

 

BANTU COMMUNITY DEVELOPMENT CENTRE

 

B.Jina linalotumika mara kwa mara-Jina lolote au kifupi cha jina ambalo hutumika kuelezea Asasi

 

BACODECE

 

C.Jina la Mradi-Kama ilivyo kwenye mkataba

IJUE KATIBA NA HAKI YAKO

 

 

D. Namba ya Mradi-FCS xxx kama ilivyo kwenye mkataba

FCS/RSG/1/12/154

 

 

E.Kipindi cha Utekelezaji wa Mradi Kinachoripotiwa-Eleza tarehe nakipindi cha robo mwaka ambacho taarifa hii inatolea maelezo.Mfano kama mradi wako ulianza aaaaaaaaaAgost 12,2010 kipindi cha utekelezaji kinachoripotiwa ni kutoka Agosti 12 hadi Novemba 111,2010 kipindi cha utekelezeji kinachofuata ni kuanzia Novemba 12 hadi 11 Februari,2011.Kamamradi wako ulianza Agosti 12,2010 na ni wa miaka miwili taarifa ya mwisho wa mwaka inahusisha vipindi vinne 4 vya utekelezaji kutoka Agost 12,2010 hadi Agost 11,2011

 

Tarehe

AUGUST-OCTOBER

 

F.Mratibu wa Mradi;Andika Jina kamili na anwani ya Mratibu anayesimamia mradi

 

CLEOPHAS MANGU

 

Sehemu ya 2. Maelezo ya Mradi

A. Mradi wenu uko kwenye Eneo gani muimu linalofadhiliwa na the Foundation?Kama ilivyoandikwa kwenye kipengele 1.2 cha fomuya ruzuku

                                                                                                                                   

 

1)Sera

                                     

 

 

2. Uimarishaji

   Asasi za Kiraia

 

3.Utawaka bora

Na uwajibikwji    

ü  

 

 

B.Eleza kwa kifupi mradi wenu unakidhi namna gani malengo ya eneo muhimu ulilolichagua hapo juu.

 

 

Mradi wa katiba unakidhi kwa kiasi kikubwa katika kata ya luale kwani jamii ya Luale haina fursa ya kufikiwa kirahisi kwa sababu ya hali za barabara, pia ni jamii ambayo bado haina ufahamu wa umuhimu wa katiba, mradi umeamsha hari na uwelewa wa naman ya kusoma katiba, hivyo luale wameelewa katiba na umuhimu wa kushiriki katika mchakato wa uandishi wa katiba mpya.

Pia mradi umewapatia ufahamu wa haki yao ya umiliki wa katiba na umuhimu wa kuzitambua haki zao zote za kikatiba ambazo awali hawakuzitambua wala hawakutambua umuhimu wa katiba kwao na kuona kama chombo cha viongozi pekee.

 

 

 

Figure 1 HATIMAYE LUALE WAPATIWA ELIMU YA KATIBA NA HAKI ZAO KIKATIBA NA KUTAMBUA MAANA NA UMUHIMU WA KATIBA KWAO

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Figure 2 MMOJA WA WASHIRIKI AKIWASILISHA MADA KATIKA MAFUNZO YA KATIBA NA HAKI YAKO LUALE TAREHE 7/9/2012

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

C.Taja maeneo{Mkoa,Wilaya,Kata naVijiji}ambavyo mradi wenu utatekelezwa na idadi ya watu watakaonufaika

Na   Mkoa         Wilaya                           Kata                 Vijiji         Idadi ya wanufaikaji

1

 

 

 

2

Morogoro

 

 

 

Morogoro

Mvomero

 

 

 

municipality

Luale

 

 

 

Uwanja wa Taifa

Kododo,

Londo

Luale

Masalawe

ukutu

224

 

 

 

19

 

 

 

 

 

 

 

Figure 3: ENEO LA MRADI WASHIRIKI WAKIPATA CHAKULA WAKATI WA PUMZIKO

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sehemu ya 3.Shughuli na matokeo ya Mradi kwa kipindi hiki cha Utekelezaji       

Matokeo ya Awali yalivyo kwenye kiambatanisho E cha Mkataba.

 

 

 

                           

Shughuli zilizopangwa kutekelezwa katika kipindi hiki cha utekelezaji kama ilivyo kwenye Mkataba.

Mafanikio {Eleza nini kilifanyika,wapi,lini,kwa watu gani,idadi yao na masuala yaliyoshughulikiwa wakati wa utekelezaji wa shughuli}

Kama kuna tofauti zozote ni kwa sababu gani?

Rasilimali{Eleza kiasi gani cha fedha kilitumika kwa kila shughuli}

1.1.Wanachama wa Asasi ya BACODECE 19 wamepatiwa mafunzo juu ya katiba na haki zao kikatiba ifikapo september 2012.

 

 

 

 

 

2.1. Viongozi, watendaji wa serikali na wananchi (24) katika kata ya luale wilaya ya Mvomero wamepatiwa Elimu juu ya ufahamu wa katiba na haki zao kikatiba ifikapo septemba 2012

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

3.1. Kuongezeka kwa ushiriki wa wananchi katika utoaji wa maoni juu ya katiba mpya ili kuboresha utendaji na kutimiza wajibu wao kikatiba

 

 

 

 

 

 

 

 

 

4.1.Mafanikio, changamoto za mradi zimekusanywa, kujadiliwa ili kuzitafutia ufumbuzi na kuziwasilisha kwa wadua wa mradi ifikapo mwisho wa mradi

 

 

 

 

 

5.Gharama za uendeshaji na utawala

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

1.Kuendesha mafunzo ya siku 3 juu ya Elimu ya uraia na haki za raia kikatiba, washiriki ni wanachama wa Asasi 19

 

 

 

 

 

 

 

 

2. .Kuendesha mafunzo ya siku 3 juu ya Elimu ya uraia na Haki za Raia kikatiba, washiriki ni viongozi, watendaji wa serikali na wananchi (24) wa ngazi ya kata ya luale, vijijivya luale, kododo, londo na masalawe

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

3.Kuendesha warsha ya siku moja kwa viongozi wa vijiji,vitongoji,kata na wananchi 200) wa kata Luale wilaya ya mvomero kupima ueledi wao juu ya katiba, haki za kiraia,utawala bora na mrejesho wa mafunzo ya awali (200)

 

 

 

 

Ufuatiliaji na tathmini ya shughuli za mradi umefanyika baada ya mafunzo na kwa washiriki wasio wa moja kwa moja ili kupima mrejesho wa mafunzo kwa kutumia dodoso, uchunguzi, mdahalo na maswali ya moja kwa moja

 

 

 

Shughuli zote za uendeshaji na utawala zimefanyika ili kukidhi lengo mahususi la mradi kama ilivyopangwa na kuratibu shughuli zote kama zilivyopangwa katika kipindi cha utekelezaji wa mradi

1.Mafunzo yametolewa siku tatu (3) kwa wanachama wa Asasi 19, mafunzo yalihusu maana ya katiba misingi ya katiba,nguzo za katiba bora, umiliki wa katiba kwa raia, umuhimu wa katiba, kupitia vipengele mbalimbali vya katiba na ustahili wa haki na utawala bora.

 

 

 

 

2. mafunzo ya siku 3 yametolewa kwa viongozi, watendaji wa serikali na wananchi (24) wa kata ya luale na vijiji vinne, mafunzo yalihusu maana ya katiba misingi ya katiba,nguzo za katiba bora, umiliki wa katiba kwa raia, umuhimu wa katiba, kupitia vipengele mbalimbali vya katiba na ustahili wa haki na utawala bora.

 

 

 

 

 

 

 

 

3.Mdahalo wa siku moja umeendesha katika kata ya luale vijiji vya kododo,luale, masalawe na londo, washiriki viongozi wa vitongoji, vijiji, kata na wananchi wa kata ya Luale Wilaya ya Mvomero kupima ueledi wao juu ya haki za kikatiba, haki za kiraia, utawala bora na mrejesho wa mafunzo ya ndani

 

 

 

 

Watathmini wawili walitembelea eneo la mradi kukusanya dodoso la maswali na kuchunguza mrejesho wa mafunzo kwa kuuliza maswali ya moja kwa moja na kufanya mijadala na vikundi vya walengwa wa nje

 

 

 

 

 

 

Malipo ya pango yalifanywa kwa miezi mitatu yote, vifaa vya ofisi vilinunuliwa,posho la uratibu na uhasibu zimeripwa kwa mratibu na mhasibu wa mradi, pia ukarabati wa jengo la ofisi umefanyika

1.Hakuna tofauti yoyote katka shughuli zilizopangwa

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2. Tofauti za majina ya vijiji kwasababu ya kugawanywa kwa kata na vijiji baadhi kuhamishiwa kata ya kikeo badala ya Luale. Pia wanachama kuhitaji kutengenezewa vyeti vya uthibitisho wa kuhitimu mafunzo

 

 

 

3.Tofauti ya idadi ya washiriki mdahalo waliotarajiwa 200 waliohudhuria 183 kwasababu ya umbali wa baadhi ya vijiji kutika makao makuu ya kata na ubovu wa barabara

 

 

Hakunatofauti, Taarifa za mafanikio na changamoto zimekusanywa

na kufanikiwa kuzifanyia uchambuzi ili kupata ufumbuzi wa changamoto

 

 

 

Tofauti ilitokea kwasababu ya ongezeko la gharama za ukarabati na taratibu za kiserikali za kutambulisha mradi na kufanya mawasiliano ili kupata kibali cha kuanza utekelezaji wa mradi.Tulikabiliana na changamoto hizo kwa kutumia fedha za michango ya wanachama

1. 1,833,050

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2.2,015,100

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

3.1,300,000

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

4.454,400

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

5. 1,646,500

 

 

 

 

 

 

SEHEMU YA 4. Mafanikio au Matunda ya Mradi

  1. Matokeoya mabadiliko ya muda mfupi yaliyotarajiwa kama yalivyo kwenye kiambatanisho E.
  2. Mkataba

Mabadiliko yaliyoletwa na mradi

Mabadiliko mengine yoyote yanayotokana na utekelezaji wa shughuli za mradi huu

Sababu za tofauti ya mabadiliko kama zipo

 

1.1  Wanachama wa asasi ya BACODECE 19 wamepatiwa mafunzo juu ya katiba na haki zao kikatiba ifikapo septemba 2012

 

 

 

 

 

 

 

2.1. viongozi na watendaji wa kata ya luale wilaya ya mvomero wamepatiwa elimu juu ya katiba na haki zao kikatiba ifikapo septemba 2012

 

 

 

 

 

 

3.1. kuongezeka kwa ushiriki wa wananchi katika utoaji wa maoni juu ya katiba mpya ili kuboresha utendaji na kutimiza wajibu wao kikatiba ifikapo septemba 2012

 

 

 

 

1.1Wastani mkubwa wa wanachama wa asasi wanaonesha uelewa wa vipengele vya katiba na haki zao kikatiba

 

1.2 Pia kiwango cha ushiriki wa wanachama katika mchakato wa katiba mpya kimeongezeka sana

 

2.1. wastani wa viongozi, watendaji na wananchi wa kata wanaonesha uelewa wa katiba kwa asilimia 100 ya viongozi na watendaji na   93% ya wananchi wa kata ya luale walengwa mahususi wa mdahalo

 

 

3.1. wastani wa wananchi wanaonesha uelewa wa vipengele vya katiba haki zao kikatiba katika kata ya Luale kwa 93% na hamasa ya usomaji wa katiba imeongezeka baada ya mafunzo

 

Pia kiwango cha ushiriki wa wananchi katika mchakato wa katiba mpya kimeongezeka

Hivi sasa wanachama wengi wanafahamu vipengele vya katiba ya nchi nahaki zaokikatiba

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Hivi sasa wananchi wengi wanafahamu baadhi ya vipengele vya katiba na namna ya kusoma katiba ya nchi ili kujua haki zao za kikatiba

 

 

 

 

 

Kwa sasa wananchi wengi wanafahamu vipengele baadhi vya katiba ya nchi na haki zao kikatiba

Ushiriki wa wanachama katika mafunzo ya katiba na haki yaliyowapa fursa ya kujadili vipengele mbalimbali vya katiba na kupendekeza (maoni) mabadiliko mbalimbali ya baadhi ya vipengele vya katiba

 

 

 

 

 

 

 

Hamasa ya ushiriki ilikuwa kubwa katika mafunzo ya katiba na haki yako na uchangiaji wa maoni tufanye ninikatika mchakato wa katiba mpya

 

 

 

 

 

 

 

Kupata mafunzo katiba na haki zao kama washiriki wa moja kwa moja na wengine kama washiriki wasio wa moja kwa moja kupitia washiriki wa moja kwa moja, pia ushiriki katika mdahalo wa katiba na haki ambao ulikuza hamasa ya usomaji katiba na kupima uwezo wa kuchangia moni ya katiba mpya.

 

Sehemu ya 5. Mambo mliyojifunza ( Eleza Uzoefu na Mawazo yoyote mapya mliyoyapata kutokana na kutekeleza shughuli za mradi huu

 

1.

 

Kunahuhitaji mkubwa sana wa mafunzo endelevu na mijadala ya katiba na elimu ya uraia kwa wananchi ili kuendelea kukuza uelewa wa katiba na haki za raia kikatiba kwa sababu mradi huu umeamsha hari ya usomaji wa katiba ingawa kumekuwa na changamoto ya upatikaji wa katiba kwa wananchi wengi na watu wa kuendelea kuwahamasisha kujadiliana katiba katika makundi

2.

Tumegundua kuna migogoro mingi na uvunjifu wa sheria kwa kiasi kikubwa unasababishwa na uelewa mdogo wa katiba ya nchi na haki za raia ndani ya nchi yao

 

3.

Pia tumegundua kuwa viongozi wengi hutumia mianya ya uelewa mdogo wa raia kuhusu katiba na taratibu mbalimbali za nchi kama daraja lao la kuendelea kuwa madarakani na kuwa na matumizi mabaya ya madaraka na hasa kwa kuminya haki za raia ambazo wananchi hawazijui

 

4.

Vilevile katika kipindi cha utekelezaji wa mradi wa ijue katiba na haki yako tumegundua tofauti kubwa ya matumizi ya rasilimali za nchi kati ya mijini na vijijini kwani viijini hawapati mgawanyo uliosawa wa rasilimali za nchi kwa sababu ya kutojua haki zao kikataiba mfano katika elimu kuna shida kubwa ya vitendea kazi na walimu vijijini kiasi cha kutumia wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kusaidia kufundisha shule za msingi. Hivyo kuwafanya waikose haki sawa ya kupata elimu

 

5.

Pamoja na yote kumekuwa na fursa chache za ushiriki wa watendaji wa kata na vijiji katika Semina,Warsha na Makongamano kwa kiasi cha kuwafanya wawe na mtazamo finyu sana katika utekelezaji wa majukumu yao ya kiutendaji hasa watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji

 

6.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

              

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sehemu ya 6.

Chagamoto na nmana mlivyokabiliana nazo ( Eleza masuala yalichangia katika kutofikia malengo ya utekelezaji wa shughuli na namna mlivykabiliana nayo

 

Na

Changamoto

Na

Namna mlivyokabilana nazo

 

1.

Taratibu za kiseikali ziliongeza gharama za Nauli na mawasiliano na mara nyingine kulazimika kufuata Ratiba za viongozi na watendaji wa serikali

 

1.

Tulitafuta tumia michango ya wanachama kwa gharama zilizotokana na taratibu za kiserikali kama kutambulisha mradi na kuendelea kufuatilia ruhusa ya kuendelea na shughuli za mradi

2.

Uduni wa miundo mbinu ya barabara na upatikanaji wa maradhi katika eneo la mradi

2.

Wawezeshaji walilazimika kukodi pikipiki kwa sababu usafiri eneo la mradi ni shida , pia wawezeshaji walilazimika kwenda na kurudi mjini wakati wa kutekeleza shughuli za mradi kwasababu ya ukosefu wa sehemu ya maradhi katika eneo la mradi

3.

Muingiliano wa shughuli za watendaji, sensa na shughuli za mradi

3.

Mratibu alilazimika kubadili ratiba ya mafunzo ili kupata ushiriki mzuri wa walengwa

4.

Mivutano ya kisiasa na maslahi ya wanasiasa yaliwagawa walengwa hasa katika mdahalo

4.

mwezeshaji alilazimika kutumia muda mwingi kuwarudisha washiriki kwenye mada ya katiba na haki yao na kuwaasa kuacha kuongozwa na mitazamo ya kisiasa

5.

Ufuatiliaji ulikuwa mgumu kwa sababu wengi wa washiriki walikuwa na shida katika kusoma na kujibu maswali kwa ueledi

5.

Watathmini walilazimika kutumia maswali ya wazi kuliko ya maelezo

6.

 

6.

 

7.

 

7.

 

 

 

Sehemu ya 7.

Mahusiano na wadau wengine. (Eleza namna mlivyoshirikiana na wadau kama Serikali, Asasi nyingine zinazofanya kazi kama yenu wakati wa utekelezaji wa shughuli)

 

Asasi                                                                                                                                              Namna Mlivyoshirikiana nayo

Halmashauri ya wilaya ya mvomero

 

 

1.

Kutambulisha mradi na kuomba ushirikiano toka kwa mkurugenzi na afisa maendeleo wa wilaya ya mvomero.pia nao walishirikiana nasi kwa kututambulisha katika eneo la mradi kata ya Luale, Mvomero

 

Umoja wa Azaki morogoro (UNGO)

 

 

 

2.

Kwa kutoa mchango wa mawazo namna nzuri ya kutekeleza mradi kwa ufanisi na kutushirikisha katika warsha na midahalo mbalimbali kuhusu katiba mpya

Asasi nyingine za kirai kama HURUMA AIDS CONCERN AND CARE (HACOCA)

 

 

 

 

3.

Kupata ushauri wa kitaalam mbinu nzuri ya kufanya ufuatiliaji na tathmini na mshiriki mmoja kuhudhuria mafunzo ya katiba kwa siku 3 ya wanachama wa Asasi

 

 

 

 

 

4.

 

 

 

 

 

 

5.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sehemu ya 8: Mipango ya Baadae

Shughuli gani zimepangwa kwa ajili ya kipindi kijacho cha utoaji wa taarifa? Taja shughuli mlizopanga kutekeleza mwaka ujao

 

Kwakuwa mradi wa Ijue katiba na Haki yako ni wa miezi mitatu ya utekelezaji hivyo tunakipindi kimoja tu cha utekelezaji.

Ingawa mipango yetu ya baadae ni Kuendelea kuhamasisha jamii kusoma katiba na kushirikishana katika kutambua haki zao kwa kutumia walengwa wa moja kwa moja kuwafundisha wenzao na tumewahamasisha viongozi, watendaji na wananchi waliopatiwa mafunzo ya ndani (moja kwa moja ) kuendelea kujadiliana na wenzao katika makundi ili elimu ya katiba iendelee kuwafikia wananchi wengi.

 

Mwezi wa 1

 

Mwezi wa 2

 

Mwezi wa 3

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sehemu ya 9.

Walengwa waliofikiwa (Taja walengwa wa moja kwa moja yaani watu walioshiriki moja kwa moja kwenye shughuli za mradi na wale mliowafikia kupitia walengwa wa moja kwa moja au ambao hawatafikiwa moja kwa moja na shughuli za mradi. Kama wanufaika hao hao wanafikiwa na shughuli zaidi ya moja wahesabu mara moja tu

Kuendesha mafunzo ya siku tatu juu ya elimu ya uraia na haki za kikatiba, washiriki ni wanachama wa asasi 19

 

 

 

 

 

Shughuli ya 1.  

Idadi kamili ya wanufaika

 

 

Walengwa wa moja kwa moja

 

 

Jumla

 

Walengwawasio wa moja kwa moja

 

 

Jumla

Wajane na Wagane

Wanaume

1

1

 

0

0

Wanawake

 

 

0

Watu wanaoishi na VVU/ UKIMWI

Wanaume

0

0

 

0

0

Wanawake

0

 

0

 

Wazee

Wanaume

3

3

 

1

1

Wanawake

0

 

1

 

Watoto yatima

Wanaume

0

0

 

0

0

Wanawake

0

 

0

 

Watoto

Wanaume

0

0

 

0

1

Wanawake

0

 

1

Watu wenye ulemevu

Wanaume

0

0

 

0

0

Wanawake

0

 

0

 

Vijana

Wanaume

9

17

 

6

8

Wanawake

8

 

2

 

Watu wengine

Wanaume

0

0

 

0

0

Wanawake

0

 

0

                                

 

 

 

 

                Figure 4: WANACHAMA WA ASASI WAKIJADILI VIPENGELE VYA KATIBA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kuendesha mafunzo ya siku tatu juu ya elimu ya uraia na haki za rai kikatiba , washiriki viongozi wa ngazi ya kata Luale, vijiji vya luale kododo, londo, na    

 

 

Shughuli ya 2.

 

 

 

 

Idadi kamili ya wanufaika

 

 

Walengwa wa moja kwa moja

 

 

Jumla

 

Walengwawasio wa moja kwa moja

 

 

Jumla

Wajane na Wagane

Wanaume

0

0

wanaume

0

1

Wanawake

0

wanawake

1

Watu wanaoishi na VVU/UKIMWI

Wanaume

0

0

 

0

0

Wanawake

0

 

0

 

Wazee

Wanaume

12

15

 

16

24

Wanawake

3

 

8

 

Watoto yatima

Wanaume

0

1

 

2

3

Wanawake

1

 

1

Watoto

Wanaume

0

1

 

5

6

Wanawake

1

 

1

Watu wenye ulemevu

Wanaume

1

1

 

0

0

Wanawake

0

 

0

 

Vijana

Wanaume

7

10

 

41

87

Wanawake

3

 

26

 

Watu wengine

Wanaume

0

 

 

0

0

Wanawake

0

 

0

 

Figure 5 WASHIRIKI WA MAFUNZO WAKIJADILIANA KUHUSU VIPENGELE VYA KATIBA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kuandaa na kuendesha mdahalo ngazi ya kata washiriki wanajamii 200 ili kupima uelewa na mrejesho waa mafunzo yaliyotolewa kwa viongozi ngazi ya kata na uwezo wao wa kutoa maoni juu ya haki zao kikatiba

 

 

 

Shughuli ya 3

 

 

Idadi kamili ya wanufaika

 

 

Walengwa wa moja kwa moja

 

 

Jumla

 

Walengwawasio wa moja kwa moja

 

 

Jumla

Wajane na Wagane

Wanaume

2

7

 

 

 

Wanawake

5

 

 

Watu wanaoishi na VVU/UKIMWI

Wanaume

0

0

 

 

 

Wanawake

0

 

 

 

Wazee

Wanaume

13

16

 

 

 

Wanawake

3

 

 

 

Watoto yatima

Wanaume

0

0

 

 

 

Wanawake

0

 

 

Watoto

Wanaume

24

100

 

 

 

Wanawake

76

 

 

Watu wenye ulemevu

Wanaume

2

2

 

 

 

Wanawake

0

 

 

 

Vijana

Wanaume

17

24

 

 

 

Wanawake

7

 

 

 

Watu wengine

Wanaume

0

0

 

 

 

Wanawake

0

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Ufuatiliaji na Tathmini

 

 

Shughuli ya 4.

 

 

Idadi kamili ya wanufaika

 

 

Walengwa wa moja kwa moja

 

 

Jumla

 

Walengwa wasio wa moja kwa moja

 

 

Jumla

Wajane na Wagane

Wanaume

0

0

 

0

0

Wanawake

0

 

0

Watu wanaoishina VVU/UKIMWI

Wanaume

0

0

 

0

0

Wanawake

0

 

0

 

Wazee

Wanaume

12

16

 

7

12

Wanawake

4

 

5

 

Watoto yatima

Wanaume

0

0

 

0

0

Wanawake

0

 

0

Watoto

Wanaume

0

1

 

12

18

Wanawake

1

 

6

Watu wenye ulemevu

Wanaume

0

 

 

0

0

Wanawake

0

 

0

 

Vijana                                                               

Wanaume

6

8

 

7

11

Wanawake

2

 

4

 

Watu wengine

Wanaume

0

0

 

0

0

Wanawake

0

 

0

 

                                                                                                                                              

SEHEMU YA 10.

 

Eleza kama Asasi yako imewahi kuhudhuria shughuli ambazo zimeandaliwa na The Foundation. Chagua kutokakwenye orodha hapo chini

 

Aina ya Shughuli/Tukio

Lini

Mambo ulioyojifunza

Hatua zilizochukuliwa

1.MAFUNZO YA USIMAMIZI WA RUZUKU

21 HADI 25, MAI,2012

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Usimamizi wa Ruzuku, Mikataba, Uandish wa Mradi, Uandishi wa Taarifa na tathmini ya Utekelezaji na ya Fedha.

Taasisi iliingia mkataba na the foundation for civil society kutkeleza mradi wa ijue katiba na haki yako kwa miezi mitatu

 

 

Chagua:

 

Aina ya TUKIO

****** Mafunzo ya usimamizi wa Ruzuku (MYG)

 

******Mafunzo mengine yoyote (taja aina ya mafunzo mf. Ufuatiliaji na thathimini)

 

******Warsha ya kupashana habari

 

******Tamasha la Asasi za Kiraia

 

Viambatanisho :-

  1. Maelezo ya mafanikio ya shughuli /mradi
  2. Taarifa yamafunzo n.k.        

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

MAFANIKIO NA CHANGAMOTO

 

MAFANIKIO

 

1.1.WANACHAMA WA ASASI YA BACODECE WABORESHA OFISI KWA UFADHILI WA

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

 

 

 

 

                                    

 

Figure 6     WANACHAMA WAKIPAKA RANGI JENGO LA OFISI

 

 

 

 

                            

 

 

 

Figure 7: OFISI YA BACODECE KABLA YA UFADHIRI WA FCS

 

 

 

 

Figure 8: JENGO LA OFISI YA BACODECE KABLA YA UKARABATI KWA UFADHIRI WA FCS

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2.1.LUALE WAPATA UFAHAMU WA VIPENGELE VYA KATIBA

 

 

Figure 9: MHESHIMIWA DIWANI KATA YA LUALE AKIHIMIZA UMUHIMI WA MAFUNZO YA KATIBA KWA WANA LUALE

 

 

 

 

Figure 10: WANA BACODECE LUALE WAPATIWA KATIBA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

3.1 WANA LUALE WAPATA SAUTI YA KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA

 

 

 

 

Figure 11: WASHIRIKI WA MDAHALO WAKIULIZA VIPENGELE VYA KATIBA NA KUTOA MAONI YAO KUHUSU KATIBA MPYA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Figure 12: MWANA LUALE AKICHANGIA MADA YA KATIBA NA HAKI YAKO

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

TAARIFA YA MAAFUNZO YA IJUE KATIBA NA HAKI YAKO YALIYOTOLEWA KWA WANACHAMA WA ASASI – BACODECE   TAREHE 28 – 29/2012 UKUMBI WA CCM VIJANA SOCIAL MOROGORO

 

 

DONDOO ZA MAFUNZO:

SIKU YA KWANZA :

1: KUWASILI NA KUJITAMBULISHA KWA WAJUMBE.

2: KUFUNGUA MAFUNZO.

3: MAFUNZO:-

(a)  MADA YA KWANZA: KATIBA NA HAKI

(b)  MADA YA PILI: MAMBO MUHIMU KATIKA UANDISHI WA KATIBA

(c)  MADA YA TATU: MISINGI NA NGUZO ZA KATIBA BORA

(d)  MADA YA NNE: MAUDHUI YA KATIBA

 

SIKU YA PILI

1: UTANGULIZI: MREJESHO WA MAFUNZO.

2: MAFUNZO

(a)  MADA YA KWANZA : MAJADILIANO - SURA YA 2 YA KATIBA KUHUSU RAISI

     (b) MADA YA PILI: HAKI

     (c) MADA YA TATU: UTAWALA BORA.

3: MENGINEYO:

(a)  TUFANYE NINI

(b)  TATHIMINI YA MAFUNZO

4: KUAHIRISHA MAFUNZO:

 

SIKU YA KWANZA:

1: KUWASILI NA KUJITAMBULISHA KWA WAJUMBE.

Wajumbe waliwasili muda uliyopangwa mnamo saa 3:00 na kulifuatiwa na utambulisho uliofanyika kwa kila mjumbe

2: KUFUNGUA MAFUNZO

Mratibu mradi alimkaribisha mwenyekiti wa bodi ili kufungua mafunzo mnamo saa 3:15, mwenyekiti aliwataka washiriki wote kuzingatia mafunzo.yatakayotolewa na wawezeshaji kwa ajili ya suala zima la mchakato wa katiba lililoko mbele yetu na wajue kuwa wao ndio watakuwa chachu ya kupeleka elimu ya katiba

3: MAFUNZO:

(a)  MADA YA KWANZA: KATIBA NA HAKI

(i)            MAJADILIANO: MAANA YA KATIBA NA HAKI.

Mwezeshaji alimtaka kila mmoja wa washiriki kujadiliana maana ya Katiba na maana ya Haki ili kupima uelewa wa washiriki kwa mada husika. Mawasilisho ya makundi yote yalikuwa kama ifuatavyo:-

Katiba ni mwongozo wa sheria wa jumuia fulani,

Katiba ni sheria mama, ni kiongozi au kielezi,

Katiba ni mawazo ya pamoja,      

Katiba ni sheria nakanuni muhimu,

 

 

Figure 13 MICHANGO MBALIMBALI YA WANACHAMA WA ASASI KUHUSU MAANA YA KATIBA

 

 

 

 

(ii)          Haki ni hali ya kutendewa pasipo shuruti,

Haki ni thamani ya utu,

Haki ni stahili kitu chochote utakachopata kwa mujibu wa sheria,

Haki ustahili wa kutendewa au kupewa,

 

HISTORIA YA KATIBA:

Mwezeshaji alituongoza washiriki kupitia vitini tulivyogawiwa kuhusu Historia ya Katiba

1961- Iliundwa katika ya Uhuru,

1962- Iliundwa katiba ya katiba ya Jamhuri,

1964- Iliundwa katiba ya Tanzania,

1977- Iliundwa katiba ya Kudumu,

MABADILIKO 14 YA KATIBA:

1979- Mabadiliko ya Kuanzisha Mahakama ya Rufaa,

1980- Mabadiliko ya kujibu kero za Muungano,

1980- Mabadiliko ya kuweka sawa Mfumo wa Uchaguzi wa Raisi wa Zanzibari, serikali ya mapinduzi na muundo wa baraza la wawakilishi,                                                                                                                                    

1982- Mabadiliko ya kuonyesha utaratibu wa uteuzi wa wakuu wa mikoa

1984- Mabadiliko ya kuingiza tamko la Haki za Binadamu,

1990- Mabadiliko ya kuanzisha Tume ya Uchaguzi,

1990- Mabadiliko ya utaratibu wa kupata Mgombea,

1992- Mabadiliko ya kufuta rasmi mfumo wa chama kimoja na kuweka mfumo wa vyama vingi,

1993- Mabadiliko ya kuweka uchaguzi wa pamoja Raisi, Wabunge na Madiwani,

1994- Mabadiliko ya kuweka mfumo wa mgombea mwenza,

1995- Mabadiliko ya kuweka kiapo cha Raisi, makamu wake, waziri mkuu na Raisi wa Zanzibar, kulinda muungano na kikomo cha Urais.

2000- Mabadiliko ya kumpa Rais uwezo wa kuteua watanzania 10 kuwa wabunge na kuondoa kigezo cha 51% kuwa Rais.

2005- Mabadiliko ya kuongeza viti maalum toka 20% hadi 30%, uhuru wa kuabudu, kushiriki maoni na kujieleza.

Baada ya majadiliano wajumbe kwa pamoja tumekubaliana kuwa katiba lazima ibadilishwe kwa sababu haijitoshelezi wakati wote kwani:-

  • Mabadiliko ya vizazi na mazingira.
  • Ukuwaji wa elimu na teknolojia,
  • Msukumo wa mataifa ya nje,
  • Kukua kwa uchumi na mabadiliko ya tabia nchi,
  • Kuwa na mahitaji yanayo fanana,
  • Uhitaji wajamii kwa wakati huo.
  •  

(b)  MADA YA PILI: MAMBO MUHIMU KATIKA UANDISHI WA KATIBA:

Mwezeshaji alituongoza na kutupitia mambo muhimu katika uandishi wa Katiba kama ifuatavyo:-

  • Usawa wa washiriki.
  • Uhuru na haki ya kukubali mapendekezo yote na mengine baadhi kuyakataa.
  • Kuacha ushabiki wa siasa na itikadi za dini.
  • Kuondoa mipaka ya kuhoji.
  • Katiba huandikwa na wananchi kwa ajili yao na nchi yao, wakiainisha jinsi wanavyotaka kujitawala.
  • Kuainisha muundo wa nchi.
  • Haki na wajibu wa raia.
  • Kikomo na nguvu za madaraka.
  • Misingi mikuu ya nchi

 

 

 

 

UMILIKI WA KATIBA

Washiriki wamebaini kuwa ktaba ni mali ya wananchi wa nchi husika hivyo tuwe na uwezo na mamlaka ya kuwawajibisha tuliowachagua, hapo katiba itakuwa miliki yetu.

 

(c)  MADA YA TATU: MISINGI NA NGUZO ZA KATIBA:

MAJADILIANO:

Katika mada hii mwezeshaji alitoa swali lijibiwe kupitia majadiliano katika makundi kama ifuatavyo:-

(i)“Je misingi ya katiba inatekelezeka”? Kama ndio kivipi”? Iwapo ni hapana tufanye nini?

Katika majumuisho ya makundi yote imebainika kuwa HAPANA, misingi ya katiba haitekelezwi. Haitekelezwi kwa sababu katiba inaelezea misingi ya kijamaa,utekelezaji/ utendaji wa kibepari, mf. Sera ya ubinafsishaji na mfumo wa vyama vingi siyo sera za kijamaa.Tuhakikishe kuwa misingi yote iliyoko katika katiba inatekelezwa kwa vitendo maana misingi hii ndio nguzo ya mshikamano na utulivu wa wananchi.

Baada ya ufafanuzi na majadiliano ya kina,na mwezeshaji imebainika kuwa Katiba ya Jamhuri imeainisha kuwa misingi mikuu ni Haki,Uhuru,Udugu,Amini ,Demokrasia, kutofungamana na Dini.

(ii)Washiriki kwa kuongozwa na mwezeshaji tulipitia na kujadili Nguzo za Katiba bora kama ilivyoonyeshwa ni:-

  • Demokrasia
  • Mamlaka kwa wananchi ( raia )
  • Kutatua matatizo ya wananchi.
  • Itokane na Historia ya nchi husika.
  • Iwezeshe wananchi/raia kumiliki raslimali za taifa.
  • Iwe hairuhusu ubaguzi wowote kwa raia.
  • Lazima iwe ni sheria mama.

(iii) “Tufanye nini kupata katiba bora”?

Baada ya majadiliano kupitia makundi tuliona kwamba ili kupata katiba bora lazima:-

  • Kushirikisha makundi yote ya kijamii katika mjadala wa katiba.
  • Kuheshimu mawazo ya kila mtu katika ushiriki wa maoni ya kujadili muundo wa katiba mpya.
  • Kuwa na mfumo mzuri wa kukusanya maoni.
  • Kutambua changamoto zilizopo kwa wakati huu ( mahitaji ya msingi).
  • Wananchi kuwa na nguvu ya maamuzi yakujitegemea kwa maslahi ya wananchi wote.

Mwezeshaji alitoa maswali na kuwataka washiriki kusoma maeleza yaliyotolewa kwenye baadhi ya vifunbu vya katiba ili yajibiwe kwa njia ya majadiliano kwenye makundi yetu:-

(i)”Mamlaka ya wananchi hayajafafanuliwa nini kifanyike? Toa maoni.

Washiriki tumetoa maoni kuwa mamlaka ya wananchi yamekasimiwa kwa viongozi na watendaji wa serikali,katiba inatuambia kuwa serikali inapaswa kuwajibika kwa wananchi.Elimu itolewe ili kila raia ajue mamlaka aliyonayo.

(ii) Je, mamlaka ya wananchi yanaheshimika na kutumika katika nyanja zote za kisiasa,kiuchumi na kijamii? Eleza.

Mamlaka ya wananchi aiheshimiki kutokana na wananchi kutojua wajibu wao kunawafanya wasifahamu mamlaka waliyonayo.Pia kutoshiriki na kutoshirikishwa kikamilifu kwa wananchi juu ya maliasili zinazowazunguka

(iii)”Je, misingi na taratibu za serikali kuwajibika kwa wanaanchi ipo? Tufanyeje.

Baada ya majadiliano ya kina yafuatayo yaliwasilishwa:-

  • Misingi ipo ila uwajibikaji wa serikali haupo.Kwa sababu ya wananchi/raia kutotambua haki zao za msingi serikali minakuwa haiwajibiki kwa wananchi.
  • Wajibu wa serikali lazima utambulike kwa raia kwa kutolewa elimu ya uraia na kuweka misingi imara ya kufundisha elimu ya uraia.
  • Tuongeze uwajibikaji na kuonyesha uzalendo ili kuondoa udhaifu wa utekelezaji wa misingi.
  • Serkali ikishindwa kutekeleza wajibu wake iwajibishwe

(d)MADA YA NNE: MAUDHUI YA KATIBA:

Mwezeshaji alifafanua maudhui ya katiba kama ifuatavyo:-

  • Katiba ina Sura10
  • Katiba ina Ibara 152
  • Sura ya I ina sehemu 3 na Ibara 32
  • Sehemu ya I ina Ibara 5
  • Sehemu ya II ina Ibara 6
  • Sehemu ya III ina Ibara 12--32
  • Sura ya II ina sehemu 3 na Ibara 33 -61
  • Sehemu ya I ina Ibara 33 -46b
  • Sehemu ya II ina Ibara 47 --50
  • Sehemu ya III ina Ibara 51--61
  • Sura ya III ina sehemu 3
  • Sehemu ya I ina Ibara 62 – 65
  • Sehemu ya II ina Ibara 66 -- 83
  • Sehemu ya III ina Ibara 84—101
  • Sura ya IV ina sehemu 4
  • Ibara ya 102 - 107
  • Sura ya V ina sehemu 3
  • Sehemu ya I ina Ibara 107A – 107B
  • Sehemu ya II ina Ibara 108 – 111
  • Sehrmu ya IV ina ibara 112 – 115
  • Sehemu ya V ina Ibara ya 116 – 123
  • Sehemu ya VI ina ibara ya 124 –
  • Sehemu ya VII ina ibara ya 125 – 128
  • Sura ya sita ina sehemu 2
  • Sehemu ya 1 ia ibara ya 129 -131
  • Sehemu ya 2 ina ibara ya 132 –
  • Sura ya vii ina sehemu 2
  • Ibara ya 133 -144
  • Sura ya viii ibara 1145 -146
  • Sura ya ix ibara ya 147-148
  • Sura ya x ibara 149 -152

 

Katika kupitia maudhui tulibaini mgongano wa kikatiba kwa suala zima la Muungano.

 

 

MENGINEYO:

Haki asili ni ile inayoonekana, inayokuwepo, na inayotekelezeka (tuazaliwa nazo).

Ni haki ya kusikilizwa, kinyume na upendeleo, na kujua sababu ya maamuzi.

 

SIKU YA PILI

1: UTANGULIZI: MREJESHO WA MAFUNZO.

Tumeanza mafunzo mnamo saa 3:11 Kwa utangulizi wa mrejesho wa mafunzo ya siku ya kwanza na kujiwekea sheria zitakazotuongoza katika mafunzo.

2: MAFUNZO

(a)MADA YA KWANZA: MAJADILIANO - SURA YA 2 YA KATIBA KUHUSU RAISI

Kupitia makundi tumejadili yafuatayo kwa kuongozwa na katiba:-

  • Madaraka ya Raisi.
  • Kiapo cha Raisi.
  • Namna ya kuachia madaraka.
  • Kikomo cha Uraisi

Kwa kupitia katiba mawazo yafuatayo yaliwasilishwa kupitia vikundi :-

  • Nafasi zote za uteuzi zinazofanywa na Raisi zifanywe kwa uwazi na kuzingatia vigezo vya fani, elimu na uzoefu na zisiwe za kisiasa.
  • Kuna migongano ya kimamlaka na kimaslahi katika mihimili yote mitatu yaani Bunge, Serikali na Mahakama.
  • Nafasi zote za uteuzi zipitiswe na bodi/kamati maalum ya taasisi hizo za uteuzi na siyo kufanywa na Raisi peke yake. Makamishna, wakurugenzi wa wilaya, makatibu tawala mkoa na wilaya waombe kazi kulingana na sifa zao. Wenyeviti wa bodi wateuliwe na bodi zao.

Kwa ujumla nafasi za uteuzi zinazofanywa na Raisi zipunguzwe kwa kuzingatia maoni yaliyotangulia hapo juu.

  • Kuwe na kikomo na muda maalum wa kukasimisha madaraka kwani inapunguza uwajibikaji.
  • Nafasi ya Raisi iachwe bila kikomo cha kukasimu.
  • Kuwe na wagombea kupitia vyama vya siasa (chama kama wadhamini), lakini pia kuwe na mgombea binafsi(ili kutimiza haki ya kikatiba).
  • Matokeo ya Uraisi yapingwe mahakamani na kuwepo na muda wa kuchunguza malalamiko na uhalali wa matokeo ndipo kiapo kifuatie.
  • Iundwe mahakimu ya katiba itakayoshughulikia kesi zote za uchaguzi ikibainika tume ya uchaguzi iko hatiani ikabiliwe na adhabu.
  • Nafasi ya Raisi ikome pale nafasi za wabunge zinapokomea na ishirikiriwe na Jaji ili kuwe na uchaguzi huru na haki na kuondoa kujipendelea na kutumia dora vibaya.

(b)MADA YA PILI: HAKI

MAJADILIANO,

Mwezeshaji alianza kwa majadiliano ya makundi kwa kuwataka washiriki kuorodhesha Haki wanazozifaham. Baada ya majadiliano yafuatayo yaliwasilishwa:-

  • Haki ya Usawa.
  • Haki ya Kuishi .
  • Haki ya Uhuru wa mawazo.
  • Haki ya kufanya kazi.
  • Haki ya asili

Mwezeshaji alitushirikisha kupitia vitini kuwa:-

Haki ni ustahili au stahili wa kupata vitu au mambo ya msingi kwa kuzingatia maadili, taratibu za sheria na uhitaji wa msingi wa mwanadamu.

Haki ni stahili ya jumla ya jamii pasipo ubaguzi wa aina yoyote kwa misingi ya kabila, wadhifa, elimu n.k.

 

Misingi ya Haki:-

  • Hakuna kubwa wala ndogo, yenye umuhimu kuliko nyingine.
  • Kushiriki na kushirikishwa.
  • Uwajibikaji wa utawala wa kisheria.
  • Haki zina ingiliana na kutegemeana

Vyanzo viwili vya Haki:-

  • Sheria za nchi.
  • Kanuni za viwango vya maadili/

Haki na uwazi wa kupata taarifa mbalimbali kupata taarifa mbalimbali kupitia katiba, sheria za fedha za serikali za mitaa, kanuni za mipango na bajeti za serikali za mitaa,

(c)  MADA YA TATU: UTAWALA BORA.

Mwezeshaji alifafanua na kutoa vitini vyenye dhana ya Utawala Bora na kupitia baadhi ya vipengele vichache na kutaka washiriki kuvisoma ili tutakapo kutana kila mmoja awe na uelewa wa kutosha.

3: MENGINEYO:

(a)TUFANYE NINI:

Wawezshaji pamoja na washiriki waliweka mkakati kila mmoja afikishe elimu aliyoipata ya IJUE KATIBA NA HAKI YAKO kwa jamii zinazotuzunguka kwa kadri tutakavyoweza.Tutakapokutana kila mmoja awe na majina na idadi ya watu aliowajengea uwezo.

(b)TATHIMINI YA MAFUNZO:

Kila mshiriki alipewa fomu ya tathimini ya mafunzo ili kujaza na kuzikusanya kwa matumizi ya ofisi na wawezeshaji.

4: KUAHIRISHA MAFUNZO:

Mafunzo yaliahirishwa na mwenyekiti wa bodi saa 10:30 kwa kuwashukuru wawezeshaji na kila mmoja namna tulivyoshirikiana kwa pamoja kwa muda wa siku mbili.

 

                                                                                                            ___________________________                                     ___________________

                 Katibu                                                                           MWENYEKITI

 

 

 

 

RIPOTI YA MAFUNZO YA WANACHAMA WA ASASI LUALE – 06-07/09/2012

  1. UTAMBULISHO

Wajumbe waliohudhuria katika kikao walijitambulisha; muda ambao ulikuwa ni saa tatukamili asubuhi (03:00) ambao wajumbe wote walikuwa wamehudhuria.

  1. UFUNGUZI WA MAFUNZO

Mwenyekiti wa bodi alifungua mafunzo kwa kuwaelekeza wajumbe juu ya ujio wao ambao ulihusu; “IJUE KATIBA NA HAKI”. Kisha akawaeleza wajumbe kuhusu utaratibu mzima wa mafunzo haya ambayo yatachukuwa muda wa siku mbili yaani tarehe 6 na 7 mwezi wa 09/2012

  1. MAANA YA KATIBA
  • Mratibu aliwaeleza wajumbe kwa kuwataka watoe maana ya katiba
  • Pia mratibu alitoa majibu ya wajumbe na kasha kuchambua maana ya Katiba.
  • Alisema Katiba ni waraka wa kisheria unaotmika kuongoza taasisi au nchi, pia alisema kuwa Katiba ni
    • Sheria mama
    • Katiba ni roho ya nchi
    • Mratibu aliendelea kuwaeleza wajumbe historia ya Katiba kwa mfumo ufutao; na kwa kuzingatia miaka ambayo ilifanywa marekebisho:-
    • 1961           -           katiba ya uhuru
    • 1962           -           katiba ya Jamhuri
    • 1964           -           katiba ya Muungano
    • 1965           -           muda (katiba ya muda)
    • 1977           -           katiba ya kudumu
    • Pia aliendelea kueleza mabadiliko 14 ya katiba. Mabadiliko haya yalizingatia mambo matatu
      • Siasa – ongezeko la mahitaji ya kijamii
      • Mahitaji ya kiuchumi
      • Mabadiliko ya sayansi na teknolojia
    • 1979           -           mahakama ya rufaa
    • 1980          -           kero za muungano
    • 1980           -           kuweka sawa mfumo wa uchaguzi
    • 1982           -           kuboresha utaratibu wa uteuzi wa wakuu wa mikoa
    • 1984           -           kuingiza tamko la haki za binadamu (1948)
    • 1990           -           mgombea mmoja wa urais wa Zanzibar
    • 1992           -           chama kimoja (mfumo wa vyama vingi)
    • 1993           -           uchaguzi wa pamoja rais, wabunge na madiwani
    • 1994           -           mgombea mwenza wa urais
    • 1995          -           kiapo cha rais (yaani rais kuapishwa na jaji mkuu)
    • 2000           -           kumpa rais uwezo wa wananchi 10 kuwa wabunge na

na kuondoa kigezo cha 51% kuwa rais

  • 2005           -           20% - 30% viti maalum pia uhuru wa kuabudu, kushiriki

Maoni na kujieleza

           

 

MAMBO MUHIMU KATIKA KATIBA

-          Mratibu aliendelea kuwawezesha wajumbe kwa kuwauliza swali ambalo lilikuwa hivi: Taja mambo unayofikiri ni muhimu katika kuandika Katiba

-          Hapa mratibu aliwataka wajumbe wakae katika makundi na waweze kuandika maoni yao. Hivyo kila wajumbe walitoa maoni yao juu ya kile walichokuwa wamepewa kujadili

Mambo ambayo wajumbe waliyawasilisha ni:-

a)       Kikomo cha urais kipunguzwe

b)       Kupunguza madarka kwa rais

c)       Kukuza ustawi wa jamii (uwe wa watu wote)

d)       Haki za binadamu (binadamu wote ni sawa )

e)       Uchaguzi upatikane katika njia sahihi

f)        Ajira kwa vijana izingatiwe

g)       Amani ya nchi (vyama vya siasa vidumishe amani)

h)       Wastahili za watumishi kwa wakati (kuondoa migomo)

i)         Wakulima wapewe pembejeo kwa wakati kujali makundi mbalimbali

j)         Wanajeshi wasipewe ukuu wa mikoa wakati wa kustaafu

k)       Tume ya uchaguziisitawaliwe na rais

l)         Nafasi ya walemavu katika uongozi

m)     Katiba ifike kwa jamii

n)       Ardhi ibaki kuwa mali ya serikali

  • Serikali itumie rasilimali zetu katika kuendeleza jamii husika

-          Mratibu aliendelea kuelezea madaraka mbalimbali ya rais kwa mfano ni amiri jeshi mkuu, uteuzi wa wakuu wa mikoa, wilaya

-          Mratibu aliendelea kuwawezesha wanajamii kwa kuwataka wajadili swali lifuatalo, Jadili kama bado tunafuata misingi ya ujamaa na kama sio tuandike nini kwenye katiba yetu?

  • Wajumbe kujadili katika makundi na pia wakawasilisha mtazamo wao wa mawazo kuhusu misingi ya ujamaa, kulitokea makundi mawili yaliyokinzana - Kundi moja lilisema ujamaa na makundi matatu yalisema ubepari urudi.
  • Katika kipengele cha ujamaa waliomba katiba iweke wazi mambo yafuatayo:- kama uwazi, ukweli na uwajibikaji
  • Mratibu aliendele kuwawezesha wajumbe kwa kuwaelezea bunge, mahakama na dola. Pia mratibu alielezea zaidi kuhusu bunge na wajumbe walichangia mawazo

Kikao kilifungwa na mwenyekiti wa kikao saa kumi kamili (saa 10:00) kwa kuwashukuru wajumbe

 

 

 

RIPOTI YA MAFUNZO YA WANACHAMA WA ASASI LUALE – 07/09/2012

Kikao kilifunguliwa saa tatu kamili asubuhi (3:00) baada ya wajumbe kupata chai ya asubuhi.

Mwezeshaji alianza kwa kuwaeleza wajumbe hali ya muungano (yaani maana ya muungano) aliendelea kuwaeleza kwa kuwapa swali na kuwataka wajadili swali lifuatalo:- Je,muungano uendelee au uvunjwe, taja faida na hasara za kila upande

-          Wajumbe walitoa mawazo yaokisha majadiliano yaliendelea kila wajumbe kuchangia, waliendelea kuchangia kero mbalimbali za muungano; kama vile ukosefu wa mgawanyo sawa wa madaraka na rasilimali

-          Katiba iwe moja

-          Marais wawili

Pia mratibu aliendelea kueleza asili ya muungano kwa kuwashirikisha wajumbe walioshiriki

Mratibu aliwaeleza wajumbe kuwa muda wa chakula cha mchana, baada ya chakula cha mchana wajumbe walirudi tena kuendelea na mada.

Mwezeshaji aliendelea kwa kuwaeleza wajumbe kuwa ijue katiba na haki yako. Aliwaleleza wajumbe misingi ya haki kwa kujadiliana mawazo mbalimbali. Aliendelea kuelezea aina mbalimbali za haki, muwezeshaji aliendelea kuelezea ni namna gani ya kupata haki bila ubaguzi.

Mwezeshaji alitoa swali kwa washiriki kwa kuwataka wajadili kimakundi, aidha mratibu aliendelea kwa kutoa maswali juu ya baraza la mawaziri, swali lilikuwa kama ifuatavyo:- Je, ni veme tuendelee kuwa na baraza la mawaziri ambalo haliwashirikishi manaibu waziri?

Jadili iwapo manaibu waziri wanaongeza ukubwa wa baraza la mawaziri tu?

Wajumbe walishirikiana kimakundi kisha mratibu akatoa majumuisho ya mwisho.

Saa kumi kamili (10:00) jioni Mwenyekiti wa mafunzo alifunga kikao kwa kuwashukuru wajumbe na wawezeshaji kwa uvumilivu wa siku zote za mafunzo.

 

Imeandaliwa na:                                                                        Imeidhinishwa na :

Jina:_____________________________                     Jina:________________________________

Saini:____________________________                      Saini:______________________________

 

 

 

 

 

 

 

 

 

October 18, 2012
Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.