UZINDUZI WA
TOVUTI
Shirika la African Heritage Foundation nchini Tanzania limezindua rasmi Tovuti yake jana Tarehe 24,Mwezi wa nane 2010 hapa Ukonga Kata ya Kitunda.Tovuti hiyo ilizinduluwa na Bwana Emmanuel.R.Kapongo mwakilishi wa Jumuiya ya watanzania washio nchini Italia ''Communita Tanzaniana in Italia".Ambayo ni jumuiya rafiki wa A.H.F.Hafla hiyo ya uzinduzi ili hudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo nchini Tanzania,Katibu Mtendaji wa shirika hilo inchini Uingereza,Wanachama pamoja na waalimu na wanafunzi wa kituo maalum cha elimu kilicho chini ya shirika hilo.Pichani aliyekaa ni Bwana Emmanuel.R.Kapongo akizimdua Tovuti Kushoto kwake ni Bwana Paul Richard na aliyesimama ni Mkurugenzi wa A.H.F Inchini Tanzania Bwana Albert.T.Msafiri.Picha zingine chini wadau wa A.H.F waliohudhuria katika hafla hiyo.